Agano la Kale 2022
Desemba 5–11. Hagai; Zekaria 1–3; 7–14: “Utakatifu kwa Bwana”


“Desemba 5–11. Hagai; Zekaria 1–3; 7–14: ‘Utakatifu kwa Bwana,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)

“Desemba 5–11. Hagai; Zekaria 1–3; 7–14,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022

Picha
Hekalu la Laie Hawaii

Hekalu la Laie Hawaii

Desemba 5–11

Hagai; Zekaria 1–3; 7–14

“Utakatifu kwa Bwana”

Unapojifunza Hagai na Zekaria, tafakari jinsi unavyoweza kuwasaidia washiriki wa darasa kupata maana katika unabii huu.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki mistari kutoka Hagai na Zekaria ambayo walitafakari au kujadili na wengine wiki hii na kujadili jinsi gani msitari hii imewasaidia wao kusogea karibu na Bwana.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Hagai 1; 2:1–9

“Zitafakarini njia zenu.”

  • Ushauri katika Hagai 1 unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kufikiria kuhusu vipaumbele vyao. Unaweza kuwaalika wasome Hagai 1:1–7 na kutafuta jinsi watu katika Yerusalemu walikuwa wakishindwa kuweka kipaumbele kitu kile ambacho Bwana aliwataka wafanye. Ni mambo gani Bwana ametutaka sisi tuyape vipaumbele vya juu katika maisha yetu? Ni vitu gani vinaweza kutuvuruga tusifokasi kwa Baba wa Mbinguni na Mwokozi na vipaumbele vyao. Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu ambao umewasaidia wao “kutafakari njia [zao]” na vipaumbele vyao.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kufikiria jinsi wanavyoweza kufokasi zaidi kabisa katika vipaumbele vya Bwana, unaweza kuwaomba wapitie Hagai 2:1–9. Je, ni ushauri gani Bwana aliutoa ambao unaweza kutusaidia sisi kufanya kazi Yake? Washiriki wa darasa wangeweza kuelezea ni kwa namna gani wao wameweza kuweka vipaumbele vya Bwana kwanza katika maisha yao wanapokabiliana na majukumu yao mengine mengi muhimu. Je, Hagai 2:1–9 inafundisha nini kuhusu jinsi Bwana anavyotubariki sisi wakati tunapomweka kwanza katika maisha yetu? (ona pia “Nyenzo za Zaida”) Wape washiriki muda wa kuandika kile wamehisi kuongozwa kufanya kwa sababu ya majadiliano haya.

Zekaria 1–3; 7–8;14

Bwana anaweza kutufanya kuwa watakatifu.

  • Ili kuanza mjadala kuhusu utakatifu, mnaweza kusoma pamoja Zekaria 14:20–21. Washiriki wa darasa wangeweza kukielezea kirai hiki “Utakatifu kwa Bwana” kina maana gani kwao. Ni ushawishi gani unaweza kuwa juu ya watu kama wanaweza kuona kirai hiki “Utakatifu kwa Bwana” kimeandikwa kwenye kila chombo cha kila siku. Ni kwa jinsi gani kirai hiki kinatugusa kila tunapokiona kwenye mahekalu leo? Washiriki wa darasa wangeweza kusoma Zekaria 1:1–6; 3:1–7; 7:8–10; 8:16–17 na kujadili kitu ambacho wanajifunza kuhusu kuwa mtakatifu ina maana gani. Kwa nini utakatifu wetu binafsi ni muhimu kwa Bwana? Je, Yeye anatusaidiaje kuwa watakatifu?

  • Washiriki wa darasa wanaweza kupitia Zekaria 2:10–11; 8:1–8; 14:9–11, 20–21 na kushiriki misukumo yao kuhusu jinsi ambavyo ingekuwa kuishi pamoja na Mwokozi katika hali ya utakatifu. Je, kwa jinsi gani Bwana anataka kutuaandaa kuishi katika hali ambazo Zekaria alizoelezea? Ni kwa jinsi gani tunaweza kupata nguvu Zake ili kutusaidia kuwa watakatifu zaidi?

Picha
Kuingia kwa shangwe kwa Yesu katika Yerusalemu

“Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwana-punda, mtoto wa punda. (Zekaria 9:9). Kuingia kwa Shangwe, na Harry Anderson

Zekaria 9:9–11; 11:12–13; 12:10; 13:6–7

Yesu Kristo ndiye Masiya aliyeahidiwa.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuona muingiliano kati ya maneno ya Zekaria na maisha ya Mwokozi, kama vile watu katika nyakati za Yesu walivyofanya, unaweza kugawa darasa katika makundi mawili. Wape washiriki wa darasa katika kundi la kwanza mojawapo ya vifungu hivi: Zekaria 9:9–11; 11:12–13; 12:10; 13:6–7. Wape washiriki wa darasa katika lile kundi lingiine mojawapo ya vifungu hivi: Mathayo 21:1–11; 26:14–16; 26:31; Yohana19:37. Kila mshiriki wa darasa anaweza kujaribu kupata mtu kutoka katika kundi lingine ambaye ana kifungu cha maandiko kinachooana na chao. Je, tunajifunza nini kuhusu Mwokozi kutoka kwenye mistari hii?

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari Zekaria 9:9–11, ungeweza kuonyesha picha ya Mwokozi akiingia kwa shangwe Yerusalemu (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Nifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Onyesha video “The Lord’s Triumphal Entry into Jerusalem” (LDS.org). Washiriki wa darasa wanaweza kujadili jinsi ambavyo wangejisikia kuwa miongoni mwa watu wakimkaribisha Yesu mjini. Je, tunamkaribishaje Yeye katika maisha yetu, nyumbani mwetu, na katika jumuiya zetu.

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

“Zitafakarini njia zenu.”

Baada ya kunukuu Hagai 1:4–7, Mzee Terence M. Vinson alifundisha:

“Tunaweza kuhisi shangwe ya kudumu pale Mwokozi na injili Yake vinapokuwa mfumo ambao tunajenga maisha yetu. Hata hivyo, ni rahisi sana kwa mfumo huo kuwa, badala ya, mambo ya ulimwengu, ambapo injili hukaa kama pendeleo la ziada au kama kuhudhuria tu kanisani kwa masaa mawili Jumapili. Wakati hii inapokuwa hivi, inakuwa sawa na kuweka mishahara yetu katika “mfuko uliotoboka toboka.”

“Hagai anatuambia sisi tuwekee sharti.…

“Hakuna hazina, wala jambo lolote la kuburudisha, wala cheo chochote, wala mtandao wo wote wa kijamii, wala mchezo wo wote wa video, wala mchezo wo wote, wala muunganiko wo wote na mtu maarufu, wala cho chote duniani ambacho kina thamani zaidi kuliko uzima wa milele. Kwa hiyo ushauri wa Bwana kwa kila mtu ni “zitafakarini njia zenu’” (“Wanafunzi wa Kweli wa Mwokozi,” Ensign au Liahona, Nov. 2019, 9,11).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Sikiliza. Kusikiliza ni kitendo cha upendo. Njia moja ya kusikiliza kwa makini ni kumtazama mtu ambaye anaongea. Hii inatuwezesha kutambua mawasiliano yasiyo ya maneno. (Ona Kufundisha Katika Njia ya Mwokozi, 34.)

Chapisha