Agano la Kale 2022
Desemba 12–18. Malaki: “Nimewapenda Ninyi, Asema Bwana”


“Desemba 12–18. Malaki: ‘Nimewapenda Ninyi, Asema Bwana,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)

“Desemba 12–18. Malaki,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022

Picha
Sanamu ya Christus

Desemba 12–18

Malaki

“Nimewapenda Ninyi, Asema Bwana”

Baadhi ya vifungu katika Malaki vinaweza kuwa na umuhimu wa kipekee kwa darasa lako kujifunza. Unapojifunza, sali ili kutambua ni vifungu hivyo vinaweza ni gani. Kufanya hivi pia kutakusaidia kuhisi upendo ambao Bwana anao kwa ajili ya wale unaowafundisha.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Unaweza kuanza mjadala kuhusu kitabu cha Malaki kwa kuandika neno Ujumbe ubaoni. Wahimize washiriki wa darasa kushiriki ujumbe muhimu ambao wameupata katika kila sura ya Malaki. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kukumbuka na kutafakari kile kilichoshirikishwa unaweza kuandika vifungu hivyo vya maneno ubaoni.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Malaki 1:6–14.

Bwana anataka “dhabihu iliyo safi.”

  • Ili kuwahimiza washiriki wa darasa kuelezea kile walichojifunza kuhusu dhabihu kutoka katika Malaki 1:6–14, ungeweza kuwaalika kupitia mistari kimya kimya na kujadili na mshiriki mwingine wa darasa kitu ambacho makuhani Waisraeli hawakuelewa kuhusu dhabihu. Je, ni kwa nini Bwana hutaka kilicho bora kutoka kwetu? Washiriki wa darasa wangeweza kutengeneza orodha ya dhabihu au sadaka, tunazofanya kwa Bwana leo. Kwa kila kitu kilicho kwenye orodha, wanaweza kujadili ni kitu gani ambacho kinaweza kuifanya dhabihu kuwa “najisi” au “safi” (Malaki 1:7,11).

Malaki 3– 4

Unabii wa Malaki unatimizwa katika siku hizi za mwisho.

  • Ungeweza kuanza mjadala kuhusu Malaki 3–4 kwa kutaja kwamba Moroni alishiriki mistari katika sura hizi alipomtokea Joseph Smith (ona Joseph Smith—Historia 1:36–39). Ni ukweli gani katika sura hizi washiriki wa darasa wanaona huenda ulikuwa na umuhimu wa kipekee kwa Joseph—na kwetu sisi —kujua? Washiriki wa darasa wangejipanga katika vikundi vidogo vidogo na kuorodhesha ukweli mwingi kadiri wanavyoweza. Himiza makundi kushiriki orodha zao na kujadili kwa nini kweli hizi ni muhimu katika siku za mwisho.

Malaki 3:8–12.

Bwana hufungua madirisha ya mbinguni wakati sisi tunapolipa zaka zetu.

  • Ili kuwahimiza washiriki wa darasa kushiriki shuhuda zao za sheria ya zaka, ungeweza kuwaalika kutafuta kanuni katika Malaki 3:8–12 na kushiriki jinsi walivyokuja kujua kanuni hizi ni za kweli. Wanaweza kuzungumza kuhusu jinsi ambavyo Bwana amewabariki—kiroho na kimwili—kwa kulipa zaka. Au wanaweza kujadili masomo kuhusu zaka ambayo Mzee David A. Bednar alishiriki katika ujumbe wake “Madirisha ya Mbinguni” (Ensign au Liahona, Nov. 2013, 17–20) na kushiriki kile ambacho wamejifunza wanapojitahidi kuishi sheria hii.

  • Waombe washiriki wa darasa wasome Malaki 3:8–12 kimya kimya huku wakitafakari jinsi wanavyoweza kumfundisha mtu kwa nini Bwana anatutaka tulipe zaka. Wanaweza pia kusoma maelezo ya Rais Gordon B. Hinckley katika “Nyenzo za Ziada.” Je, tungependa wengine waelewe nini kuhusu zaka? Kwa mfano, Je, kulipa zaka maana yake ni nini? Je, ni kwa nini Bwana anataka sisi tuilipe? Je, ni kwa jinsi gani “madirisha ya mbinguni” (mstari wa 10) hufunguka tunapolipa zaka? Je ni shaka gani mtu angekuwa nayo kuhusu kulipa zaka, na tungemjibu namna gani? Waombe washiriki wa darasa kushiriki jinsi kutii amri hii kumeimarisha imani yao katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Picha
Eliya akiwatokea Joseph Smith na Oliver Cowdery katika Hekalu la Kirtland

Kielelezo cha Eliya akiwatokea Joseph Smith na Oliver Cowdery katika Hekalu la Kirtland, na Robert T Barrett

Malaki 4:5–6.

“Nitawapelekea Eliya nabii.”

  • Washiriki wa darasa wangeweza kupata umaizi wenye msaada kuhusu Malaki 4:5–6 kwa kulinganisha mistari hii na ile namna Moroni alivyoinukuu kwa Joseph Smith katika Joseph Smith—Historia 1:38–39. (Inaweza kusaidia kuwa na mtu akiandika mistari ya kila toleo sambamba ubaoni.) Maneno ya Moroni yanaongeza nini katika uelewa wetu wa mistari hii katika Malaki? Wangeweza pia kujadili maswali kama haya: Kina nani ndiyo “akina baba”? (ona Kumbukumbu la Torati 29:13). Ni kwa jinsi gani mioyo yetu inageuzwa kuwaelekea baba zetu, na mioyo yao hugeuzwaje kutuelekea sisi? Ili kusaidia darasa lako kuelewa jinsi unabii wa Malaki ulivyotimizwa, wanaweza kusoma kuhusu wakati ambapo Eliya alikabidhi funguo za kufunga kwa Joseph Smith (ona Mafundisho na Maagano 110:13–16). Kwa nini washiriki wa darasa wanashukuru funguo hizi zilirejeshwa?

  • Malaki 4:5–6 inatoa fursa kubwa ya kuzungumza kuhusu kazi ya hekalu na historia ya familia. Labda washiriki wa darasa wanaweza kushiriki uzoefu walio nao wakati walipokuwa wanafanya kazi hii na jinsi uzoefu huu ulivyowasaidia kuigeuza mioyo yao kwa baba zao. Je, tunaweza kufanya nini ili kusaidia kizazi kijacho kuigeuza mioyo yao kutuelekea sisi?

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Zaka suala la kiimani.

Rais Gordon B. Hinckley alisema, “Sisi tunaweza kulipa zaka zetu. Hii sio suala la fedha sana bali kwani ni suala la kiimani zaidi. Mimi sijapata mlipa zaka mwaminifu ambaye hawezi kushuhudia kwamba katika njia halisi na ya ajabu madirisha ya mbinguni yamefunguliwa na baraka kumiminwa juu yake” (“Acha Tusogeze Kazi Hii Mbele,” Ensign, Nov. 1985,85).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Elezeni mahangaiko yenu na imani yenu. Wakati mwingine watu ambao wanapitia majaribu hujihisi ni wapweke. Inaweza kuwa sahihi mara moja moja kushiriki uzoefu binafsi kuhusu wakati ambapo ulikuwa unahangaika na jinsi Mwokozi alivyokusaidia.

Chapisha