Vitabu vya Maelekezo na Miito
7.Uaskofu


“7. Uaskofu,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“7. Uaskofu “ Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla.

Picha
mtu akizungumza kwenye mimbari

7.

7.Uaskofu

7.1

Askofu na Washauri Wake

Askofu anashikilia funguo za ukuhani ili kuongoza kazi ya Kanisa katika kata (ona 3.4.1). Yeye na washauri wake wanaunda uaskofu.

Askofu ana majukumu makuu matano:

  • Yeye ndiye kuhani mkuu kiongozi katika kata.

  • Yeye ni rais wa Ukuhani wa Haruni.

  • Yeye ni mwamuzi wa wote.

  • Anaratibu kazi ya wokovu na kuinuliwa, ikijumuisha kuwajali wale wenye uhitaji.

  • Anasimamia rekodi, fedha, na matumizi ya nyumba ya mikutano.

Jukumu kubwa kuliko yote la askofu ni kwa kizazi kinachoinukia katika kata (watoto, vijana, na vijana wakubwa waseja). Ili kumwezesha kujikita kwenye jukumu hili, yeye ananaibisha majukumu mengi (ona 4.2.5).

7.1.1

Kuhani Mkuu Kiongozi

Askofu ni kiongozi wa msingi kiroho katika kata.

7.1.1.1

Vikundi katika Kata na Akidi za Ukuhani

Askofu ana wajibu kwa ajili ya Muungano wa Usaidizi na Vikundi vya Wasichana katika Kata. Anawapangia washauri wake jukumu la Shule ya Jumapili na kikundi cha Msingi na programu zingine katika kata.

Majukumu ya askofu kwa ajili ya akidi za Ukuhani wa Haruni yameelezwa kwa muhtasari katika 7.1.2. Majukumu yake kwa ajili ya akidi za wazee yameelezwa kwa muhtasari katika 8.3.1.

7.1.1.2

Ibada na Baraka

Askofu anaelekeza usimamizi wa ibada na baraka zifuatazo katika kata:

  • Sakramenti

  • Kuwapa majina na kuwabariki watoto

  • Ubatizo na uthibitisho kwa watoto umri wa miaka 8 watoto wa rekodi (kwa ajili ya waongofu, ona 31.2.3.2)

  • Utunukiaji wa Ukuhani wa Haruni,na utawazo kwenye ofisi za shemasi, mwalimu, na kuhani

7.1.1.3

Mabaraza na Mikutano

Askofu anaongoza baraza la kata na baraza la vijana katika kata (ona 29.2:5 ona 29.2.6).

Uaskofu unapanga mikutano ya sakramenti na mikutano mingine ya kata iliyoorodheshwa katika sura ya 29

7.1.1.4

Miito na Kupumzishwa

Majukumu ya askofu kwa ajili ya miito na kupumzisha yameelezwa kwa muhtasari katika sura ya 30.

7.1.2

Rais wa Ukuhani wa Haruni

Askofu ana majukumu yafuatayo kama rais wa Ukuhani wa Haruni katika kata. Washauri wake wanamsaidia.

  • Kusaidia wazazi katika kuwafundisha vijana.

  • Kusimamia akidi za Ukuhani wa Haruni na madarasa ya wasichana. Askofu ni rais wa akidi ya makuhani (ona Mafundisho na Maagano 107:87–88). Mshauri wake wa kwanza ana wajibu kwa ajili ya akidi ya walimu. Mshauri wake wa pili ana wajibu kwa ajili ya akidi ya mashemasi.

  • Anashauriana na rais wa wasichana katika kata.

  • Anakutana mara kwa mara na kila kijana.

7.1.3

Mwamuzi wa Wote

Askofu ni mwamuzi wa wote katika kata (ona Mafundisho na Maagano 107:71–74). Anayo majukumu yafuatayo:

  • Kuwasaidia vijana na watu wazima wastahili kwa ajili na kuwa na kibali cha hekaluni.

  • Kuendesha usaili kama inavyoelezwa kwa muhtasari katika 31.2

  • Kukutana na waumini wa kata wanaotafuta mwongozo wa kiroho, walio na matatizo mazito binafsi au waliofanya dhambi kubwa, kuwasaidia wachote nguvu ya uponyaji ya Yesu Kristo.

  • Chini ya maelekezo ya rais wa kigingi, kuendesha mabaraza ya uumini kama inavyohitajika. Kwa ajili ya mwongozo, ona sura ya 32.

7.1.4

Kuratibu Kazi ya Wokovu na Kuinuliwa

Askofu anaratibu kazi ya Wokovu na kuinuliwa katika kata (ona sura ya 1). Washauri wake na viongozi wengine wa kata wanamsaidia.

7.1.4.1

Kuongoza Juhudi za Kuwajali Wale Walio katika Shida.

Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi askofu anavyowajali Wale Walio katika Shida, ona 22.6.1.

7.1.5

Rekodi, Fedha, na Nyumba ya Mikutano

Kwa taarifa kuhusu rekodi, ona 3.4.33Sura ya 33. Kwa maelezo kuhusu utunzaji wa fedha, ona 4.2.34sura ya 34. Kwa taarifa kuhusu nyumba za mikutano, ona sura ya 35.

7.3

Katibu Mtendaji wa Kata na Katibu Mtendaji Msaidizi wa Kata

Askofu anampendekeza mwanamume anayeshikilia Ukuhani wa Melkizedeki kuhudumu kama katibu mtendaji wa kata.

Anayo majukumu yafuatayo:

  • Kukutana na askofu na kuandaa ajenda kama zilivyopangwa.

  • Kuhudumu kama mshiriki wa baraza la kata na kuhudhuria mikutano ya baraza la kata.

  • Kupanga miadi kwa ajili ya uaskofu.

7.4

Karani wa Kata na Makarani Wasaidizi wa Kata

Majukumu ya karani wa kata na makarani wasaidizi wa kata yameelezwa kwa muhtasari katika 33.4.2.

Chapisha