Watoto na Vijana
Mawazo kwa ajili ya Ukuaji katika Nyanja Zote za Maisha


“Mawazo kwa ajili ya Ukuaji katika Nyanja Zote za Maisha,” Maendeleo Binafsi: Kitabu cha Mwongozo cha Watoto (2019)

“Mawazo kwa ajili ya Ukuaji katika Nyanja Zote za Maisha,” Maendeleo Binafsi: Kitabu cha Mwongozo cha Watoto

Mawazo kwa ajili ya Ukuaji katika Nyanja Zote za Maisha

Kurasa zifuatazo zina mawazo ya jinsi unavyoweza kumfuata Mwokozi na kukua katika nyanja zote za maisha yako. Huitaji kutumia haya—mawazo mazuri zaidi yanaweza kuwa yako mwenyewe! Omba kuhusu kile unachoweza kukifanyia kazi sasa.

Unaweza kupata mawazo zaidi kwenye ChildrenandYouth.ChurchofJesusChrist.org.

Picha
kiroho, kijamii, kimwili, kiakili

Mawazo kwa ajili ya Ukuaji wa Kiroho

Ni nini Mawazo Yako?

Picha
kijana akiomba

Soma Kitabu cha Mormoni Kila Siku

Picha
kijana akisoma maandiko

Jenga tabia ya kusoma kila siku, hata kama ni mistari michache tu.

Jiandae Kwenda Hekaluni

Picha
kijana akiwa hekaluni

Jifunze na ishi “Viwango Vyangu vya Injili” (ukurasa wa 63), na waalike wengine kufanya vivyo hivyo.

Jifunze Makala za Imani

Picha
kijana akihesabu

Kariri Makala za Imani (ukurasa wa 62), na jifunze zinamaanisha nini.

Boresha maombi yako

Picha
kijana akisoma

Kabla ya kuomba, fikiria kuhusu kile ulicho na shukrani nacho na kile unachohitaji usaidizi nacho.

Mshukuru Baba wa Mbinguni kwa Baraka Zako

Picha
orodha ya vitu vya kufanya

Andika mambo matatu ambayo kwayo una shukrani. Jaribu kuandika mambo mapya matatu kila siku.

Itakase Siku ya Sabato

Picha
familia nje ya kanisa

Amua kile unachoweza kuanza kufanya au kuacha kufanya ili kuifanya siku ya Sabato iwe siku maalumu.

Mtumikie Mtu Mwingine

Picha
kijana akifanya usafi

Tafuta njia za kumsaidia mtu katika familia yako, shuleni, au kanisani.

Fanya Historia ya familia

Picha
bibi na babu

Andika barua kwa bibi na babu, shangazi, au mjomba. Waombe wakusimulie hadithi kuhusu wakati walipokuwa na umri sawa na wako.

Shiriki Injili

Picha
watu wakizungumza

Zungumza na rafiki kihusu injili. Mwalike rafiki yako kanisani au kwenye shughuli.

Fundisha Injili

Picha
familia ikisoma

Fundisha hadithi ya andiko unalolipenda kwa familia yako. Igiza au chora picha ili kukusaidia kufundisha.

Imba Wimbo wa Msingi

Picha
kijana akipiga gita

Imba pamoja na mwanafamilia. Gundua jinsi kusikiliza muziki mzuri kunavyokufanya uhisi.

Mawazo kwa ajili ya Kukua Kijamii

Ni nini Mawazo Yako?

Picha
kijana akiomba

Jifunze kuhusu Familia

Picha
familia ikitembea pamoja

Soma “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” na zungumza na wazazi wako kuhusu kile ulichojifunza.

Onyesha Upendo kwa Familia Yako

Picha
familia mezani

Fanya jambo zuri kwa ajili ya watu katika familia yako.

Wajumuishe Wengine

Picha
kijana akitembea

Tafuta njia za kutumia muda pamoja na au mtumikie mtu ambaye anaweza kuhisi kuachwa au ambaye anaweza kuhitaji urafiki wako.

Jifunze kuhusu Tamaduni Zingine

Picha
kijana akiwa na Ilama

Soma kuhusu tamaduni zingine, zungumza na watu kutoka nchi zingine, au nenda kwenye sherehe za kiutamaduni karibu nawe.

Watumikie Jirani Zako.

Picha
kijana akikunja nguo

Pamoja na wazazi au viongozi, fanya kitu katika jumuiya yako kuwasaidia watu wenye uhitaji.

Jifunze Kuomba Msamaha na Kusamehe

Picha
kijana mwenye jeraha

Igiza hali ambapo mtu anahitaji kuomba msamaha au kusamehe. Fanyia mazoezi jinsi ya kushiriki hisia zako na kujibu.

Jifunze kuhusu Jumuiya Yako

Picha
kijana nje ya mahakama

Tembelea kituo cha polisi, kituo cha moto, au huduma nyingine za jumuiya. Jifunze kuhusu nini wanafanya, na washukuru kwa huduma yao.

Tafuta Rafiki Mpya

Picha
vijana kwenye bembea

Jitambulishe kwa mtu mgeni, na mualike mtu huyo kucheza na wewe.

Zungumza Maneno ya Ukarimu

Picha
Katuni ya uso wa furaha

Fanyia mazoezi kutumia maneno ambayo yangemfanya mtu kuwa na furaha, si huzuni. Zungumza kuhusu kile unachoweza kusema ikiwa mtu anasema maneno yasiyo ya ukarimu kwako.

Zuia Hasira Yako

Picha
kijana mwenye hisia pinzani

Fanyia mazoezi kutulia wakati unapohisi hasira. Kwa mfano, vuta pumzi ndefu, hesabu mpaka 10, au fikiria upo mahala unapopapenda.

Wakaribishe Wengine

Picha
vijana wakizungumza

Jitambulishe kwa mtu mgeni katika shule yako, ujirani wako, au kata au tawi. Msaidie mtu huyu kukutana na watu wengine.

Mawazo kwa ajili ya Ukuaji Kimwili

Ni nini Mawazo Yako?

Picha
kijana akiomba

Jifunze Kupika

Picha
kijana akipika

Saidia kuandaa chakula chenye afya au asusa. Shiriki chakula hicho pamoja na familia yako na marafiki.

Uweke Mwili wako Imara

Picha
kijana akifanya mazoezi

Fanya jambo mara kwa mara kusogeza mwili wako, kama michezo, kudansi, kufanya mazoezi, au kucheza nje.

Onesha Heshima kwa Mwili Wako

Picha
kijana akipiga mswaki na kuchana nywele

Weka mwili wako safi kila siku. Oga kila mara. Piga mswaki na tunza nywele zako kila siku.

Tunza Nyumba Yako

Picha
kijana akikusanya uchafu

Fanya jambo kusaidia kuifanya nyumba yako mahala pazuri pa kuishi, kama vile kusafisha, kupamba, au kazi ya ua.

Tunza Vizuri Vitu Unavyomiliki

Picha
kijana akipanga vitu vyake

Waombe wazazi wako wakufundishe jinsi ya kurekebisha au kutunza vitu unavyotumia.

Jifunze Ujuzi Mpya wa Sanaa

Picha
kijana akipaka rangi

Chora, paka rangi, au tengeneza picha, na mpe mtu unayempenda.

Jifunze Ujuzi Mpya wa Muziki

Picha
kijana akipiga gitaa

Jifunze jinsi ya kuimba wimbo, kupiga ala, au kuongoza muziki. Jitolee kushiriki ujuzi wako katika jioni ya familia au shughuli nyingine.

Tii Neno la Hekima

Picha
kijana akifikiria kuhusu asusa

Soma Mafundisho na Maagano 89 kuona kile Baba wa Mbinguni anachoahidi ikiwa unatii Neno la Hekima. Amua jinsi unavyoweza kuliishi vyema.

Furahia Muda Mbali na Nyumbani

Picha
Familia ikipanda mlima

Nenda kwenye matembezi au panda mlima pamoja na familia na marafiki ili kuchunguza ulimwengu unaokuzunguka.

Shiriki Talanta Zako

Picha
watu wakipiga tarumbeta

Shiriki mojawapo ya talanta zako pamoja na mtu mwingine ambaye yuko mpweke.

Jiandae kwa Dharura

Picha
watu wakiangalia ramani

Tengeneza mpango pamoja na wazazi au viongozi wako kwa ajili ya nini cha kufanya katika dharura.

Mawazo kwa ajili ya Kukua Kiakili

Ni nini Mawazo Yako?

Picha
kijana akiomba

Jifunze kuhusu Zaka

Picha
kijana akilipa zaka

Jifunze kwa nini ni muhimu kulipa zaka. Toa asilimia kumi ya pato lako kwa Bwana.

Boresha Ujuzi Wako wa Kujifunza

Picha
mama na binti wakisoma

Soma kitabu kuhusu mada mpya, au soma kitabu ambacho ni kirefu kuliko yalivyo mazoea yako ya kusoma.

Jifunze Jinsi ya Kuwa Salama Mtandaoni

Picha
familia ikitumia kompyuta

Tengeneza orodha ya sheria za familia yako kwa ajili ya kutumia intaneti au apps.

Jifunze Jambo Jipya

Picha
kijana akisoma

Chagua jambo unalovutiwa nalo, na jifunze kila kitu unachoweza kulihusu.

Hudhuria au Angalia Matukio ya Kiutamaduni

Picha
watu kwenye makumbusho

Tembelea makumbusho au tukio la kiutamaduni katika eneo lako. Zungumza na rafiki zako au familia kuhusu jambo jipya ulilojifunza.

Jifunze kuhusu Kazi Tofauti

Picha
watu wakitengeneza gari

Mtembelee mtu unayemfahamu kwenye kazi yao ili kujifunza kile wanachofanya na jinsi mambo yanavyoenda.

Jifunze kuhusu Watu Unaovutiwa Nao

Picha
watu wakizungumza

Huyu angeweza kuwa mtu unayemjua au mtu kutoka kwenye historia au maandiko. Amua jinsi unavyoweza kuwa zaidi kama wao.

Jifunze Jinsi ya Kufanya Chaguzi Nzuri

Picha
chati, sababu na matokeo

Chaguzi zote zina matokeo, ambayo ni mambo yanayotokea kama matokeo ya kile unachofanya. Tengeneza orodha ya baadhi ya chaguzi na matokeo yake.

Boresha kumbukumbu yako

Picha
mtu akifikiria

Kariri andiko unalolipenda, shairi, au wimbo.

Jifunze Lugha Mpya

Picha
kijana akitumia simu janja

Jifunze kusema halo na maneno mengine muhimu katika lugha nyingine. Fanya mazoezi pamoja na mtu mwingine anayezungumza lugha hiyo, kama inawezekana

Andika Hadithi

Picha
kijana akiandika

Andika hadithi kuhusu maisha yako au kuhusu mwanafamilia.

Chapisha