Watoto na Vijana
Viwango Vyangu vya Injili


“Viwango Vyangu vya Injili,” Maendeleo Binafsi: Kitabu cha Mwongozo cha Watoto (2019)

“Viwango Vyangu vya Injili,” Maendeleo Binafsi: Kitabu cha Mwongozo cha Watoto

Viwango Vyangu vya Injili

Viwango vya injili hukusaidia kutenda katika njia ambazo Yesu angetenda. Vinaweza kukupa mawazo kwa ajili ya shughuli mpya za kupanga au kufanya.

  • Nitafuata mpango wa Baba wa Mbinguni kwa ajili yangu.

  • Nitakumbuka agano langu la ubatizo na kumsikiliza Roho Mtakatifu.

  • Nitachagua mema. Ninajua ninaweza kutubu ninapofanya kosa.

  • Nitakuwa mwaminifu kwa Baba wa Mbinguni, kwa wengine, na kwangu mwenyewe.

  • Nitatumia majina ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kwa heshima.

  • Sitaapa au kutumia maneno machafu.

  • Nitafanya mambo yale katika siku ya Sabato ambayo yatanisaidia kuhisi kuwa karibu na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

  • Nitawaheshimu wazazi wangu na kufanya sehemu yangu ili kuimarisha familia yangu.

  • Nitayaweka mawazo yangu na mwili wangu katika hali ya utakatifu na safi, na sitatumia vitu ambavyo ni hatari kwangu.

  • Nitavaa kwa staha ili kuonesha heshima kwa Baba wa Mbinguni na kwangu mwenyewe.

  • Nitasoma, nitaangalia, na kusikiliza mambo ambayo yanampendeza Baba wa Mbinguni.

  • Nitasikiliza muziki ambao unampendeza tu Baba wa Mbinguni.

  • Nitatafuta marafiki wazuri na kuwatendea wengine kwa ukarimu.

  • Nitaishi sasa ili kustahili kwenda hekaluni na kufanya sehemu yangu kuwa na familia ya milele.

Chapisha