Watoto na Vijana
Wewe ni Mtoto wa Thamani wa Mungu


“Wewe ni Mtoto wa Thamani wa Mungu,” Maendeleo Binafsi: Kitabu cha Mwongozo cha Watoto (2019)

“Wewe ni Mtoto wa Thamani wa Mungu,” Maendeleo Binafsi: Kitabu cha Mwongozo cha Watoto

Wewe ni Mtoto wa Thamani wa Mungu

Mwanzo uliishi na Baba wa Mbinguni, ambaye anajua kila kitu na anampenda kila mtu. Yeye anataka wewe uwe kama Yeye! Yeye amekupatia mwili, uwezo, na vipawa vya kiroho. Anataka wewe na watoto Wake wote kugundua na kuendeleza vipawa hivi. Ametupatia mpango ili kutusaidia kuwa na furaha na kuwabariki wengine.

mbingu na familia

Ulikuja duniani kutoka mbinguni. Wewe ni sehemu ya familia.

ubatizo

Uliahidi kumfuata Yesu Kristo wakati ulipobatizwa na wakati unapopokea sakramenti.

uthibitsho

Unapothibitishwa, unapokea kipawa cha Roho Mtakatifu ili kukuongoza.

watu nje ya jengo la kanisa

Unaweza kupata shangwe na amani wakati unapochagua kuishi kama ambavyo Yesu angeishi.

watu wakifanya shughuli

Unaweza kujifunza na kukua. Unaweza kuwapenda na kuwatumikia wengine, kama ambavyo Yesu angefanya.

Yesu akiwafundisha watu

Baba wa Mbinguni alimtuma Mwanawe, Yesu Kristo, kuwa mfano na kufanya iwezekane kwako kutubu na kubadilika.

familia nje ya hekalu

Unaweza kufanya maagano hekaluni ambayo yatakuwezesha kuishi na Baba wa Mbinguni tena.