Mlango wa 1Lehi atoa unabii kuhusu nchi ya uhuru—Uzao wake utatawanywa na kuchapwa kama utamkataa yule Mtakatifu wa Israeli—Anawasihi wanawe wajivike mavazi ya silaha ya haki. Karibia mwaka 588–570 K.K. Mlango wa 2Ukombozi unatokana na Masiya Mtakatifu—Uhuru wa kuamua ni muhimu kwa kuishi na kwa maendeleo—Adamu alianguka ili wanadamu wawe—Wanadamu wako huru kuchagua uhuru na uzima wa milele. Karibia mwaka 588–570 K.K. Mlango wa 3Yusufu akiwa Misri aliona Wanefi kwenye ono—Alitoa unabii kuhusu Joseph Smith, mwonaji wa siku za mwisho; kuhusu Musa, ambaye atakomboa Israeli; na kutokea kwa Kitabu cha Mormoni. Karibia mwaka 588–570 K.K. Mlango wa 4Lehi anashauri na kubariki uzao wake—Anafariki na kuzikwa—Nefi anashangilia wema wa Mungu—Nefi anamwamini Bwana milele. Karibia mwaka 588–570 K.K. Mlango wa 5Wanefi wajitenga kutoka kwa Walamani, wanatii sheria ya Musa, na kujenga hekalu—Kwa sababu ya kutoamini kwao, Walamani wanaondolewa kutoka uwepo wa Bwana, wanalaaniwa, na wanakuwa mjeledi kwa Wanefi. Karibia mwaka 588–559 K.K. Mlango wa 6Yakobo aeleza historia ya Wayahudi: Uhamisho wa Kibabilonia na marejeo; huduma na kusulubiwa kwa yule Mtakatifu wa Israeli; msaada uliopokelewa kutokana na Wayunani; na uamsho wa siku za mwisho kwa Wayahudi watakapomwamini Masiya. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 7Yakobo anaendelea kusoma kutoka katika Isaya: Isaya azungumza kimasiya—Masiya atakuwa na ulimi wa aliyeelimika—Atawapa mgongo Wake wale wampigao—Hatafadhaishwa—Linganisha Isaya 50. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 8Yakobo anaendelea kusoma kutoka katika Isaya: Katika siku za mwisho, Bwana ataifariji Sayuni na kukusanya Israeli—Waliokombolewa watakuja Sayuni kwa shangwe kuu—Linganisha Isaya 51 na 52:1–2. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 9Yakobo anaelezea kwamba Wayahudi watakusanywa katika nchi zao zote za ahadi—Upatanisho ni ukombozi wa mwanadamu kutokana na Anguko—Miili ya wafu itafufuka kutoka kaburini, na roho zao zitatoka jehanamu na peponi—Watahukumiwa—Upatanisho unaokoa kutokana na kifo, jehanamu, ibilisi na mateso yasiyo na mwisho—Wenye haki wataokolewa katika ufalme wa Mungu—Adhabu ya dhambi yaelezwa—Yule Mtakatifu wa Israeli ni mlinzi wa mlango. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 10Yakobo anaeleza kwamba Wayahudi watamsulubisha Mungu wao—Watatawanywa mpaka waanze kumwamini Yeye—Marekani itakuwa nchi ya uhuru ambako hakuna mfalme yeyote atakayetawala—Jipatanisheni na Mungu na pokeeni wokovu kwa neema Yake. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 11Yakobo alimwona Mkombozi wake—Sheria ya Musa inamwakilisha Kristo na kuthibitisha kwamba Yeye atakuja. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 12Isaya anaona hekalu la siku za mwisho, kusanyiko la Israeli, na hukumu ya milenia na amani—Walio na kiburi na waovu watashushwa chini katika Ujio Wake wa Pili—Linganisha Isaya 2. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 13Yuda na Yerusalemu zitaadhibiwa kwa sababu ya maasi yao—Bwana hutetea na huhukumu watu Wake—Mabinti wa Sayuni wanalaaniwa na kusumbuliwa kwa sababu ya kupenda anasa—Linganisha Isaya 3. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 14Sayuni na mabinti zake watakombolewa na kutakaswa katika siku ya milenia—Linganisha Isaya 4. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 15Shamba la mizabibu la Bwana (Israeli) litakuwa lenye ukiwa, na watu Wake watatawanywa—Shida zitawajia katika hali yao ya ukengeufu na hali ya kutawanyika—Bwana atainua bendera na kuwakusanya Israeli—Linganisha Isaya 5. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 16Isaya anamwona Bwana—Isaya anasamehewa dhambi zake—Anaitwa kutoa unabii—Anatoa unabii kuhusu kukataliwa kwa mafundisho ya Kristo na Wayahudi—Baki litarejea—Linganisha Isaya 6. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 17Efraimu na Shamu wanashambulia Yuda—Kristo atazaliwa na Bikira—Linganisha Isaya 7. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 18Kristo atakuwa kama jiwe la kujikwaa na mwamba wa kuchukiza—Mtafute Bwana, sio mlio wa wachawi—Tegemea sheria na ushuhuda kwa maongozo—Linganisha Isaya 8. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 19Isaya anazungumza kiumasiya—Watu wale walio gizani wataona nuru kuu—Kwetu sisi mtoto amezaliwa—Atakuwa Mwana Mfalme wa Amani na atatawala kwenye kiti cha enzi cha Daudi—Linganisha Isaya 9. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 20Maangamizo ya Ashuru ni kielelezo cha maangamizo ya waovu wakati wa Ujio Wake wa Pili—Watu wachache watasalia baada ya Bwana kurudi—Baki la Yakobo litarejea katika siku ile—Linganisha Isaya 10. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 21Shina la Yese (Kristo) litahukumu kwa haki—Elimu ya Mungu itafunika dunia katika Milenia—Bwana atainua bendera na kukusanya Israeli—Linganisha Isaya 11. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 22Katika siku ile ya milenia watu wote watamsifu Bwana—Ataishi miongoni mwao—Linganisha Isaya 12. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 23Maangamizo ya Babilonia ni mfano wa maangamizo katika wakati wa Ujio wa Pili—Itakuwa siku ya ghadhabu na kulipiza kisasi—Babilonia (ulimwengu) itaanguka milele—Linganisha Isaya 13. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 24Israeli itakusanywa na kufurahia pumziko la Milenia—Lusiferi alifukuzwa kutoka mbinguni kwa sababu ya maasi—Israeli itashinda Babilonia (ulimwengu)—Linganisha Isaya 14. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 25Nefi anautukuza unyoofu—Unabii wa Isaya utafahamika katika siku za mwisho—Wayahudi watarejea kutoka Babilonia, watamsulubu Masiya, na watatawanywa na kuadhibiwa—Watarudishwa wakimwamini Masiya—Atakuja kwanza miaka mia sita tangu Lehi aondoke Yerusalemu—Wanefi wanatii sheria ya Musa na kumwamini Kristo, aliye Mtakatifu wa Israeli. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 26Kristo atawahudumia Wanefi—Nefi anaona mbele maangamizo ya watu wake—Watazungumza kutoka mavumbini—Wayunani watajenga makanisa ya bandia na makundi maovu ya siri—Bwana anawakataza wanadamu wasifanye ukuhani wa uongo. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 27Giza na ukengeufu yataufunika ulimwengu katika siku za mwisho—Kitabu cha Mormoni kitatokea—Mashahidi watatu watakishuhudia kitabu—Mtu aliyeelimika atasema hawezi kukisoma kitabu kilichotiwa muhuri—Bwana atatenda kazi kuu na ya maajabu—Linganisha Isaya 29. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 28Makanisa mengi ya bandia yatajengwa katika siku za mwisho—Yatafundisha mafundisho ya uwongo, yasiyofaidi, na ya kipumbavu—Ukengeufu utaendelea kwa sababu ya walimu wa bandia—Ibilisi atavuma katika mioyo ya wanadamu—Atafundisha kila aina ya mafundisho ya uwongo. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 29Wayunani wengi watakataa Kitabu cha Mormoni—Watasema, Hatuhitaji Biblia zaidi—Bwana huzungumzia mataifa mengi—Atahukumu ulimwengu kutoka vitabu vitakavyoandikwa. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 30Wayunani walioongoka watahesabika kuwa watu wa maagano—Walamani wengi na Wayahudi wataliamini neno na kuwa wema—Israeli itarudishwa na walio waovu kuangamizwa. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 31Nefi anaeleza ni kwa nini Kristo alibatizwa—Wanadamu lazima wamfuate Kristo, wabatizwe, wampokee Roho Mtakatifu, na wavumilie hadi mwisho ili waokolewe—Toba na ubatizo ndiyo lango la kuingia katika njia ile nyembamba na iliyosonga—Uzima wa milele huja kwa wale wanaotii zile amri baada ya ubatizo. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 32Malaika wanazungumza kwa uwezo wa Roho Mtakatifu—Wanadamu lazima wasali na kupokea ufahamu kwa wao wenyewe kutoka kwa Roho Mtakatifu. Karibia mwaka 559–545 K.K. Mlango wa 33Maneno ya Nefi ni ya kweli—Yanamshuhudia Kristo—Wale ambao wanamwamini Kristo wataamini maneno ya Nefi, ambayo yatasimama kama shahidi mbele ya baraza la hukumu. Karibia mwaka 559–545 K.K.