Mlango wa 1Amaroni anamuelemisha Mormoni kuhusu maandishi matakatifu—Vita vinaanza miongoni mwa Wanefi na Walamani—Wale Wanefi watatu wanaondelewa—Uovu, kutoamini, uchawi, na ulozi unaenea. Karibia mwaka 321–326 B.K. Mlango wa 2Mormoni anaongoza majeshi ya Wanefi—Damu na mauaji yanajaa katika nchi—Wanefi wanalia na kuomboleza kwa huzuni ya waliolaaniwa—Siku yao ya neema imeisha—Mormoni anapata mabamba ya Nefi—Vita vinaendelea. Karibia mwaka 327–350 B.K. Mlango wa 3Mormoni anawasihi Wanefi watubu—Wanapata ushindi mkuu na kujisifu kwa nguvu zao—Mormoni anakataa kuwaongoza, na sala zake kwa niaba yao hazina imani—Kitabu cha Mormoni kinawakaribisha makabila kumi na mawili ya Israeli kuamini injili. Karibia mwaka 360–362 B.K. Mlango wa 4Vita na mauaji vinaendelea—Wale waovu wanawaadhibu wale walio waovu—Uovu mkuu unaenea kuliko mbeleni katika Israeli yote—Wanawake na watoto wanatolewa kafara kwa sanamu—Walamani wanaanza kuwaangamiza Wanefi walio mbele yao. Karibia mwaka 363–375 B.K. Mlango wa 5Mormoni tena anayaongoza majeshi ya Wanefi katika vita vya damu na mauaji—Kitabu cha Mormoni kitakuja mbele kusadikisha Israeli yote kwamba Yesu ni Kristo—Kwa sababu ya kutoamini kwao, Walamani watatawanyika, na Roho itawaacha kukaa nao—Watapokea injili kutoka kwa Wayunani katika siku za baadaye. Karibia mwaka 375–384 B.K. Mlango wa 6Wanefi wanajikusanya kwenye nchi ya Kumora kwa vita vya mwisho—Mormoni anaficha maandishi matakatifu katika kilima cha Kumora—Walamani wanashinda, na taifa la Wanefi linaangamizwa—Mamia ya maelfu wanachinjwa kwa upanga. Karibia mwaka 385 B.K. Mlango wa 7Mormoni anawaalika Walamani wa siku za mwisho kuamini katika Kristo, waikubali injili Yake, na waokolewe—Wote wanaoiamini Biblia pia wataamini Kitabu cha Mormoni. Karibia mwaka 385 B.K. Mlango wa 8Walamani wanawawinda na kuwaangamiza Wanefi—Kitabu cha Mormoni kitajitokeza kwa uwezo wa Mungu—Shida zinatamkwa juu ya wale ambao wanatoa nje ghadhabu na mzozo dhidi ya kazi ya Bwana—Maandishi ya Wanefi yatatokea mbele katika siku ya uovu, uharibifu, na ukengeufu. Karibia mwaka 400–421 B.K. Mlango wa 9Moroni anawahimiza wale ambao hawaamini katika Kristo watubu—Anamtangaza Mungu wa miujiza, ambaye hutoa unabii na anayetoa vipawa na ishara juu ya waumini—Miujiza hukoma kwa sababu ya kutoamini—Ishara hutolewa kwa wale ambao huamini—Watu wanashauriwa kuwa na busara na kutii amri. Karibia mwaka 401–421 B.K.