Mlango wa 1Pahorani wa pili anakuwa mwamuzi mkuu na anauawa na Kishkumeni—Pakumeni anachukua kiti cha hukumu—Koriantumuri anaongoza majeshi ya Walamani, anateka Zarahemla, na anamuua Pakumeni—Moroniha anawashinda Walamani na kuteka tena Zarahemla, na Koriantumuri anauawa. Karibia mwaka 52–50 K.K. Mlango wa 2Helamani, mwana wa Helamani, anakuwa mwamuzi mkuu—Gadiantoni anaongoza kikundi cha Kishkumeni—Mtumishi wa Helamani anamuua Kishkumeni, na kundi la Gadiantoni linatorokea nyikani. Karibia mwaka 50–49 K.K. Mlango wa 3Wanefi wengi wanahamia kwenye nchi iliyopo kaskazini—Wanajenga nyumba za saruji na wanaandika kumbukumbu nyingi—Maelfu wanaongoka na kubatizwa—Neno la Mungu linawaongoza watu kwenye wokovu—Nefi mwana wa Helamani anachukua kiti cha hukumu. Karibia mwaka 49–39 K.K. Mlango wa 4Wanefi walioasi na Walamani wanaunganisha majeshi na kuteka nchi ya Zarahemla—Kushindwa kwa Wanefi kunatokea kwa sababu ya uovu wao—Kanisa linafifia, na watu wanakuwa dhaifu kama Walamani. Karibia mwaka 38–30 K.K. Mlango wa 5Nefi na Lehi wanajitoa wenyewe kuhubiri—Majina yao yanawakumbusha kuishi maisha mazuri kama babu zao—Kristo anakomboa wale ambao wanatubu—Nefi na Lehi wanapata waongofu wengi na wanafungwa gerezani, na moto unawazingira—Wingu la giza linawafunika watu mia tatu—Ardhi inatetemeka, na sauti inawaamrisha watu watubu—Nefi na Lehi wanaongea na malaika, na umati unazingirwa na moto. Karibia mwaka 30 K.K. Mlango wa 6Walamani walio wenye haki wanawahubiria wale Wanefi waovu—Watu wote wanafanikiwa wakati wa enzi ya amani na neema—Lusifa, mwanzilishi wa dhambi, huchochea mioyo ya waovu na wezi wa Gadiantoni katika uuaji na uovu—Wezi wanachukua serikali ya Wanefi. Karibia mwaka 29–23 K.K. Mlango wa 7Nefi anakataliwa kaskazini na anarudi Zarahemla—Anaomba juu ya mnara ulio ndani ya bustani yake na anawaambia watu watubu au waangamie. Karibia mwaka 23–21 K.K. Mlango wa 8Waamuzi wabaya wanataka kuchochea watu dhidi ya Nefi—Ibrahimu, Musa, Zeno, Zenoki, Ezia, Isaya, Yeremia, Lehi, na Nefi wote walimshuhudia Kristo—Kwa maongozi ya Mungu Nefi anatangaza uuaji wa mwamuzi mkuu. Karibia mwaka 23–21 K.K. Mlango wa 9Wajumbe wanapata mwamuzi mkuu amekufa kwenye kiti cha hukumu—Wanawekwa gerezani na baadaye wanaachiliwa—Kwa maongozi ya Mungu, Nefi anamtambua Seantumu kama muuaji—Nefi anakubaliwa na baadhi yao kama nabii. Karibia mwaka 23–21 K.K. Mlango wa 10Bwana anampatia Nefi, uwezo wa kuidhinisha—Anawezeshwa kufunga na kufungua duniani na mbinguni—Anaamrisha watu watubu au sivyo waangamie—Roho inambeba kutoka umati hadi mwingine. Karibia mwaka 21–20 K.K. Mlango wa 11Nefi anamshawishi Bwana kurudisha njaa badala ya vita vyao—Watu wengi wanaangamia—Wanatubu, na Nefi anaomba Bwana alete mvua—Nefi na Lehi wanapata ufunuo mwingi—Wezi wa Gadiantoni wanajiweka katika nchi. Karibia mwaka 20–6 K.K. Mlango wa 12Wanadamu si waaminifu na ni wapumbavu na ni wepesi kutenda maovu—Bwana huwarudi watu Wake—Ubure wa wanadamu unalinganishwa na uwezo wa Mungu—Katika siku ya hukumu, watu watapata maisha yasiyo na mwisho au laana isiyo na mwisho. Karibia mwaka 6 K.K. Mlango wa 13Samweli Mlamani anatabiri kuangamizwa kwa Wanefi isipokuwa watubu—Hao na utajiri wao wanalaaniwa—Wanakataa na kuwapiga manabii kwa mawe, wanazingirwa na pepo mbaya, na wanatafuta furaha kwa kutenda uovu. Karibia mwaka 6 K.K. Mlango wa 14Samweli anatabiri kwamba kutakuwa na mwangaza wakati wa usiku na nyota mpya wakati Kristo atakapozaliwa—Kristo anakomboa watu kutokana na kifo cha kimwili na cha kiroho—Ishara za kifo Chake zitajumuisha siku tatu za giza, kupasuka kwa miamba, na mabadiliko makubwa ya ulimwengu. Karibia mwaka 6 K.K. Mlango wa 15Bwana aliwarudi Wanefi kwa sababu Yeye aliwapenda—Walamani walioongoka wako imara na thabiti katika imani—Bwana atakuwa na huruma kwa Walamani katika siku za mwisho. Karibia mwaka 6 K.K. Mlango wa 16Wanefi ambao wanamwamini Samweli wanabatizwa na Nefi—Samweli hawezi kuuawa kwa mishale na mawe ya Wanefi ambao hawajatubu—Wengine wanashupaza mioyo yao, na wengine wanawaona malaika—Wasiosadiki wanasema hakuna maana ya kuamini katika Kristo na kuja Kwake katika Yerusalemu. Karibia mwaka 6–1 K.K.