2. Palmyra-Manchester, New York, 1820–1831
-
Nyumba ya Magogo ya Joseph Smith Mkubwa Malaika Moroni alimtokea Joseph Smith katika chumba cha orofani cha nyumba hii mnamo 21–22 Septemba 1823 (ona JS—H 1:29–47).
-
Shamba la Joseph Smith Mkubwa Shamba hili la hekta 40 liliendelezwa na familia ya Smith tangu mwaka 1820 hadi 1829.
-
Kijisitu Kitakatifu Ono la Kwanza la Joseph Smith Mdogo lilitokea katika eneo hili la miti katika shamba la Smith mapema katika majira ya kuchipua ya mwaka 1820 (ona JS—H 1:11–20).
-
Nyumba ya Mbao ya Joseph Smith Mkubwa Nyumba hii ilianza kujengwa katika mwaka 1822 na Alvin Smith, na ilikaliwa na familia ya Smith tangu 1825 hadi 1829.
-
Kilima Kumora Hapa malaika Moroni alimpa Nabii Joseph Smith mabamba ya dhahabu mnamo 22 Septemba 1827 (ona JS—H 1:50–54, 59).
-
Shamba la Martin Harris Shamba hili liliwekwa rehani na sehemu ya eneo lake liliuzwa ili kulipia gharama za kupiga chapa Kitabu cha Mormoni.
-
Kiwanda cha Kupigia Chapa cha E. B. Grandin Nakala 5000 za Kitabu cha Mormoni zilipigwa chapa hapa mwaka 1829–1830.
-
Kijito cha Hathaway Katika kijito hiki, mra nyingi kiliitwa Kijito Kilichopinda na wakazi wake wa awali, baadhi ya ubatizo wa mwanzo wa Kanisa ulifanyika.