6. Kuhama kwa Kanisa Kuelekea Magharibi
Kask.
Canada
New York
Himaya ya Oregon
Himaya Wahindi Wakendu
Fayette
Mji wa New York
Mto Snake
Fort Hall
Fort Bridger
Mto Platte wa Kaskazini
Bahari ya Pasifiki
Fort Laramie
Winter Quarters
Iowa
Pennsylvania
4 Februari 1846 Kuanza kwa msafara wa meli ya Brooklyn
Council Bluffs
Illinois
Indiana
Kirtland
San Francisco
Njia ya California
Great Salt Lake
Jiji la Salt Lake
Mto Platte wa Kusini
Nauvoo
Philadelphia
Fort Leavenworth
Far West
Ohio
Jiji la Washington
Bahari ya Atlantiki
Sacramento
Quincy
Liberty
California
Mexico
Pueblo
Mto Arkansas
Independence
Kuwasili kwa meli ya Brooklyn katika Yerba Buena (San Francisco) 31 Julai 1846
Los Angeles
Missouri
Santa Fe
Mto Canadian
Himaya Wahindi Wakendu
San Bernardino
Misioni ya San Luis Rey
Mto Gila
Rio Grande
Mto Pecos
San Diego
Tucson
Ufunguo
Njia ya Kikosi cha jeshi la Mormoni
Njia ya Watakatifu kuelekea magharibi
Njia ya meli ya Brooklyn
Kilomita
0 150 300 450 600
A B C D E F G H
1 2 3 4
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
-
Fayette Nabii Joseph Smith aliondoka Fayette kwenda Kirtland, Ohio, katika Januari 1831. Matawi matatu ya New York (Fayette, Colesville na Manchester) yalifuatia katika Aprili na Mei 1831 chini ya amri ya Bwana ya kukusanyika (ona M&M 37–38).
-
Kirtland Makao makuu ya Kanisa kimsingi yalikuwa Kirtland tangu mwaka 1831 hadi 1838.
-
Independence Bwana aliitambulisha Independence (katika Wilaya ya Jackson, Missouri) kama kitovu cha Sayuni katika Julai 1831 (ona M&M 57:3). Makundi ya wahuni waliwalazimisha Watakatifu kuihama Wilaya ya Jackson katika Novemba 1833.
-
Liberty Watakatifu wa kutoka Wilaya ya Jackson walikusanyika katika Wilaya ya Clay kuanzia 1833 hadi 1836, wakati walipotakiwa tena kuondoka. Nabii Joseph Smith na wengine watano walifungwa bila haki gerezani hapa toka Desemba 1838 hadi Aprili 1839.
-
Far West Kimbilio lilianzishwa hapa kwa ajili ya Watakatifu mwaka 1836–1838. Yalikuwa makao makuu ya Kanisa katika mwaka 1838. Katika mwaka 1838–1839 Watakatifu walilazimika kuikimbia Illinois.
-
Nauvoo Makao makuu ya Kanisa mwaka 1839–1846. Baada ya mauaji ya kishahidi ya Nabii na kaka yake Hyrum, Watakatifu walihamia magharibi.
-
Council Bluffs Mapayonia waliwasili hapa Juni 1846. Washirika wa Kikosi cha Jeshi la Mormoni waliondoka 21 Julai 1846, chini ya uongozi wa James Allen.
-
Winter Quarters Makazi muhimu ya muda 1846–1848. Kikosi cha mstari wa mbele chini ya maelekezo ya Rais Brigham Young kiliondoka kwa safari ya kwenda Magharibi Aprili 1847.
-
Fort Leavenworth Kikosi cha jeshi la Mormoni kilipewa mavazi na silaha hapa kabla ya kuanza msafara wa magharibi katika Agosti 1846.
-
Santa Fe Philip Cooke aliongoza Kikosi cha Jeshi la Mormoni kilipoondoka hapa 19 Oktoba 1846.
-
Pueblo Vikosi vitatu vya wagonjwa vya Jeshi la Mormoni waliamriwa kubaki Pueblo ili kurudisha nguvu, mahali ambapo walikaa majira ya baridi ya mwaka 1846–1847 pamoja na Watakatifu wa kutoka Mississippi. Makundi haya ya watu yaliingia katika Bonde la Salt Lake Julai 1847.
-
San Diego Kikosi cha jeshi la Mormoni kilimaliza safari yake ya kilomita 3200 (maili 2000) hapa mnamo 29 Januari 1847.
-
Los Angeles Kikosi cha Jeshi la Mormoni kiliachiliwa hapa 16 Julai 1847.
-
Sacramento Baadhi ya washiriki wa kikosi cha jeshi la Mormoni walifanya kazi hapa na kwenye kiwanda cha mbao cha Sutter mashariki ya Mto Marekani. Walikuwepo hapa wakati dhahabu ilipogundulika Januari 1848.
-
Jiji la Salt Lake Makao makuu ya Kanisa tangu 1847 hadi leo. Brigham Young aliwasili katika Bonde la Salt Lake 24 Julai 1847.