Misaada ya Kujifunza
4. Kirtland, Ohio, 1830–1838


4. Kirtland, Ohio, 1830–1838

ramani ya historia ya Kanisa 4

Kask.

Shamba la Morley

Tawi la Mashariki, Mto Chagrin

kwenda Willoughby

kwenda Mentor

Kiwanda cha Mbao

Barabara Markell

Kiwanda cha Kusaga Nafaka

Maeneo ya kubatizia

Nyumba ya Whitney

kwenda Painesville

Duka la Whitney

Kiwanda cha Kutengenezea Ngozi

Hoteli ya Johnson

Shule

Mtaa wa Cowdery

Kiwanda cha majivu

Kijito cha Stoney

Nyumba ya Joseph Smith Mdogo

Duka la Bidhaa Mbalimbali la Joseph Smith Mdogo

kwenda Chardon

Makaburini

Mtaa wa Whitney

Ofisi ya Kupigia Chapa

Hekalu la Kirtland

Nyumba ya Sidney Rigdon

Benki

Barabara ya Chillicothe

Mtaa wa Joseph

Nyumba ya Hyrum Smith

Mita

0 150 300

A B C D

1 2 3 4

1

2

3

4

5

6

7

  1. Nyumba ya Newel K. Whitney Joseph na Emma waliishi kwa wiki kadhaa baada ya wao kuhamia kwanza Kirtland katika mwaka 1831. Joseph alipokea mafunuo kadhaa akiwa hapa.

  2. Shamba la Isaac Morley Joseph na Emma Smith waliishi hapa tangu Machi hadi Septemba 1831. Makuhani wakuu wa kwanza walitawazwa hapa. Joseph alifanya kazi ya Tafsiri ya Joseph Smith ya Biblia (TJS).

  3. Duka la Newel K. Whitney Urais wa Kwanza wa Kanisa ulipewa funguo za ufalme hapa. Shule ya Manabii walikutana hapa wakati wa majira ya baridi ya mwaka 1833. TJS ilikuwa katika hatua za kukamilika hapa katika mwaka 1833. Joseph na Emma waliishi hapa kuanzia mwaka 1832 hadi 1833. Joseph alipokea mafunuo mengi hapa.

  4. Hoteli ya Johnson Hoteli ilikuwa na ofisi ya kwanza ya kupiga chapa katika Kirtland. The Evening and the Morning Star lilikuwa likipigwa chapa hapa kufuatia kuharibiwa kwa kiwanda cha kupiga chapa katika Wilaya ya Jackson, Missouri. Mitume Kumi na Wawili waliondokea hapa 4 Mei 1835, kwa ajili ya misheni zao za kwanza.

  5. Nyumba ya Joseph Smith Mdogo Joseph na Emma waliishi hapa kuanzia mwishoni mwa mwaka 1833 hadi mwanzoni mwa 1838. Tafsiri ya Kitabu cha Ibrahimu ilikamilika, na Joseph alipokea mafunuo kadhaa hapa.

  6. Ofisi ya Kupigia Chapa Lectures on Faith (Mihadhara juu ya Imani) ilitolewa ndani ya jengo hili. Wale Kumi na Wawili na Akidi ya Kwanza ya wale Sabini waliitwa na kutawazwa hapa. Mafundisho na Maagano (Toleo la 1), Kitabu cha Mormoni (toleo la 2), The Evening and the Morning Star, Latter Day Saints’ Messenger and Advocate, na toleo la kwanza la Elders’ Journal yalipigwa chapa hapa.

  7. Hekalu la Kirtland Hekalu hili lilikuwa ndilo hekalu la kwanza katika kipindi hiki. Yesu Kristo alitokea na kulikubali hekalu hili. Musa, Elia, na Eliya walitokea na kurejesha funguo fulani za ukuhani (ona M&M 110). Shule ya Manabii pia ilikutana hapa. Mafunuo yaliyopokelewa hapa ni: M&M 109–110; 137.

    Kirtland Mnamo 17 Agosti 1835. Mafundisho na Maagano kilikubalika kuwa maandiko. Mafunuo yaliyopokelewa katika Kirtland yanajumuisha M&M 41–50; 52–56; 63–64; 72; 78; 84–98; 101–104; 106–110; 112; 134; na 137. Sehemu ya 104 inaonyesha mali fulani itolewe kama usimamizi kwa waumini wa Kanisa waliokuwa wakishiriki katika mpango wa ushirika (ona mstari wa 19–46).