3. New York, Pennsylvania, na Ohio Eneo la Marekani
-
South Bainbridge Joseph Smith Mdogo, na Emma Hale walioana hapa mnamo 18 Januari 1827 (ona JS—H 1:57).
-
Colesville Tawi la Kwanza la Kanisa lilianzishwa hapa katika nyumba ya Joseph Knight Mkubwa, katika Eneo la Mji wa Colesville, katika mwaka 1830.
-
Nyumba ya Joseph Smith Mdogo, katika Harmony Sehemu kubwa ya tafsiri ya Kitabu cha Mormoni ilimalizika hapa. Kwenye kingo za Mto Susquehanna, ukuhani ulirejeshwa jirani ya hapa katika mwaka 1829 (ona M&M 13; 128:20; JS—H 1:71–72).
-
Fayette Mashahidi Watatu waliyaona mabamba ya dhahabu na malaika Moroni hapa (M&M 17). Tafsiri ya Kitabu cha Mormoni ilikamilika hapa katika Juni 1829. Kanisa liliundwa hapa mnamo 6 Aprili 1830 (ona M&M 20–21).
-
Mendon Nyumbani kwa awali kwa Brigham Young na Heber C. Kimball.
-
Kirtland Wamisionari ambao walikuwa wametumwa kwenda kwa Walamani walisimama hapa katika mwaka 1830 na walimbatiza Sidney Rigdon na wengine katika eneo la Kirtland. Ilikuwa ni makao makuu ya Kanisa kuanzia mwaka 1831 hadi 1838. Hekalu la kwanza la kipindi hiki lilijengwa katika Kirtland na liliwekwa wakfu 27 Machi 1836 (ona M&M 109).
-
Mfereji wa Erie Matawi matatu ya Kanisa katika New York (Colesville, Fayette, na Manchester) yalihamia kupitia Mfereji wa Erie na Ziwa Erie hadi Kirtland Ohio, katika Aprili na Mei 1831.
-
Hiram Joseph na Emma waliishi hapa tangu Septemba 1831 hadi Septemba 1832. Joseph na Sidney Rigdon walifanya kazi ya Tafsiri ya Joseph Smith ya Biblia (TJS). Mafunuo yaliyopokelewa hapa: M&M 1, 65–71; 73; 76–77; 79–81; 99; 133.
-
Amherst Joseph Smith alikubalika kama Rais wa Ukuhani Mkuu 25 Januari 1832 (ona M&M 75).
-
Toronto Nyumbani kwa John Taylor, Rais wa tatu wa Kanisa, na Mary Fielding Smith, mke wa Hyrum Smith.