Tangazo
Mkutano wa Ibada ya MEK wa Vijana • Novemba 2, 2014 • Ogden Tabernacle, Ogden, Utah
Wapendwa kaka na dada zangu, kila mmoja wetu ni mwana au binti wa Baba wa Mbinguni mwenye upendo ambaye anawaita na kuwaongoza viongozi kutupatia msaada na mwelekeo. Ni baraka iliyoje kujiunga pamoja tunapojifunza kutoka kwa wale ambao wamechaguliwa kutufundisha. Asanteni kwa kuwa hapa usiku wa leo. Tunapoanza, ninataka kuwapa matangazo mawili mafupi lakini muhimu.
Tangazo letu la kwanza ni kwamba kuanzia Januari 2015, Mikutano ya Ibada ya MEK kama huu sasa itaitwa Mikutano ya Ibada ya Duniani Kote kwa Vijana Wazima. Mikutano hii ya ibada ya duniani kote itafanyika mara tatu kila mwaka - mnamo Januari, Mei, na Septemba. Mabadiliko haya yananuiwa kuonyesha umuhimu wa kila mojawapo ya matangazo na kuhakikisha kwamba kila kijana, popote ulipo na bila kujali hali yako, unaalikwa kushiriki. Tunatumaini kwamba utajitahidi kuhudhuria kila mkutano wa ibada na kuwatia moyo wengine kuhudhuria pamoja nawe ili nyote mpate fursa ya kujiunga pamoja, kusikiliza ushauri kutoka kwa viongozi wetu, na kupokea ufunuo na mwelekeo wa kibinafsi. Tunawahimiza viongozi wa ukuhani wafanye mikutano hii ya ibada ya duniani kote kuwa matukio muhimu katika maeneo yao.
Tangazo lingine linahusiana na madarasa ya dini yanayohitajika kwa kuhitimu katika Vyuo vya Dini na Vyuo Vikuu vya Kanisa. Bodi ya Elimu ya Kanisa na Bodi za wadhamini za BYU, BYU---Idaho na BYU---Hawaii, na LDS Business College zimehidhinisha kozi nne mpya ambazo zitatolewa kuanzia majira ya kupukutika ya 2015. Kozi hizi ni “Jesus Christ and the Everlasting Gospel,” “The Teachings and Doctrine of the Book of Mormon,” “Foundations of the Restoration,” na “The Eternal Family.”
Kozi hizi zinakusudiwa kuwa kiini cha elimu yetu ya Dini. Zitazingatia maandiko na mafundisho ya manabii wa siku za mwisho, kwa kumzingatia Mwokozi, mafundisho Yake, na matukio muhimu katika historia ya Kanisa. Unapojifunza maandiko yote ya Kanisa, maandiko yataunganishwa pamoja, yakikusaidia kuendeleza, kuelewa na kufahamu injili kwa ukamilifu kila kitabu cha maandiko cha Kanisa. Madarasa haya yataongezea zaidi uzoefu wako wa zamani wa kanisa na wa kibinafsi, na mafunzo ya injili. Yatakusaidia kutumia kanuni za injili kwa njia ambazo ni muhimu kwa hali yako ya sasa.
Pia ninaweza kuelezea kwamba kozi zote za maandiko pamoja na madarasa mengine ya dini yataendelea kutolewa katika vyuo vyetu vya dini na vyuo vikuu vyetu. Kozi hizi mpya zitahitajika kwa wanafunzi wote wanaojiunga na wale wanaoendelea. Tunawaomba wote mhudhurie madarasa haya na kujitahidi kuhitimu kutoka chuo kikuu cha Kanisa au Chuo cha Dini. Kama tayari umepata mahitaji ya kuhitimu, mtafikiria kuchukua madarasa haya mnapoendeleza masomo yenu ya injili kupitia kwa ushiriki wa chuo na madarasa ya dini ya chuo na ya chuo kikuu cha Kanisa. Katika siku zijazo utaweza kujifunza zaidi kuhusu madarasa haya mapya kwa kutembelea education.lds.org.
Nina hakika kwamba unaposhiriki katika mikutano ya ibada ya duniani kote na madarasa ya dini, utaweza kuelewa vyema maandiko, utashirikiana na wengine ambao watakuinua na kukuongoza, na utaimarisha imani yako na ushuhuda katika Yesu Kristo. Na hiyo iwe hivyo kwa kila mmoja wenu, katika jina la Yesu Kristo, amina.
© 2014 by Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Kiingereza kilihidhinishwa: 1/14. Tafsiri ilihidinishwa: 1/14. Tafsiri ya Announcement. Lugha PD10052815 743