Mikutano ya Ibada ya Ulimwenguni Kote
Kutuni Mioyo Yetu na Sauti ya Roho


56:3

Kutuni Mioyo Yetu na Sauti ya Roho

Ibada ya MEK kwa Vijana Wazima • Machi 2, 2014 • Chuo Kikuu cha Brigham Young–Idaho

Ni fursa nzuri kukutana nanyi katika ibada hii. Nimeomba kwamba Bwana awabariki ninyi ili msikie kitu fulani ambacho kitaweza kuongeza uwezo wenu wa kutambua sauti ya Roho. Inawezekana tayari mmepokea ujumbe ambao mmehisi ulikuwa kwa ajili yenu katika huo muziki maridadi ambao tumesikiliza.

Karibu miaka 41 iliyopita, kwa kujisukuma tu nilihudhuria ibada ya vijana wazima iliyofanyika katika Temple Square. Dhoruba kubwa ya theluji ambayo tulipata mchana huo wa ibada ilijaribu imani yangu. Lakini kwa sababu nilikuwa nimeombwa kushiriki kidogo kwa njia fulani, nilienda kutimiza wajibu wangu. Nimejifunza katika miaka mingi kwamba kitu fulani Rais Eyring alishiriki kuwa ni kweli: “Mtu hawezi kutoa gamba la mkate kwa Bwana na badala yake akose kupokea mkate.”1 Mume wangu wa ajabu ndiyo “mkate” niliopokea kwa “gamba la mkate” langu la kushiriki! Ilikuwa katika ibada ile ambapo nilikutana naye. Alikuwa anaimba katika kwaya na kwa ujasiri alikuja na kujitambulisha yeye mwenyewe kwangu hapo mwisho wa mkutano. Nilikuwa na shukrani ilioje ambayo mimi nilihisi kuwa na wajibu hata kushiriki usiku huo na kwamba Baba yetu wa Mbinguni mwenye rehema alipokea hata juhudi zangu za shingo upande kuwa pale ambapo nilihitajika kuwepo.

Mimi nina shukrani kuwa na baadhi ya watoto wetu na mjukuu wetu mkubwa wa kike hapa pamoja nasi usiku wa leo. McKaela hucheza violini. Akiwa umri wa miaka 3 alianza masomo ya violini, na sasa, akiwa umri wa miaka 16, hakika ni mwana muziki mwenye kipaji. Na ninaweza kusema hivyo kwa sababu mimi ni bibi yake, na akina bibi hawadanganyi! Imekuwa maongozi kutazama maendeleo yake hatua kwa hatua, akijifunza kutumia chombo si tu kubariki maisha yake mwenyewe bali pia maisha ya wengi wenu. Amejifunza sanaa ya kutuni chombo chake, umuhimu wa mazoezi ya kila siku kwa bidii, na shangwe ya kucheza na kuchanganya chombo chake na vingine.

Nilipokuwa nikihudumu misheni pamoja na mume wangu miaka michahe iliyopita, nilijifunza kusoma ishara na kusema sauti za herufi za Kikorea. Nilijifunza salamu fulani za kawaida, maonyesho machache, na maneno machache ya injili, na ningeweza kutofautisha lugha ya Kikorea na lugha zingine. Nilikariri nyimbo chache ninazozipenda na nyimbo za Msingi katika Kikorea. Lakini nilikuwa sina ufasaha katika uwezo wangu wa kuongea au kuelewa mengi ya lugha hiyo maridadi.

Kwa nini ninashiriki hii mifano inayoweza kuonekana haihusiki nanyi? Kwa sababu ningependa sisi tujadili kuhusu kujifunza lugha ya Roho---jinsi Yeye anavyosema nasi na jinsi tunaweza kuongeza uwezo wetu wa kusikia sauti Yake. Kama vile tu kijifunza chombo au lugha ni mchakato, kujifunza lugha ya Roho pia ni mchakato, mmoja ambao ni muhimu sana kwetu kujifunza, aidha sisi tumebatizwa majuzi au washiriki wa siku nyingi wa Kanisa.

Mwokozi alifundisha katika Kitabu cha Mormoni kwamba Walamani “walibatizwa kwa moto na Roho Mtakatifu, na hawakujua hivyo.”2 Ni hamu yangu kuu kwamba tutaongeza uwezo wetu wa kusikia na kuelewa minong’ono ya Roho na kutenda juu ya minong’ono ambayo sisi tunapata kutoka kwa Roho Mtakatifu. Ili kufanya hivyo, sisi sharti kwanza tujifunze kutambua sauti Yake.

Acha tuchukue dakika moja kutathimini uzoefu wetu. Sasa, kwa sababu hadhira yetu hapa ni kubwa sana na tunaungana na vijana wazima kote duniani. Ningependa kufanya kitu fulani kipya. Bila kuwa wabinafsi sana, ninyi mnaweza kushiriki baadhi ya uzoefu wenu kwa maswali yafuatayo kati yenu katika Twita? Mnapokuwa na muda, “twitini” majibu yenu kwa #cesdevo.

Hapa kuna maswali kwa majibu yenu: Tunaweza kujua vipi ikiwa tumesikia sauti ya Roho?

Acha tujiulize wenyewe maswali machache ya ziada yafuatayo tunapotakafari swali hili:

  • Je! Nimeshapata uzoefu wa hisia za upendo, shangwe, amani, subira, unyenyekevu, upole, imani matumaini na faraja?

  • Je! Mawazo yameshanijia akilini mwangu au hisia moyoni mwangu, ambazo mimi najua zinatoka kwa Bwana, na sio kutoka kwangu?

  • Je! Nimesikia sauti yangu ikiongea ukweli bila kupanga kile nitakachosema?

  • Je! Nimeshapata upanuzi wa ujuzi na uwezo wangu?

  • Je! Nimeshapata mwongozo na ulinzi kutokana na ulaghai?

  • Je! Nimeshatambua dhambi katika maisha yangu na nikapata hamu ya kurekebisha?

  • Je! Nimeshahisi Roho akitukuza na kushuhudia juu ya Mungu Baba na Yesu Kristo?3

Kama mlijibu“ndio” kwa lolote kati ya maswali haya, umeshahisi Roho wa Bwana wakati fulani katika maisha yako. Lakini swali muhimu sana ni “Unaweza kuhisi hivyo sasa? ”4

Ushauri wa nabii Mormoni kuhusu kufuata Nuru ya Kristo unaweza kutusaidia kujua jinsi ya kupokea Roho Mtakatifu. Mormoni alisema:

“Kwani tazama, Roho ya Kristo imetolewa kwa kila mtu, ili ajue mema na maovu; kwa hivyo, ninawaonyesha njia ya kuhukumu; kwani kila kitu kinachokaribisha kufanya mema, na kushawishi kuamini katika Kristo, kinasababishwa na uwezo na thawabu ya Kristo; kwa hivyo mngejua na ufahamu kamili kwamba ni cha Mungu.

Lakini kitu chochote ambacho hushawishi watu kufanya maovu, na kutoamini katika Kristo, na kumkana, na kutomtumikia Mungu, hapo mtajua na ufahamu kamili kwamba ni cha ibilisi; kwani kwa njia hii ndiyo ibilisi hufanya kazi, kwani hamshawishi mtu yeyote kufanya mema, la, sio mmoja; wala malaika wake; wala wale ambao hujiweka chini yake.”5

Rais Gordon  B. Hinckley alisema: “Huu ni mtihani, baada ya kila kitu kusemwa na kufanywa. Je! Kinamshawishi mtu kufanya mema, kuinuka, kusimama wima, kufanya kitu kilicho sahihi, kuwa mpole, kuwa mkarimu? Basi hiyo ndiyo Roho ya Mungu.”6

Kwa nini kutambua minong’ono ya Roho inaonekana kuwa vigumu sana? Labda sababu moja ni kwamba Roho huwasiliana kote kwa akili zetu na kwa mioyo yetu. Katika kujifunza lugha ya Roho, sisi wakati mwingine tunachanganya mawazo yetu wenyewe na hisia zetu wenyewe pamoja na minong’ono ya Roho. Sababu nyingine ni kwamba kutambua Roho ni kipawa cha Roho. Kama vile kujifunza lugha huwa rahisi kwa wengine na si hivyo kwa wengine, vivyo hivyo uwezo wa kuelewa minong’ono ya Roho. Mara nyingi sana, kujifunza chombo au lugha kunahitaji juhudi kubwa sana, ikijumuisha kufanya mazoezi na wakati mwingine kufanya makosa. Vivyo hivyo ndivyo ilivyo na mchakato wa kujifunza lugha ya Roho.

Je! Inaweza kukusaidia kujua kwamba ufunuo wa kibinafsi ni mstari kwa mstari, fundisho juu ya fundisho mchakato ambao hata manabii, waonaji, na wafunuaji wanajifunza kuelewa? Ufuatao ni mfano kutoka kwa maisha ya Mzee Jeffery R. Holland.

“Kuna nyakati ambapo njia pekee ya kutoka A hadi C ni kwa kupitia njia ya B.

“Kwa kuwa nililelewa Utah ya kusini na nilipata kufurahia maajabu na urembo wote wa Utah ya kusini na Arizona ya kaskazini, nilitaka kumjulisha mwana wangu hayo na nilitaka kumuonyesha sehemu ambazo niliziona na kufurahia nilipokuwa umri wake. Kwa hivyo, mama yake alituwekea chakula kidogo na tukachukua gari la pikaapu la babu yake na tukaelekea kusini hata kule tunakokuita Arizona Strip ya kale.

“Kuona kwamba jua lilikuwa linaenda kutua tuliamua kwamba ilikuwa vyema turudi nyumbani. Lakini tulirudi kwenye njia panda mahususi katika barabara, ambayo wakati huo ilikuwa haitambuliki. Nilimuomba mwanangu aombe kuhusu barabara gani tulitakiwa kuifuata yeye alihisi sana kwamba tulifaa kwenda kulia na mimi nikakubali. Na tukaenda njia ya kulia, na ilikuwa na kikomo. Tulitembea yadi mia nne au tano au sita na ikawa haiendelei kabisa, wazi kuwa ilikuwa barabara ambayo siyo.

“Tuligeuza, na kurudi nyuma, na kuchukua ile barabara nyingine. Na wazi barabara ya kushoto ilikuwa barabara sahihi.

“Wakati wa safari yetu, Matt alisema, ‘Baba, kwa nini tulihisi, baada ya kusali juu yake, kwamba barabara ya kulia ndio ilikuwa sawa kuchukua, sahihi kuchukua, na haikuwa?’ Na mimi nikasema, ‘Nafikiria kwamba Bwana, matarajio Yake kwetu hapo na jibu Lake kwa maombi yetu ilikuwa ni kutupeleka katika barabara sahihi haraka iwezekanavyo na kwa uhakika fulani, kwa uelewa fulani tulikuwa katika barabara sahihi na hatukuwa na haja ya kuwa na wasi wasi juu yake. Na wakati huu, njia rahisi ya kufanya hivyo ilikuwa ni kutuacha twende yadi 400 au 500 kwenye barabara isiyo sahihi na kwa upesi sana kujua bila shaka hii barabara si sahihi na kwa hivyo, kwa uhakika sawa, kwa uthibitisho sawa kwamba ile nyingine ndio barabara sahihi.’

Mimi nina elimu ya hakika kabisa, elimu kamili kwamba Mungu anatupenda sisi. Yeye ni mwema. Yeye ni Baba yetu na Yeye anatutarajia sisi kusali na kuwa na matumaini na tukiamini na bila kukata tamaa na kuwa na wasi wasi na bila kurudi nyuma na bila kuyumbayumba wakati kitu kinaonekana si sahihi. Tukae tu, tuendelee kufanya kazi, tuendelee kuamini,tuendelee kuwa na matumaini, kufuata njia ile ile na tutaishi kuangukia katika mikono Yake na kuhisi ukumbatio Wake na kumsikia Yeye akisema, ‘Nilikuambia itakuwa sawa, Nilikuambia itakuwa sawa. ’”7

Hiyo si ni vizuri sana? Nilishapata uzoefu sawa na wa Mzee Holland nilipokuwa nikijitayarisha kuongea usiku wa leo. Nilikuwa nimeanza katika njia moja, kutafiti na kuandika mawazo yangu juu ya mada moja ya kuongea kuihusu, nikaishia tu kushindwa kupata muafaka kuhusu mada. Nilipata hisia kulikuwa na kitu fulani kingine ninapaswa kukishughulikia. Ndio basi ndipo nikakumbuka uzoefu ambao nilipata karibu miaka miwili iliyopita. Nilipoitwa kwanza kuhudumu kama rais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, nilikosa usingizi usiku kadhaa. Mojawapo ya usiku wa siku nyingi, mawazo yangu yalijaa katika akili yangu na yakajisukuma ndani ya moyo wangu. Niliyaandika na kuyahifadhi kando, nisiyakumbuke tena mpaka wiki chache zilizopita, wakati hizo hisia za wasi wasi kuhusu mada yangu ya kwanza zilianza kunisumbua. Baba wa Mbinguni aliniacha niende ile njia nyingine kwa muda fulani, lakini Yeye alinielekeza katika hii barabara kupitia hisia nyororo katika moyo wangu na kuamsha kumbukumbu katika akili yangu kupitia kipawa cha Roho Mtakatifu.

Tunaweza kufanya nini ili kutuni katika sauti ya Roho? Tunaweza kuanza kutambua kwamba Baba yetu wa Mbinguni anataka kuwasiliana nasi. Tunajua hivyo kwa sababu manabii wote wa siku za mwisho wamefunza mafundisho ya ufunuo wa kibinafsi. Fikiria juu ya baraka zingine nyingi Bwana ametupatia sisi ili kwamba tuweze kuwasiliana na Yeye na kupokea maneno Yake: maandiko, baraka za baba mkuu, sala, maagizo, viongozi wenye maongozi na wazazi, na kipawa cha Roho Mtakatifu.

Tutaanza wapi katika juhudi zetu za kujongea karibu na Mungu na kusikia sauti Yake ikiongea nasi? Tunaanza na mambo ya msingi. Tunafanya vitu vidogo na rahisi ambavyo vinaonyesha kwamba Yeye anakuja mbele katika maisha yetu na kwamba tunataka kupokea ufunuo kutoka Kwake. Wakati nilipotembelea Afrika Magharibi, nilijifunza kishazi ninachokipenda ambacho kinaonekana kinaweza kutumika katika mchakato wa ufunuo wa kibinafsi: pole pole, kidogo kidogo.” Ni baadhi ya vitu gani “pole pole, kidogo kidogo” tunaweza kufanya?

Nambari 1: Kusali kwa Uaminifu na Unyenyekevu.

Moyo wangu wa kimama umeguswa kote katika miaka mingi ninapowatazama watoto wangu mwenyewe na wajukuu wangu wakifanya imani kwa kuomba katika sala ya unyenyekevu na uaminifu usaidizi wa Bwana kwa matatizo yao rahisi. Kumbukumbu nyororo katika familia yangu inaonyesha haya.

Mwana wetu ndiye mtoto mkubwa katika familia yangu. Ana dada watano na hana kaka. Kabla tu ya kuzaliwa kwa binti yetu wa tatu, mume wangu alimwahidi mwana wetu mbwa kama huyu mtoto angekuwa msichana mwingine. Wakati mtoto wetu wa kike alipozaliwa, mume wangu mwema alitimiza ahadi yake. Mbwa huyu akawa rafiki wa dhati wa mwana wetu. Alimpenda huyu mbwa. Siku moja, huyu mbwa alipotea. Tukamtafuta na kumtafuta, lakini hatukumpata. Tulimwita mudhitbiti wa wanyama. Na yeye hakutupatia matumaini mengi, kwa vile tuliishi karibu na barabara kuu. Huyu ofisa alihisi kwamba wakati mwingi ulikuwa umepita na kulikuwa na uwezekano mwingi sana mbwa huyo alikuwa amekwenda kwenye barabara kuu na kugongwa na gari.

Sisi tulifanya tuwezavyo kumfariji mwana wetu wakati tulishiriki kile tulikuwa tumesikia, lakini alikuwa anafadhaika sana. Nakumbuka nikimwalika yeye kusali kwa Baba wa Mbinguni kwa faraja. Mvulana wetu mdogo alinitazama katika macho na kusema, “Nimekuwa nikiomba na kuomba, Mama.”

Baada ya siku kadhaa kupita. Kisha asubuhi moja mapema mlango wetu uligongwa. Mmoja wa watoto wetu alienda mlangoni na kurudi kuniita. Niliingia wasi wasi nilipoona gari limeegeshwa katika barabara ya nyumbani kwetu ikiwa imeandikwa “Udhibiti wa Wanyama” ubavuni. Mtu aliyekuwa mlangoni alinitazama na kusema, “Bi. Burton, nadhani nina kitu katika gari langu ambacho ni cha mwanao.”

Moyo wangu ukapasuka, Mimi nakumbuka nikiwa na wasi wasi kwamba alikuwa amemuokota mbwa wetu na kwamba mbwa huyo alikuwa labda amekufa au amejeruhiwa vibaya sana. Kwa furaha yangu kuu, kulikuwa na mbwa wetu hapo nyuma ya gari---mchangamfu, mzima, na tayari kuruka nje ya gari na kukimbia mikononi mwa mvulana wetu mdogo.

Mimi nilimuuliza ofisa wa udhibiti ni wapi alipompata huyu mbwa. Alisema: “Kitu kisicho cha kawaida kutendeka asubuhi ya leo nilipokuwa nikiondoka nyumbani. Hapo, mbele ya nyumba yangu, kulikuwa na mbwa ambaye alifanana na maelezo uliyonipatia kwenye simu. Mbwa huyu aliitika nilipomwita jina lake. Kwa hivyo nikafikiria nimlete nyumbani na nitulize akili ya mvulana wako mdogo kabla yeye kwenda shule.

Najua kwamba Bwana hujibu maombi ya uaminifu, ororo, ya kitoto. Baba wa Mbinguni hutaka watoto wamjue Yeye yupo hapo katika maisha yao ili wao waendelee kumtumainia Yeye wanapokua na kukomaa. Kwa sababu watoto kwa kawaida wamejawa na unyenyekevu, wao huitimu kupokea ahadi ya Baba wa Mbinguni kama ilivyotolewa katika Mafundisho na Maagano: “Jinyenyekeze; na Bwana Mungu wako atakuongoza kwa mkono, na kukupa jibu la sala zako.”8

Ninaposhiriki swali lifutalo ambalo Rais Spencer  W. Kimball aliuliza kundi sawa na hii, fikirieni unyenyekevu wenu wenyewe na uaminifu wa sala zenu wenyewe. Hapa kuna. Dondoo: Je! Mnataka mwongozo? Je! Mmesali kwa Bwana kwa maongozi? Je! Mnataka kufanya kile kilicho sahihi au mnataka kufanya kile mnataka kama ni sahihi au si sahihi? Je! Mnataka kufanya kile kilicho bora kwenu katika muda mrefu ujao au kile kinachoonekana cha kutamanisha sana kwa wakati huu? Je! Mmesali? Je! Mmsali kiasi gani? Je! Mmesali vipi? Je! Mmsali kama Mwokozi alifanya … au mmeomba kile mnachotaka bila kujali kama kinafaa?”

Rais Kimball kisha anaendelea. “Je! Mnasema katika sala zenu: ‘Mapenzi yako yatimie’? Je! Mlisema, ‘Baba wa Mbinguni, kama utanipatia maongozi na kunipatia msukumo wa kile kilicho sahihi, mimi nitaka kile kilicho sahihi’? Au, mlisali, Baba wa Mbinguni, nakupenda, naamini katika wewe, mimi najua wewe upo kila mahali. Mimi ni mwaminifu. Mimi kwa uaminifu nina hamu ya kufanya kile kilicho sahihi. Mimi najua unaweza kuona mwisho kutoka mwanzo. Unaweza kuona siku zijazo. Wewe unaweza kutambua kama katika hali hii ninayowasilisha, nitakuwa na amani au taabu, furaha au majonzi, ufanisi au kushindwa. Niambie, tafadhali, Baba mpendwa wa Mbinguni, na mimi naahidi kufanya kile utaniambia nifanye.’ Je! Mmeshasali kwa njia hii? Je! Hamfikirii inaweza kuwa ni busara? Je! Mna ujasiri wa kutosha kusali sala hii?”9

Njia moja ya kusali kwa uaminifu nikujifunza kujenga maswali ya uaminifu na yanayotoka moyoni na kwa unyenyekevu kuyapeleka kwa Bwana. Fikiria maswali ya Joseph Smith: “Ni nini cha kufanya? Ni kundi gani kati yao haya yote lililo sahihi; au, je, yote si sahihi? Kama lolote kati yao ni sahihi, ni lipi, na nitajuaje?”10 Kwa busara, yeye aligeukia maandiko, chanzo cha ukweli mtakatifu, ambao ulimfanya yeye “kutafakari sana”na kumpelekea kwa “azimio la ‘kuomba kwa Mungu.’”11 Akiamini maombi yake yatajibiwa.

Kuomba kwa uaminifu humaanisha tunadhamiria kutenda juu ya majibu tunayopokea. Juu ya maombi yake ya dhati katika Kichaka Kitakatifu, Joseph alisema, “Kusudi langu la kwenda kumwomba Bwana lilikuwa ni kutaka kujua ni lipi kati ya madhehebu yale yote lilikuwa sahihi, ili nipate kujua lipi nijiunge nalo.”12 Ilikuwa wazi kwamba Joseph alikuwa na dhamira ya kutenda juu chochote Bwana angechagua kumfunulia. Hata hivyo, kabla hata ya kuuliza swali rahisi, yeye alipokea mengi zaidi ya yale aliyokuwa anatumainia. Alipata fursa ya ajabu ya kumuona Baba yetu aliye Mbinguni na Mwanawe Mpendwa, Yesu Kristo! Mimi nafurahia katika hili jibu tukufu kwa hamu ya moyoni rahisi na uaminifu kwa elimu ya nabii mvulana, Joseph Smith!

Nambari 2: Tenda papohapo juu ya misukumo ya kiroho.

Tukio la kusisimua kutoka kwa maisha ya nabii wetu mpendwa mwenyewe, Rais Thomas  S. Monson, linaonyesha umuhimu mkuu wa kujibu mara moja misukumo kutoka kwa Roho.

[Msimuliaji:]: Askofu Monson alipoendelea kukomaa katika majukumu yake, alijifunza masomo mengi, miongoni mwa hayo ni umuhimu wa kufuata Roho na kuweka matumaini katika Bwana.

“Usiku mmoja wakati wa mkutano wa kigingi wa uongozi wa ukuhani, alipokea msukumo wa kipekee kwamba anafaa kuondoka upesi kutoka kwenye mkutano na kuendesha gari mpaka hospitali ya askari waliostaafu juu katika barabara za Mjini Salt Lake. Kabla ya kuondoka nyumbani usiku huo, alikuwa amepokea simu ikimtaarifu kwamba mshiriki wa kata mzee alikuwa mgonjwa na alikuwa amelazwa huko hospitalini kwa kuhudumia. Inawezekana askofu, mpiga simu alimwomba, atafute muda wa kwenda hospitalini na akatoe baraka? Huyu askofu kijana mwenye shughuli nyingi alielezea kuwa yeye alikuwa njiani kwenda kwenye mkutano lakini atakwenda huko hospitalini baadaye. Sasa msukumo ulikuwa wa nguvu sana kushinda kawaida: ‘Ondoka mkutanoni na uende hospitalini mara moja.’

Askofu Monson alitazama jukwani. Rais wa kigingi alikuwa anaongea! Hakuona jinsi angesimama katikati ya hotuba na kupita kwenye safu nzima ya wanaume. Kwa maumivu, yeye alingojea dakika za mwisho za ujumbe wa rais wa kigingi kisha akatoka haraka sana kuelekea mlangoni kabla ya maombi ya kufunga kutangazwa. Akakimbia ushoroba wote wa ghorofa ya nne ya hospitali, huyu askofu kijana aliona shughuli nyingi nje ya chumba alichokuwa anaenda.

Mhudumu alisimama na kusema, “Wewe ni Askofu Monson?’

“Ndio,” yeye alijibu.

“Pole,” alisema. “Mgonjwa alikuwa anaita jina lako kabla yeye kufa.”

Akipigana na machozi, Askofu Monson alitembea tena katika usiku ule. Aliapa wakati huo kwamba hatasita kamwe kutenda juu ya mnong’ono kutoka kwa Bwana. Angefuata mara moja msukumo wa Roho popote utakapomwongoza.

[Mzee Jeffrey R. Holland:] Hakuna mtu anayeweza kumwelewa Rais Thomas  S. Monson ambaye haelewi idadi ya marudio, marudio ya aina hii ya minong’ono ya kiroho katika maisha yake na kuyajibu kwake kwa uaminifu.”13

Nambari 3: Kupekua Maandiko Kila Siku..

Mzee Robert  D. Hales alifunza: “Tunapotaka kusema na Mungu, sisi tunaomba. Na tunapotaka Yeye aseme nasi, tunapekua maandiko; kwa maneno Yake yanasemwa kupitia manabii Wake.”14

Mimi nilipokuwa na umri wa miaka 20, nilikuwa ninakabiliana na uamuzi mgumu na haikuonekana ninapata jibu la maombi yngu. Usiku mmoja, baba yangu alikuja nyumbani alikuja usiku sana kutoka mkutano wa Kanisa na kuona taa ya chumba ninacholala inawaka . Alikaa pembeni mwa kitanda changu na kuuliza kama yeye angeweza kusaidia, akihisi kusumbuka kwangu. Nilimwaga moyo wangu kwake. Alishauri kwamba nigeukie maandiko ili nipate mwongozo wa maamuzi yangu, akinipatia vifungu mahususi ambavyo ningetafakari na kuomba. Nilifuata ushauri wake wenye maongozi na kupekua maandiko. Baada ya muda fulani na nikaendelea kwa juhudi hii kwa dhati, nilibarikiwa na majibu ya wazi kwa maombi yangu. Nilifanya fikira zangu bora na maamuzi kwa Bwana, na kwa uaminifu niliomba uthibitisho wa maamuzi hayo na kuhisi uhakikisho tulivu, wa amani katika kina cha moyo wangu.

Tunajifunza katika maandiko kwamba wana wema wa Helamani, Lehi na Nefi, walipata “funuo nyingi kila siku.”15 Tunaposherehekea kila siku katika maneno ya Kristo katika maandiko na kutafakari mambo tunayosoma, sisi pia tunaweza kupata mafunuo ya kila siku kupitia kipawa cha Roho Mtakatifu, hasa tunapoweka kumbukumbu za mawazo na hisia tunazopokea kwa makini.

Nambari 4: Ishi sheria ya mfungo.

Ili kuongeza uwezo wetu wa kusikia sauti ya Roho, sisi sote tutaweza kufanya vyema kufunga kwa masaa 24 kila siku ya Jumapili ya mfungo na kutoa toleo letu la ukarimu la mfungo ili kusaidia wale walio na mahitaji. Rais Harold B. Lee alishauri: “Bwana alisema kwa Isaya, kwamba wale wanafunga na kutoa mkate kwa wenye njaa, wanaweza kumwita na Bwana atajibu, wanaweza kulia na Bwana atasema, ‘Mimi hapa’ [Ona Isaya 58:6–9.] Hio ni njia moja ya kuendelea katika masharti ya kuongea na Bwana. Yajaribu mwaka huu. Ishi sheria ya mfungo kikamilifu.”16

Katika kitabu cha Alma, tunajifunza kwamba wana wa Mosia “walikuwa wamejitoa kwa sala, na kufunga; kwa hivyo walikuwa na roho ya unabii, na roho ya ufunuo,, na walipofundisha, walifundisha kwa uwezo na mamlaka ya Mungu.”17 Kishazi hiki “walikuwa wamejitoa” ni wazo la kutafakari tunapotathimini juhudi zetu za mfungo wa kweli.

Nambari 5: Kuwa mstahiki na kuabudu katika hekalu.

Kulingana na Rais George Albert Smith, dondoo, “Kila mmoja wetu ana haki ya maongozi ya Bwana kulingana na vile tunavyoishi maisha ya kiungu.”18 Tafadhali fahamu kwamba yeye hakusema tunafaa kuwa wakamilifu ndio tupokee maongozi. Bali sisi tunahitaji kufanya juhudi zetu zote kuishi kwa ustahiki.

Kumbuka na ujifunze kutoka kwa mfano mbaya wa watu wa Mfalme Limhi katika Kitabu cha Mormoni: “Bwana alikuwa mgumu wa kusikia kilio chao kwa sababu ya maovu yao.”19

Ustahiki unaonekana kuwa gharama ndogo ya kulipwa ili kufungua madirisha ya mbinguni. Tunapoweka maagano yetu na kupokea sakramenti kwa ustahiki, tunaahidiwa kwamba daima tutakuwa na Roho kuwa nasi.20Lakini hayo huja baada ya sisi kuahidi na kuweka agano kwamba sisi daima tutamkubuka Mwokozi! Cha ziada, kuzingatia na kuishi kwa ustahiki ili kuingia katika hekalu, na kufanya hivyo kila mara kadri hali zetu zinaruhusu, hutuwezesha “kukua katika [Bwana], na kupokea ujalivu wa Roho Mtakatifu.”21

Nambari 6: “Usicheze na mambo matakatifu.” 22

Tambua kwamba ufunuo kutoka kwa Bwana ni amana takatifu. Mzee Richard G. Scott alifundisha kwamba “maongozi yaliyoandikwa kwa makini yanaonyesha Mungu kwamba mawasiliano yake ni matakatifu kwetu. … kumbukumbu kama hizo … zinafaa kulindwa zisipotee au zisiingiliwe na wengine.”23

Ushahidi mwa pili kwa mafundisho huja kutoka kwa uzoefu wa Rais Harold  B. Lee, ambaye alisema: “Wakati fulani usiku wa manane niliamka na singeweza kulala mpaka nilipoondoka kitandani na kuandika kile nilichokuwa ninakabiliana nacho katika karatasi. Lakini inahitaji ujasiri mwingi kutenda tunapoelekezwa kama jibu la maombi.”24

Nambari 7: Jitayarishe kusonga mbele kwa imani.

Wakati mume wangu nami tulichumbiana ili tuonane, tulikuwa na mazungumzo marefu kuhusu siku za usoni pamoja. Tutafanya nini kuhusu kisomo? Tutapata watoto lini? Ni ajira gani ambayo itaweza kukidhi mahitaji ya familia yetu na kuturuhusu sisi kuhudumu katika Kanisa? Kwa sababu tuliamini katika ushauri uliotolewa na nabii aliye hai ambaye alitufunza kwamba tunaweza kuwa na watoto hali tunaendelea na masomo na kazi yote kwa wakati mmoja, tulisonga mbele kwa imani.

Haikuwa rahisi. Mume wangu aliishia kufanya kazi tatu za muda hali huku anaenda shuleli kuniruhusu mimi kuanza ajira yangu mpya kama mama na mtunzaji. Njia hiyi ilikuwa kinyume kabisa na mantiki ya ulimwengu, hata kwa wakati huo. Nikitazama nyuma, sasa tunaona jinsi kuchukua hatua hizo za imani kumeleta matokeo ya baraka za milele, baraka ambazo tungekosa kama hatungesikia sauti ya Roho kupitia nabii mteule wa Bwana.

Ili kuelezea zaidi, fikiria uzoefu wa Mzee Robert  D. Hales. Yeye alipangiwa kuwa mwenzi mdogo wa Rais Ezra Taft Benson katika mkutano wa kigingi ambapo rais mpya wa kigingi alikuwa anaitwa. Anaelezea yafuatayo: “Baada kuomba, kuhojiana, kutafiti na kuomba tena, Mzee Benson aliuliza kama mimi najua nani atakaye kuwa rais mpya. Mimi nilisema nilikuwa sijapokea maongozi hayo bado. Alinitazama kwa muda mrefu na kujibu yeye pia hakujua. Hata hivyo, tulipata maongozi kuwaomba wenye ukuhani watatu wastahiki kuongea katika kikao cha Jumamosi jioni cha mkutano mkuu. Muda baada ya msemaji wa tatu kuanza, Roho alinisukuma kwamba yeye anafaa kuwa rais mpya wa kigingi. Nilimtazama Rais Benson na niliona machozi yakimtiririka usoni mwake. Ufunuo ulikuwa umetolewa kwetu sote---lakini tu kwa kuendelea kutafuta mapenzi ya Baba yetu wa Mbinguni tunaposonga mbele kwa imani.”25

Nambari 8: Acha Bwana aamue utondoti wa kile Yeye anachagua kufunua na wakati Yeye anachagua kukifunua.

Maoni ya mtunzi Corrie ten Boom yanaonekana kutumika hapa: “Kila uzoefu ambao Mungu hutoa kwetu, kila mtu Yeye umweka katika maisha yetu, ni matayarisho maridhawa kwa siku za usoni ambazo Yeye anaweza kuona.”26

Labda wengine wenu mshapata uzoefu kama huo ambao kwao watoto wetu sita wameshapata jinsi kila mmoja alipokuwa anatafuta mwenzi wa milele mstahiki. Kwa sababu utambuzi ni 20/20, wanaweza kuona sasa kwamba kila mmoja alihitaji uzoefu fulani ili aweze kutambua mkono wa Bwana ukiwaelekeza wao kwa wenzi wao wa milele. Baadhi ya uzoefu huu ulihitaji miaka mingi ya kungoja kwa subira na kusonga mbele kwa imani. Nyakati zingine mbingu zilionekana kufungwa kwao walipokuwa wanaomba. Wakati masaa ya Bwana yanahitalifiana ya hamu zetu wenyewe, tumaini kwamba kunaweza kuwa na uzoefu fulani wa matayarisho Bwana anatuhitaji sisi kuwa nao kabla maombi yetu kujibiwa.

Mzee Dallin  H.Oaks alifunza:

“Tunapaswa kutambua kwamba Bwana atasema nasi kupitia Roho katika wakati wake mwenyewe na katika njia yake mwenyewe. Watu wengi hawaelewi kanuni hii. Wao wanaamini kwamba wakati wao wako tayari na inapokuwa ni sawa na nafasi zao, wanaweza kumwita Bwana na Yeye atajibu upesi, hata katika njia makini sana wamepelekeza. Ufunuo hauji kwa njia hiyo. …

“…  Hatuwezi kulazimisha mambo ya kiroho.”27

Karibu miaka 15 iliyopita, mama yangu alipoteza kuona kwake. Alisumbuka kwa miezi mingi juu ya haya majaribio magumu. Alipata faraja alipoomba kwa dhati kwa uelewa katika shahiri rahisi ambalo lilikuwa la kuenziwa. Lilinukuliwa majuzi na Rais Monson.

Mimi sijui ni kwa mbinu gani nadra,

Lakini najua hivi, Mungu hujibu maombi.

Mimi najua Kwamba Yeye ametoa neno Lake,

Ambalo linaniambia maombi daima usikika,

Na yatajibiwa, punde au baadaye.

Na kwa hivyo naomba na kungojea kimya.

Sijui ikiwa baraka ninazotaka

Zitakuja tu kwa njia ninayofikiria;

Bali acha maombi yanguKwake pekee,

Ambaye mapenzi yake ni busara kuliko yangu mwenyewe,

Nikiwa na hakika Yeye atajibu maombi yangu,

Au atatuma majibu fulani ya baraka zaidi.28

Kama vile wengi wetu, mama yangu bado anatafuta kuweka matumaini yake katika mapenzi Yake na wakati Wake. Tunapofanya hivyo, tunapaswa kukumbuka mafundisho haya kutoka kwa Mzee Richard  G. Scott. Dondoo: “Wewe unafanya nini wakati ushajitayarisha kwa makini, ushaomba kwa dhati, ushangoja kwa muda wa kutosha kwa jibu, na bado hauhisi jibu? Unaweza kutaka kutoa shukrani wakati haya yanatokea, kwani ni ushahidi wa matumaini kwa [Baba wa Mbinguni]. Unapoishi kwa ustahiki na chaguo lako linalingana na mafundisho ya Mwokozi na unahitaji kutenda, kuendelea kwa matumaini. Unapokuwa msikivu kwa minong’ono ya Roho, mojawapo wa vitu viwili hakika kitatokea katika wakati unaofaa: aidha mduwazo wa mawazo utatokea, kuonyesha chaguo lisilofaa, au amani inayochoma kifuani itahisiwa, kuthibitisha kwamba chaguo ni sahihi. Wakati unaishi kwa haki na unatenda kwa matumaini, Mungu hatakuacha usonge mbele sana bila kupatia onyesho la onyo ikiwa umefanya maamuzi yasiyo sahihi.”29

Sauti ya onyo ya Roho mara nyingi huja kupitia sauti ta watumishi wateule wa Bwana, ambayo sasa inatuleta katika ile pointi yetu inayofuata:

Nambari 9: Sikiliza maonyo ya kinabii.

Fikiria kwa makini maonyo ya kinabii machache katika siku zetu. Kwanza, machache kutoka kwa Rais Boyd  K. Packer. Dondoo:

Sasa onyo! Baadhi ya muziki ni wa unaangamizo sana kiroho… Mdundo,sauti, na maisha ya wale wanaoimba hufukuza Roho. Ni hatari sana kuliko unavyoweza kudhania, kwani unaweza kutuliza hisia zako za kiroho”

Onyo lingine:

“Kunaweza kuwa mafunuo gushi, minong’ono kutoka kwa ibilisi, majaribu!  …

“Kama kamwe utapokea mnong’ono wa kufanya jambo ambalo linakufanya ujihisi kuwa na wasi wasi, kitu ambacho unajua kwa akili yako ni kosa na kinyume na kanuni za haki, husijaribu!

Na hapa kuna linngine: “Kama mtu atakuwa mkosoaji na ana hisia hasi, Roho atajiondoa.” 30

Na nabii wetu mpendwa, Rais Thomas S. Monson, alipaza sauti ya onyo wakati alisema, “Kuweni macho kwa jambo lolote linaloweza kukuibia baraka za milele.” 31

Kwa nini tutuni mioyo yetu kwa sauti ya Roho? Ni baraka gani zitakuja tunapofanya hivyo?

Nimerudi tu kutoka Ufilipino ambapo niliona madhara ya haiyan tufani kali. Nilisikia yaliyowatokea ndugu na dada zetu wapendwa huko Ufilipino waliposhuhudia kuhusu kuwa unaogozwa na Roho katika ile dakika ya haja ili wajue kile cha kufanya na mahali pa kwenda. Niliwasikia wakisema juu ya kusonga mbele kwa imani wakati mapito si wazi. Mimi nimesikia hadithi za wamisionari vijana, kina dada kwa wazee, kufuata minong’ono ambayo inawaelekeza wao kwenye usalama wa mwili katikati ya ulimwenguni anaosambaratikana karibu na wao. Nina shukrani jinsi gani kwa “kipawa kisichosemeka cha Roho Mtakatifu,”32 ambaye huonya, huelekeza, hufariji na uongoza wale ambao wanaishi kwa ustahiki.

Kati ya vipawa vya Baba yetu wa Mbinguni ambavyo angachagua kuwapatia wana na mabinti Zake tunapoondoka kutoka maji ya ubatizo, Yeye alichagua kutupatia kipawa cha Roho Mtakatifu.

“Roho Mtakatifu hufanya kazi kikamilifu kwa umoja na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. …

Yeye ‘huwashuhudia Baba na Mwana’(2 Nefi 31:18) na hufunua na hufunza ‘ukweli wa vitu vyote.’ (Moroni 10:5). Tunaweza kupokea ushuhuda wa hakika wa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo tu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Mawasiliano Yake kwa roho yetu uwa na uhakika mwingi zaidi kuliko mawasiliano yoyote tunayoweza kupokea kupitia hisia zetu za asili.”33

Ndugu na akina dada, kama mnavyofahamu vyema, lile jengo kuu na pana lililojaa wale wanaotudhiaki na kutukejeli na kutuotea vidole vya fedhea linatuzingira sisi. Sauti ya uilmwengu ipo juu sana, haisiti, inashwishi, na inasisitiza. Isipokuwa tujifunze kutuni mioyo yetu kwa sauti ya Roho na kurekebisha uwezo wetu wa kutafuta, kupokea, na kutenda juu ya ufunuo wa kibinafsi, sisi tuko katika ardhi dhaifu sana. Tunahitaji sauti ya Roho kutuongoza sisi mbali na yote ambayo ni takataka, upumbavu, machafu, katili, choyo, na dhambi. Tunahitaji Roho Mtakatifu si tu kutuongoza sisi kwa kila kitu ambacho ni “chema, au cha kupendeza, chenye sifa njema na kusifiwa”34 bali kutusaidia sisi kukuza hamu kwa vitu hivyo ili kuzizuia na mvuto wa ulimwengu.

Mojawapo wa baraka bora tunazoweza kupokea tunapojifunza kusikia sauti ya Roho ni uwezo wa sisi kujiona wenyewe kama tunavyoonekana na Baba yetu wa Mbinguni na, “pole pole, kidogo kidogo,” kuwa bora tuwezavyo.

Fikiria hii dondoo nzuri kutoka kwa Mtume wa siku za mwisho: “Kipawa cha Roho Mtakatifu … huamusha akili zote, huongeza, hukuza, hupanua na husafisha hamu zote za kihalisi na upendo; na huzitohoa, kwa kipawa cha hekima, kwa matumizi yake ya kiahalali. Hutoa maongozi, huendeleza, hupalilia na hukomaza huruma yote, shangwe, ladha, hisia za jamii, na upendelo wa uhalisi wetu. Hutoa maongozi ya wema, ukarimu, uzuri, uororo, ungwana na hisani. Huendeleza urembo wa mtu, umbo, na hali. Hutunza afya, nguvu, bidii, na hisia za kijamii. Hutia nguvu sehemu zote za kimwili na akili ya mtu. Huimarisha, na hupatia toni kwa neva. Kwa kifupi, ni, uboho kwa mfupa, shangwe kwa moyo, nuru kwa macho, muziki kwa masikio, na uzima kwa kiumbe kizima.”35

Roho Mtakatifu anaweza kutufanyia sisi kimwili, kiroho, kihisia, kiakili na kielemu, ambacho dawa ambayo imetengenezwa binadamu inaweza kuiga.

Je! Haukubaliani nami kwamba kuishi kwa ustahiki kwa baraka kama hizo inastahili chochote kinachohitajika, hata kama inahitaji dhabihu kubwa? Ni “mkate” tunaopokea kwa mafananisho yetu ya “gamba la mkate” za juhudi. Nawaalika sisi sote kuanza usiku wa leo tutuni mioyo yetu kwa sauti ya Roho Mtakatifu.

Si kwa bahati kwamba Bwana alimuinua Rais Thomas  S. Monson kama nabii Wake aliye hai ili kutuongoza sisi katika hizi siku za mwisho. Rais Monson ni mtu ambaye amejifunza vyema kusikia na kujibu minong’ono ya Roho. Tutafanya vyema kufuata mfano wake.

Mimi nashuhudia kwamba yeye ni msemaji wa Bwana katika siku zetu. Pia nashuhudia kwamba Baba yetu aliye Mbinguni anatutaka sisi turudi katika uwepo Wake na ametoa njia kwetu ya kufanya hivyo kwa kumtoa Mwanawe wa Pekee na kipawa cha Roho Mtakatifu. Nashuhudia inastahili kila juhudi katika upande wetu kupokea na kubakiza kile kipawa kisichosema, katika jina la Yesu Kristo, amina.

©  2014 by Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifdhiwa. Kiingereza kiliidhinishwa: 1/14. Tafsiri Iliidhinishwa: 1/14. Tafsiri ya Tuning Our Hearts to the Voice of the Spirit. Swahili. PD10050686 743

Muhtasari

  1. Melvin J. Ballard, in Henry B. Eyring, “Opportunities to Do Good,” Ensign or Liahona, May 2011, 25.

  2. 3 Nefi 9:20.

  3. Ona Hubiri Injili Yangu: A Guide to Missionary Service (2004), 89–102.

  4. Alma 5:26.

  5. Moroni 7:16–17.

  6. Teachings of Gordon B. Hinckley (1997), 261.

  7. Jeffrey R. Holland, “Wrong Roads,” Mormon Messages video; lds.org/media-library/video.

  8. Mafundisho na Maagano 112:10; mkazo umeongezewa.

  9. Teachings of Presidents of the Church: Spencer W. Kimball (2006), 246–47.

  10. Joseph Smith—Historia 1:10.

  11. Joseph Smith—Historia 1:8, 13.

  12. Joseph Smith—Historia 1:18.

  13. From On the Lord’s Errand: The Life of Thomas S. Monson; lds.org/media-library/video.

  14. Robert D. Hales, “Holy Scriptures: The Power of God unto Our Salvation,” Ensign or Liahona, Nov. 2006, 26–27.

  15. Helamani 11:23.

  16. Teachings of Presidents of the Church: Harold B. Lee (2000), 54–55.

  17. Alma 17:3; mkazo umeongezewa.

  18. Teachings of Presidents of the Church: George Albert Smith (2011), 117.

  19. Mosia 21:15.

  20. Ona Moroni 4:3.

  21. Mafundisho na Maagano 109:15; mkazo umeongezewa.

  22. Mafundisho na Maagano 6:12.

  23. Richard G. Scott, “How to Obtain Revelation and Inspiration for Your Personal Life,” Ensign or Liahona, May 2012, 46.

  24. Teachings: Harold B. Lee, 54.

  25. Robert D. Hales, “Personal Revelation: The Teachings and Examples of the Prophets,” Ensign or Liahona, Nov. 2007, 87–88.

  26. Corrie ten Boom, with Elizabeth and John Sherrill, The Hiding Place, 35th anniversay ed. (2006), 12.

  27. Dallin H. Oaks, “In His Own Time, in His Own Way,” Ensign, Aug. 2013, 22, 24.

  28. Eliza M. Hickok, “Prayer,” in James Gilchrist Lawson, ed., The Best Loved Religious Poems, Gleaned from Many Sources (1933), 160.

  29. Richard G. Scott, “Using the Supernal Gift of Prayer,” Ensign or Liahona, May 2007, 10.

  30. Boyd K. Packer, “Personal Revelation: The Gift, the Test, and the Promise,” Ensign, Nov. 1994, 61.

  31. Thomas S. Monson, “May You Have Courage,” Ensign or Liahona, May 2009, 125.

  32. Mafundisho na Maagano 121:26.

  33. Gospel Topics, “Holy Ghost”; LDS.org.

  34. Makala ya Imani 1:13.

  35. Parley P. Pratt, Key to the Science of Theology, 5th ed. (2000), 101–2.