Kupata Uzoefu wa Nguvu za Ukuhani
Wanawake ambao wanasaidia kuongoza Kanisa waliulizwa jinsi nguvu za ukuhani zinavyogusa maisha yao. Hapa ni baadhi ya mawazo waliyotoa.
Wanaume na wanawake wana majukumu tofauti lakini yenye muhimu ulio sawa nyumbani na katika Kanisa. Nguvu za ukuhani zinaweza kumsaidia kila mtu kutekeleza majukumu hayo kwa manufaa ya wote.
“Kwa sababu nguvu za ukuhani wa Mungu ziko duniani leo, baraka kuu zinapatikana kwa waumini wote wenye kustahili, iwe ni wazee au vijana, wanaume, au wanawake, waseja au wameoa au kuolewa.
—Rais Joy D. Jones, Rais Mkuu wa Msingi
“Huduma hukuza nafsi zetu, hupanua mtazamo wetu na huturuhusu kusogea kwenye nguvu za Mungu kwa wingi sana. Bwana anajua hili, na Shetani vivyo hivyo. Katika jaribio lake daima kututenganisha na nguvu za Mungu, adui atatuzidia au kutufanya tuhisi kwamba kile tunachofanya hakitoshi. …
“… Kamwe usipuuze kitendo cha ukarimu.
“Kwa kusudi kufanya huduma kwa wengine kuwa sehemu ya maisha yetu, tutagundua siri za Mungu. Tutagundua amani, tutapata nguvu, na kupokea ongezeko la nguvu tunapomtumikia Mwokozi wetu, Yesu Kristo.”
—Rais Bonnie H Cordon, Rais Mkuu wa Wasichana
“Mara nyingi sana, wanawake hujilinganisha wenyewe na watu wengine. Lakini hakuna kati yetu anayejisikia vyema katika kulinganisha huko. Kila mwanamke anayo aina ya kipekee ya uwezo na vipaji, na hivi vyote ni zawadi zilizotolewa na Mungu. Kwa sababu tu mimi na wewe hatuko sawa—au idadi yoyote ya wanawake sio ile ile—hii haitufanyi sisi kuwa wapungufu au zaidi. Tunahitaji kutafuta vipawa vyetu na kuvikuza, tukikumbuka ni nani aliyetupatia, na kisha tuvitumie kwa madhumuni Yake. Tunaposhiriki vipawa vyetu ili kuwabariki wengine, tutaona nguvu ya ukuhani katika maisha yetu.”
—Rais Jean B. Bingham, Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama
“Kila mara tafuta kuongezea uelewa wako juu ya ‘mafundisho ya ukuhani.’ Kila mmoja wetu anahitaji kutafuta uelewa huu yeye mwenyewe.
“Kujifunza maandiko na maneno ya manabii wa sasa kutatoa msingi mzuri wa maarifa haya kukua. Vivyo hivyo utiifu wa amri za Mungu na kuishi kweli kwa maagano tuliyofanya kupitia ibada za ukuhani. Uelewa umetolewa kwetu, ‘mstari juu ya mstari, kanuni juu ya kanuni’ [2 Nefi 28:30]. Kupitia ufunuo binafsi, ‘yatatonatona’ juu ya nafsi zetu ‘kama umande utokao mbinguni’ [Mafundisho na Maagano 121:45].”
—Dada Lisa L. Harkness, Mshauri wa Kwanza katika Urais Mkuu wa Msingi
“Kila mmoja wetu yuko safarini. … Tunasafiri kupitia changamoto za uhusiano, changamoto za kifedha, na changamoto za afya ya kiakili na kimwili. Tunasafiri kupitia wajibu mgumu na orodha ya vitu vya kufanya kila siku. Baadhi yetu wanaweza kuwa wanasafiri kupitia huzuni, au hata upweke au uchoshi. Changamoto zetu ni tofauti, lakini wote tunazo.”
“Kushika maagano yetu haimaanishi kwamba hizi changamoto zitaondolewa, lakini inamaanisha kwamba Bwana anaahidi kuwa nasi.”
—Dada Michelle D. Craig, Mshauri wa Kwanza katika Urais Mkuu wa Wasichana
“Ninachukulia nguvu za ukuhani kama uzi mmoja, laini, mwororo mweupe ambao unatoka kwa Mungu na umesukwa nje ndani na kitanzi, unaonekana kuwa na mwelekeo wake wenyewe katika maisha yetu. Lakini baada ya muda mfumo mgumu hufunuka. Huu usanifu hufunika madhabahu ya Mungu, mahali patakatifu zaidi ambapo tunafunga duniani na tunafunga mbinguni. …
“Ninapoona kitambaa cha madhabahu kwenye hekalu takatifu, ninahisi ni mojawapo ya ishara zenye uweza wa jinsi Bwana anavyoazimisha nguvu Zake kwa watoto Wake walio waaminifu ili kukusanya na kuzifunga pamoja katika usanifu mgumu na ulio mtakatifu.”
—Dada Silvia H. Allred, Mshauri wa Kwanza katika Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama.
“Kupitia uzeofu wa maisha yangu mwenyewe, ninajua kwamba kushika amri za Bwana, kuwa na imani, na kumuamini Yeye kiukamilifu ni njia za kupata nguvu za ukuhani Wake.
”… Tunapobakia waaminifu, tunaweza kupokea hizo nguvu za ukuhani na baraka katika hali zote za maisha yetu. Inaweza kutupatia ulinzi, faraja, nguvu, amani, na ahadi ambazo zinafikia kwenye milele yote. Kupitia hiyo nguvu ya ukuhani, Roho Mtakatifu pia hunisaidia kukumbuka matukio katika maisha yangu ambayo yanaendelea kujenga ushuhuda wangu na imani yangu katika Mungu.”
—Dada Cristina B. Franco, Mshauri wa Pili katika Urais Mkuu wa Msingi
“Miaka imepita tangu nipokee baraka yangu ya kipatriaki, lakini nakumbuka tukio hili wazi kabisa. …
“Tukio hilo limeongoza maamuzi mengi niliyofanya kote katika maisha yangu. Nilijua ili kufikia hizo baraka tamaniwa, ningepaswa kutenda sehemu yangu.
“Sasa naona kwamba kuna hata zaidi ambayo Baba yetu anataka mimi nipokee, hata zaidi kuliko kilichotajwa katika baraka yangu ya kipatriaki.”
—Dada Mshauri wa Pili katika Urais Mkuu wa Wasichana
“Nilijiunga na Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho nikiwa na umri wa miaka 26. Ingawa nilipata hisia za kutuliza katika moyo wangu nilipofuata shauku ya kubarikiwa na Mungu kwa kufanya agano Naye, najua kwamba uelewa wangu wa agano hilo ilikuwa ni kama mbegu ndogo wakati huo.
“Kadiri miaka ilivyosonga mbele na nilivyofanya juhudi za kushika lile agano la ubatizo na maagano mengine niliyofanya na Baba wa Mbinguni, ninahisi kwamba Yeye amenibariki na uelewa wa kina kumhusu Yeye, kuhusu Mwokozi wangu, na kuhusu nafasi yangu kama binti wa agano wa Wazazi wa Mbinguni.
—Dada Reyna Isabel Aburto, Mshauri wa Pili Katika Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama