2021
Yesu Kristo Alituokoa Sisi kutokana na Dhambi na Kifo.
Machi 2021


Misingi ya Injili

Yesu Kristo Alituokoa Sisi kutokana na Dhambi na Kifo

Kwa sababu ya dhabihu Yake, sisi sote tuna nafasi ya kupata amani na furaha ya milele.

the Savior in Gethsemane

Kristo Akiumba Dunia, na Robert T. Barrett; Ee Baba Yangu, na Simon Dewey; Mazishi ya Kristo, na Carl Heinrich Boch; Kristo Akiwaaita Petro na Andrea, na James Taylor Harwood

Tunamtaja Yesu Kristo kama Mwokozi wetu. Hiyo ni kwa sababu Yeye alilipia thamani ya dhambi zetu na kuzishinda nguvu za kifo. Yeye alituokoa! Dhabihu Yake kwa ajili yetu, inaitwa Upatanisho, ni tukio muhimu zaidi ambalo limeshapata kutokea. Kwa sababu Yake, kifo sio mwisho. Kwa sababu Yake, tunaweza kusamehewa dhambi zetu, kuwa safi tena, na kukua tukiwa bora kila siku.

Yesu Kristo akiwa Mzaliwa wa Kwanza

Kabla ya kuja duniani, tuliishi pamoja na wazazi wetu wa mbinguni. Kama Mzaliwa wa Kwanza, Yesu Kristo alisaidia kuumba ulimwengu. Alichaguliwa kuwa Mwokozi wetu na alikubali kuzaliwa duniani ili Yeye aweze kuweka mfano kamili, kufundisha injili Yake, na kukamilisha Upatanisho kwa ajili yetu.

Yesu Kristo Alilipia Dhambi Zetu

Wakati Yesu alipojua kwamba angekufa hivi karibuni, alienda kwenye bustani iliyoitwa Gethsemani kusali. Wakati huo wa sala, Yeye alianza kulipia thamani ya dhambi zetu, Kwa hiyari aliteseka ili kwamba sisi tusihitajike kufanya hivyo, kama tutatubu. Tunapogeuka kutoka kwenye dhambi zetu na kumfuata Mwokozi, tunaweza kupata msamaha na uponyaji. Katika njia tusiyoweza kuelewa, Yesu anaelewa kwa ufasaha hasa vile ilivyo kwa kila mmoja wetu. Alihisi huzuni yote, maradhi yetu na uchungu wetu. Hii ni sehemu ya kwanza ya Upatanisho.

Yesu Kristo Alishinda Kifo

burial of Jesus

Kristo Akiumba Dunia, na Robert T. Barrett; Ee Baba Yangu, na Simon Dewey; Mazishi ya Kristo, na Carl Heinrich Boch; Kristo Akiwaaita Petro na Andrea, na James Taylor Harwood

Baada ya sala katika Gethsemane, Yesu alisalitiwa, akakamatwa, na kuhukumiwa kifo kwa kusulubiwa. Ingawa Yeye alikuwa na uweza wote, Yesu aliruhusu mwenyewe kufa msalabani. Wafuasi Wake waliuweka mwili Wake katika kaburi. Hawakutambua kwamba ingawa mwili Wake ulikuwa umekufa, roho Yake ilikuwa bado hai katika ulimwengu wa roho. Siku tatu baadaye, Yesu alikuwa hai tena na kuwatembelea wao, kuthibitisha kwamba anaweza kushinda kifo. Kwa sababu Yesu alifufuka, kila mmoja wetu ataishi baada ya sisi kufa. Hii ilikamilisha Upatanisho.

Umuhimu wa Krismasi na Pasaka

Watu wengi ulimwenguni husherekea hizi siku kuu mbili ambazo zinatusaidia kukumbuka Upatanisho wa Yesu Kristo. Wakati wa Krismasi, tunakumbuka kwa shukrani kwamba Yesu alikuwa radhi kukubali misheni ya kuja duniani, ingawa kwamba ilijumuisha kuteseka na kufa kwa ajili yetu. Pasaka tunasherekea ushindi wa Mwokozi dhidi ya dhambi na kifo, ambayo hutupatia tumaini kwa ajili ya kudra ya milele ya furaha.

Maandiko Yanasema Nini kuhusu Upatanisho wa Mwokozi?

Kwa sababu Yesu anatujua sisi kikamilifu, Yeye anaweza “kutusaidia” (ona Alma 7:11–12).

Manabii wa kale walishuhudia kwamba Mwokozi ataelewa huzuni yetu na manung’uniko yetu (ona Isaya 53:2–5).

Mungu alimtuma Yesu kutuokoa kwa sababu Mungu anampenda kila mmoja wetu (ona Yohana 3:16–17).

Yesu alisali kwa ajili ya wafuasi Wake, ikijumuisha sisi, ili tulindwe kutokana na uovu na kuwa wamoja pamoja na Yeye na Baba wa Mbinguni (ona Yohana 17).

Mwokozi wetu anatualika tumfuate Yeye na kurudi katika uwepo Wake (ona Mafundisho na Maagano 19:16–19, 23–24; 132:23)