Njoo, Unifuate
Fumbo la Kabaila: Fundisho katika Utiifu
Mafundishi na Maagano 101:43–62 inatoa fumbo ambalo lilitolewa kuelezea kwa nini Watakatifu walifukuzwa kutoka Missouri.
Katika fumbo, mtumwa anaanza kujenga mnara lakini baadae anaamua kwamba “hakuna uhitaji” kwa ajili yake (Mafundisho na Maagano 101:49). Ila kwa sababu hawajengi mnara, hawana tahadhari wakati adui atakapovunja na kuharibu shamba la mizabibu.
Je, niliwahi kuhoji juu ya amri za Mungu?
Mmewahi, kama watumushi, kuwahi kushangaa ikiwa amri ilikuwa hakika ya lazima? Fumbo hili linatufundisha kwamba amri za Bwana hutulinda na kutusaidia sisi kuishi maisha ya furaha (ona pia Mosia 2:41; Mafundisho na Maagano 82:8–10).
Je, tunaweza kufanya nini kama hatuoni uhitaji wa amri?
-
Jifunze mada na usali katika Bwana kutusaidia “kuhisi kwamba ni sahihi.” (Mafundisho na Maagano 9:8).
-
Kumbuka nyakati katika siku za kale wakati utiifu ulipoleta baraka.1
-
Tenda katika imani, tukiamini kwamba tutaelewa “baada ya majaribu ya imani [yetu]” (Etheri 12:6).