Kanisa Liko Hapa
Riga, Latvia
Picha
view of city of Riga, Latvia
Picha kutoka stock.adobe.com
Riga, mji mkuu wa Lativia, ni bandari ya mtoni kutoka kwenye mdomo wa Mto Daugava. Tawi la kwanza la Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho katika Lativia liliundwa katika Riga mwaka wa 1993. Leo, Riga ni makao ya Misheni ya Baltic. Kanisa katika Lativia lina:
Waumini 1,272
Makusanyiko 5
Misheni 1
Muda wa Pamoja
Picha
family walking together in city
Kitu rahisi kama vile kutembea kupita kwenye mji kunaweza kutoa burudani nzuri. “Hakuna mbadala wa kutumia muda pamoja,” anasema Aleksandr Samigullin wa Riga, ambaye hufurahia kuwa na mke wake, Svetlana, na watoto wao.