Karibu kwenye Toleo Hili
Heshima kwa Watoto Wote wa Mungu
Rais Russell M. Nelson ametualika “kupanua mduara wetu wa upendo ili kukumbatia familia yote ya mwanadamu.” (Mafundisho ya Russell M. Nelson [2018], 83). Tukiwa na utofauti mwingi miongoni mwa watoto wa Mungu, je, tunawezaje kutengeneza jamii ambayo watu wote wataishi kwa amani?
Katika makala yake “Kuileta Sayuni” (ukurasa wa 12), Mzee Gerrit W. Gong wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili anatualika kuunganisha mioyo na akili zetu tunapowaalika wote kuja kwa Kristo. “Kushinda Ubaguzi wa Rangi na Chuki: Tunaweza Kujenga Madaraja” (ukurasa wa 18) yanayoweza kutusaidia katika juhudi zetu za kuwa wamoja. Kwa hakika, kuwa wamoja kunajumuisha kujichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo kama kanisa, lakini pia kama watu binafsi. Jifunze zaidi katika “Hivyo Ndivyo Litakavyoitwa Kanisa Langu” na Rais Henry B. Eyring (ukurasa wa 8).
Kuunda umoja katika utofauti wetu si tu ni amri (ona Yohana 17:21; Mafundisho na Maagano 38:27), lakini pia ni fursa ya sisi kujifunza kutoka kwa, na kubarikiwa na kaka na dada zetu wa tamaduni zingine, makabila na uzoefu. Tunatumaini toleo la mwezi huu litatusaidia sote kuishi kwa umoja zaidi katika Kristo.
Kwa moyo wa dhati,
Mzee Walter F. González
Wa Sabini
Mshauri wa jarida la Liahona