Msaada kutoka Upande Mwingine wa Pazia
Wakati nimelala kwa maumivu hospitalini, nilijisikia mpweke mpaka nilipowakumbuka mababu zangu wa kale.
Mnamo mwaka 2017, nilipata ujauzito wa mtoto wetu wa kwanza. Mume wangu, Lukas, na mimi tulijawa na shangwe lakini na woga wa ujio wa kichanga Juan Lionel.
Usiku mmoja mwanzoni mwa Februari 2018, nilianza kushikwa na uchungu. Nilikuwa na miezi nane, lakini ilionekana kwamba mtoto wetu angeweza kuja mapema kuliko ilivyotazamiwa. Tulibeba vitu vichache na kukimbilia kliniki. Sikujisikia tayari kwenda chumba cha uzazi, ila nilisali, nikimwomba Mungu kwamba mapenzi Yake yatimie licha ya hofu yetu.
Tulipofika kliniki, dakitari wangu wa magonjwa ya wanawake alitaarifiwa ila alisema asingeweza kufika wakati huo ila baadae. Mume wangu alipiga simu na kutuma ujumbe kwa wazazi wetu na ndugu, ila hakuna hata mmoja kati yao alikuwa macho. Aliendelea kupiga simu na kutuma ujumbe usiku kucha, ila hakuna hata mmoja aliyeitikia. Hilo lilinifanya nijisikie mpweke.
Kadiri maumivu kutokana na uchungu wa kuzaa yalivyoongezeka, nilijisikia zaidi na zaidi mpweke. Ghafla, hata hivyo, jambo la kustaajabisha lilitokea. Nilianza kuwafikiria mababu zangu wa kale—hususani bibi yangu mzaa mama, Rosa Mercado, na mama yake, Javiera Balmaceda.
Kadiri nilivyowakumbuka, nilijihisi moyoni mwangu na akilini kwamba wote walikuwa na mimi kwa wakati huo. Nilihisi uwepo wao kwa njia ambayo ni ya nguvu na kuvutia ambayo siwezi kuielezea kiundani kwa maneno nilivyohisi. Sikuweza kuwaona, ila nilihisi kuwa karibu nao, wakinipa hamasa, wakiniunga mkono, na upendo kama mama zangu na kama sehemu ya familia yangu. Nilihisi kwamba walikuwa kama malaika wakinihudumia wakati wa uhitaji wangu.
Miaka kadhaa ya nyuma hekaluni, mama yangu, baba, ndugu, mume, na mimi tulifanya kazi ya uwakala na uwakala wa mababu zetu wengine. Niljisikia ujasiri ule nilioupokea na hisia nilizokuwanazo kwamba mababu zangu walikuwa karibu ilikuwa ni zawadi kupitia nguvu na mamlaka kutoka kwa Mungu.
Tangu wakati huo, nimehisi roho ya mababu zangu katika matukio mengine, wakinisaidia na kuniongoza kama mama na mke na katika nyanja nyingine za maisha yangu.
Nashuhudia kwamba Mungu hatatuacha peke yetu katika njia ya maisha yetu. Tukifanya kazi Yake, tutapata msaada kutoka ule upande mwingine wa pazia. Tutapokea upendo, maarifa, nguvu, na amani “ambavyo hupita uelewa wote” (Wafilipi 4:7).