2021
“Kwani Hivyo Ndivyo Kanisa Langu Litakavyoitwa”
Septemba/ Oktoba 2021


“Kwani Hivyo Ndivyo Kanisa Langu Litakavyoitwa”

Tunapotumia jina kamili la Kanisa, tunabarikiwa na tunawabariki wengine.

various people walk by a Church sign in Korean

Katika Afrika, watu binafsi wanaolitafuta kanisa kujiunga hutoa taarifa ya kuwa na ndoto. Katika ndoto zao, walielekezwa kutafuta kanisa linaloitwa kwa jina la Yesu Kristo. Wakati walipotafuta, walikuta Kanisa pekee ambalo jina la Mwokozi ndicho kiini—Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Katika Amerika ya Latini, Watakatifu wengi wa siku za Mwisho waliarifu kwamba mialiko yao kwa marafiki kuhudhuria “Kanisa la Mormoni” walikutana na kuchanganyikiwa. Hiyo ilibadilika walipotoa mwaliko kwa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. “Ikiwa kanisa lako linaitwa Kanisa la Yesu Kristo,” rafiki zao waliitikia, “tungependa kuja na kuona.”

Katika Marekani, mvulana wa Msingi aliwaalika jirani zake kwenye ubatizo wake. Mchungaji wa imani nyingine alisema asingeweza kwenda kwenye ubatizo wa “Kanisa la Mormoni” Ila kwa sababu aliona kanisa la mvulana yule lililenga juu ya Yesu Kristo, mchungaji alihudhuria na mke wake.

Wakati wakala wa safari za ndege alipomuuliza muumini wa Kanisa anwani ya barua pepe, muumini alijibu, “ldschurch.org.”

“Hilo ni kanisa gani?” wakala aliuliza.

“Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho,” muumini alijibu.

“Huwa naenda kazini katika siku ambazo muda mwingine huwa siwezi kusema neno kuhusu Bwana,” wakala alisema. “Kujua kwamba naongea na Mkristo mwingine huifanya siku yangu kuwa nzuri.”

Kwa haraka muumini wa Kanisa alisasisha taarifa zake za shirika la ndege kwa anwani mpya ya barua pepe ya Kanisa: ChurchofJesusChrist.org.1

Ahadi Ilitimizwa

family walking in front of a Church building

Hadithi hizi za kushangaza zinawakilisha utimilifu wa ahadi ambayo Rais Russell M.Nelson alitoa kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho mnamo Oktoba 2018 na tena mnamo Aprili 2020.

“Ninawaahidi kuwa kama tutafanya bidii kurejesha jina sahihi la Kanisa la Bwana, Yeye ambaye hili Kanisa ni Lake atatoa nguvu Zake na baraka juu ya vichwa vya Watakatifu wa Siku za Mwisho, ambazo hatujapata kuona,” Rais Nelson alisema. “Tutapata uelewa na nguvu za Mungu kutusaidia kupeleka baraka za injili ya urejesho ya Yesu Kristo katika kila taifa, ukoo, ndimi, na watu, kusaidia kuuandaa ulimwengu kwa Ujio wa Pili wa Bwana.”2

Hivi karibuni, kupitia ukurasa wangu wa taarifa za kijamii, niliwaalika waumini wa Kanisa kuniambia baraka ambazo wamezipata kutokana na kutumia jina sahihi la Kanisa. Niliguswa kwa kupokea majibu zaidi ya 2,600.

Ningependa kushiriki nanyi baadhi yake. Yataonekana ya kawaida kwenu sababu mmewahi nanyi kupokea baraka kama hizo kadiri mlivyofuata ushauri wa Rais Nelson.

Karibu zaidi na Yesu Kristo.

Nilisukumwa na ushuhuda wa Jacob jinsi ambavyo jina kamili la Kanisa lilimsaidia kuzingatia Mwokozi: “Nimegundua kwamba kuzingatia kwangu kwa Yesu Kristo kumezama katika kila jambo kwenye maisha yangu,” alishiriki nami. “Ninapopokea sakramenti, ninamfikiria Yeye na dhabihu Yake ya upatanisho. Ninaposoma maandiko, nazingatia sana kwenye maneno Yake na marejeo Yake mengine. Hii imenileta karibu zaidi na Yeye na imenisaidia kuelewa vizuri kazi Yake kama Mwokozi na Mkombozi wangu.”

Nilijihisi kubarikiwa nilipojifunza jina la Mwokozi linamaanisha nini kwa Beth na Bryce: “Nimejisikia muunganiko wa karibu kwa Mwokozi wangu,” Beth alisema. “Ninapoulizwa Kanisa gani huwa naenda, na ninajibu kwamba mimi ni wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, najihisi kiuhakika kuwa mmoja wao. Mimi ni mmoja wa watu Wake. Ni wafamilia Yake. Mimi ni Wake.”

Bryce aliniambia kwamba jina sahihi la Kanisa humsaidia yeye “kukumbuka nani ninamtumikia na ni nani natafuta kuwa kama yeye zaidi. Hunikumbusha kwamba Mwokozi ndiye anayetoa mafundisho haya na kwamba hayatoki kwa watu.”

“Jina la Mwokozi Lina Nguvu”

Christus statue

Haley, mmisionari wa kudumu, alisema: “Kutumia jina sahihi la Kanisa la Mwokozi huleta nguvu zaidi na mamlaka tunapowafundisha wengine juu ya injili Yake ya urejesho. Nnaposema ‘Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho,’ Roho wa Bwana ananithibitishia na kunishuhudia kwamba hili ni Kanisa la Bwana lililorejeshwa duniani leo. Mimi napenda kutumia jina sahihi sababu naongezea pia ushuhuda wangu uliohai juu ya ukweli huu!”

Na Nicola aliniambia: “Kabla ya hapo, ikiwa nilisema ‘Mormoni,’ mara kwa mara pangekuwepo utata na kutokuwa na uhakika kwa wale ambao sio wa imani yetu. Ungeweza kusikia kwa uharaka wa kumbukumbu wa yote ambayo wamesikia kuhusu ‘Wamormoni.’ Ila kwa sasa kuna amani, ambayo kwa zaidi inakubalika. Jina la Mwokozi lina nguvu. Yeye huleta amani. Ushuhuda wangu wa ukweli wa injili umekua kwa sababu ya kusema jina sahihi la Kanisa. Ninamhisi Roho wakati wote ninapolitamka. Wakati mwingine ndicho ninachoweza kusema katika yale tunayoamini, ila inatosha.”

Kufafanua Dhana Potofu

Harold, profesa wa chuo kikuu katika Marekani, alisema kwamba kutumia jina kamili la Kanisa imemsaidia kufafanua dhana potofu. Aliniambia kwamba mwanafunzi mmoja, akijaribu kufupisha mjadala kuhusu dini, alitamka, “nadhani dini zote ni Wakristo, isipokuwa Wamormoni.”

Aliona ni wakati mzuri wa kuondoa dhana potofu, Harold alisema, “niliwambia wanafunzi kuwa ‘Mormoni’ lilikuwa jina la utani walilopewa waumini wa Kanisa kwa sababu ya imani yetu kwenye Biblia na Kitabu cha Mormoni kama maandiko yote ya kale yanavyomshuhudia Yesu Kristo.”

Maria alifungua moyo wake kwangu, na kushiriki jinsi jina kamili la Kanisa lilivyombariki katika kuwafundisha watoto wake: “Watoto wangu hawachanganyikiwi sana ninapowafundisha kuwa sisi ni Watakatifu wa Kanisa la Yesu Kristo katika siku hizi za mwisho badala ya kujiita wenyewe kama Wamormoni.’ Walikuwa wakichanganyikiwa na kuuliza, ‘Kwa nini Mormoni? Hii inamaanisha kwamba sisi sio Wakristo?’ Nahisi kwamba mabadiliko yamewasaidia wanapoongea na watoto wengine shuleni ambao sio waumini.”

“Mimi ni Mmisionari wa Yesu Kristo”

Rais Nelson aliahidi kwamba tutakapotumia jina sahihi la Kanisa, “tutakuwa na maarifa na nguvu za Mungu” kueneza injili. Teresa alinihamasisha na hadithi yake kuhusu kilichotokea wakati rafiki yake alipomuliza kuhusu Kanisa. Kufuatia ushauri wa Rais Nelson, Teresa alianza kwa kushiriki jina kamili la Kanisa.

“Alipendezwa na Kanisa,” aliniambia. “Alilichunguza kwa miezi kadhaa na baadae, kimiujiza, alibatizwa na mtoto wangu wa kiume, askofu. Nilihisi furaha kwa siku hiyo, na familia yangu pia. Ahadi ni za kweli.”

Jordan alisema kwamba watu wengi bado hawana mazoea na jina la Kanisa. “Kutumia jina kamili la Kanisa,” alisema, “hunipa mimi nafasi ya kueleza ni kwa jinsi gani Kanisa limejikita katika Yesu Kristo na kwa nini tunajiita Watakatifu wa Siku za Mwisho.”

Wakati mwanaume mmoja alipomuuliza Chloe kama alikuwa “Mmisionari wa Kimormoni,” kwa nguvu alishuhudia, “Hapana, Mimi ni Mmisionari kwa ajili ya Yesu Kristo.” Chloe aliniambia mwanaume huyo alielezea tamaa yake ya kumfuata Mwokozi, kwa hiyo alimfundisha kuwa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho linaongozwa na Mwokozi. Baadae alimpa maelezo kuhusu Kanisa Lake.

“Mliite kanisa katika Jina Langu”

sister missionaries talking to a family in front of a Church building

Katika Kufunua jina la Kanisa Lake kwa Nabii Joseph Smith, Mwokozi alitamka, “Kwani hivyo ndivyo kanisa langu litakavyoitwa katika siku za mwisho, hata Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho” (Mafundisho na Maagano 115:4). Na kwa Wanefi, alisema, “Mtaliita kanisa kwa jina langu,” kwani “linawezaje kuwa kanisa langu isipokuwa liitwe kwa jina langu?” (3 Nefi 27:7, 8).

Ninashuhudia pamoja na Mtakatifu wa Siku za Mwisho kwa jina Tommie kwamba tunapotumia jina kamili la Kanisa, tunabarikiwa na kuwabariki wengine. Tommie aliniambia, “Ninaposhiriki na wengine baraka za kuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho katika nyakati ugomvi na hofu umekithiri, natambua ninasaidia wengine kujua kwamba kuna kimbilio kutoka kwenye kimbunga kwa ajili ya wafuasi wa Yesu Kristo, ambaye huwajali na wale wanaomfuata Yeye.”

Muhtasari

  1. Namshukuru Mzee Gerrit W. Gong wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawilii kwa kushiriki hadithi hizi nami.

  2. Russell M. Nelson, “Jina Sahihi la Kanisa,” Liahona, Nov. 2018, 89; ona pia “Kufungua Mbingu kwa Msaada,” Liahona, Mei 2020, 73.