2021
Amani Binafsi katika Nyakati zenye Changamoto
Novemba 2021


“Amani Binafsi katika Nyakati zenye Changamoto,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Nov. 2022.

Kikao cha Jumapili Asubuhi

Amani Binafsi katika Nyakati zenye Changamoto

Dondoo

machweo ya jua kwenye ghuba yenye gati

Amani ulimwenguni haijaahidiwa wala kuthibitishwa mpaka Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. …

Hata hivyo, amani binafsi inaweza kupatikana licha ya hasira, ubishi na mgawanyiko ambao unaharibu na kuchafua ulimwengu wetu leo. Kamwe haijawa muhimu zaidi kutafuta amani binafsi kama sasa. …

Wakati kamwe hatutarudi nyuma kutoka kwenye juhudi za kufanikisha amani ulimwenguni kote, tumehakikishiwa kwamba tunaweza kuwa na amani binafsi, kama Kristo anafundisha. Kanuni hii imewekwa wazi katika Mafundisho na Maagano: “Lakini jifunzeni ya kwamba yeye afanyaye matendo ya haki atapata thawabu yake, yaani, amani katika ulimwengu huu, na uzima wa milele katika ulimwengu ujao.” [Mafundisho na Maagano 59:23].

Ni zipi baadhi ya “kazi za haki” ambazo zitatusaidia kushughulikia mabishano, na kupunguza ukinzani na kupata amani katika ulimwengu huu? Mafundisho yote ya Kristo yanaelekeza kwenye mwelekeo huu. Nitataja kazi chache ambazo ninaamini kwa kipekee ni muhimu.

Kwanza: Mpende Mungu, Ishi Amri Zake, na Samehe Kila Mtu …

Pili: Tafuta matunda ya Roho …

Tatu: Tumia Uhuru wa Kujiamulia Kuchagua Haki …

Nne: Jenga Sayuni katika Mioyo Yetu na Majumbani …

Tano: Kufuata Onyo la Sasa la Nabii Wetu …

Ninashuhudia na kutoa ushahidi wangu binafsi wa kitume kwamba Yesu Kristo, Mwokozi na Mkombozi wa ulimwengu, analiongoza na kulilinda Kanisa Lake la urejesho. Maisha yake na kazi ya upatanisho ni vyanzo vya kweli vya amani. Yeye ni Mwana Mfalme wa Amani.