2021
Huruma ya Kudumu ya Mwokozi
Novemba 2021


“Huruma ya Kudumu ya Mwokozi,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Nov. 2022.

Kikao cha Jumamosi Asubuhi

Huruma ya Kudumu ya Mwokozi

Dondoo

Yesu Kristo akimponya msichana

Moja ya kanuni muhimu sana zilizofundishwa na Mwokozi wakati wa huduma Yake duniani ilikuwa ni kuwatendea wengine kwa huruma. …

… Mwokozi alitenda kwa huruma kwa wote ambao wangekuja Kwake—bila ubaguzi—na hasa zaidi kwa wale ambao walihitaji zaidi usaidizi Wake. …

… Onyesho la huruma kwa ajili ya wengine ni, kwa ukweli, kitovu cha injili ya Yesu Kristo na alama iliyowekwa ya ukaribu wetu wa kiroho na kihisia kwa Mwokozi. …

… Kama yule mwanamke mwenye dhambi na yule mjane wa Naini, watu wengi katika maeneo tunayoishi wanatafuta faraja, kusikilizwa, kujumuishwa, na msaada wowote tunaoweza kuwapatia. Sisi sote tunaweza kuwa vyombo mikononi mwa Bwana na kuwatendea kwa huruma wale wenye mahitaji, kama vile Yesu alivyofanya. …

… Hatupaswi kufanya hukumu ya haraka na katili kwa majirani zetu, kwa sababu sote tunahitaji kusikilizwa na rehema kwa ajili ya madhaifu yetu kutoka kwa Baba yetu mpendwa wa Mbinguni. …

Wapendwa marafiki zangu, ninashuhudia kwamba tunapojitahidi kuhusisha mfano wa huruma ya Mwokozi ndani ya maisha yetu, uwezo wetu wa kusifu wema wa majirani zetu utaongezeka na hisia zetu za asili za kuhukumu mapungufu yao utapungua. Ushirika wetu na Mungu utakua, na kwa hakika maisha yetu yatakuwa matamu zaidi, hisia zetu zitakuwa nyororo zaidi, na tutapata chanzo kisichokauka cha furaha. Tutafahamika kama wapatanishi, ambao maneno yao ni ya upole kama umande wa asubuhi ya majira ya kuchipua.