2021
Naomba Yeye Atutumie Sisi
Novemba 2021


“Naomba Yeye Atutumie Sisi,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Nov. 2022.

Kikao cha Jumamosi Jioni

Naomba Yeye Atutumie Sisi

Dondoo

Picha
Lundo la nguo

Kanisa la Yesu Kristo lina agizo takatifu la kuwatunza maskini. Ni mojawapo ya nguzo za kazi ya wokovu na kuinuliwa. …

Kanisa hujibu agizo hili kwa njia nyingi tofauti, ikijumuisha:

  • Uhudumiaji tunaofanya kupitia Muungano wa Usaidizi, akidi za ukuhani na madarasa;

  • Kufunga na kutumia matoleo ya mfungo;

  • Mashamba ya ustawi na vyakula vya kopo;

  • Vituo vya makaribisho kwa wahamiaji;

  • Kuwafikia wale walio gerezani;

  • Juhudi za msaada wa kibinadamu za Kanisa;

  • na programu ya JustServe app, ambayo inaoanisha wenye kujitolea na fursa za kutumikia.

… Wakati miradi zaidi ya 1500 ya UVIKO-19 ilikuwa hakika ndio fokasi ya msaada wa Kanisa katika miezi 18, Kanisa pia lilijibu majanga ya asili 933 na matatizo ya wakimbizi katika nchi 108. …

Akizungumzia juhudi za msaada wa kibinadamu wa Kanisa, Mzee Jeffrey R. Holland wakati mmoja alisema: “Maombi hujibiwa … mara nyingi … na Mungu akiwatumia watu wengine. Hivyo, naomba kwamba atatutumia” [“Neonatal Resuscitation with Elder Holland” (video), The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints, Nov. 10, 2011, youtube.com]. …

Akina kaka na akina dada, kupitia huduma yenu, michango yenu, muda wenu na upendo wenu, mmekuwa jibu la maombi mengi sana. Na bado kuna mengi sana ya kufanya. Kama waumini waliobatizwa wa Kanisa, tuko chini ya agano la kuwatunza wale walio na uhitaji. Juhudi zetu za kibinafsi si lazima zihitaji pesa au maeneo ya mbali; zinahitaji mwongozo wa Roho Mtakatifu na moyo wa hiari kumwambia Bwana, “Mimi hapa; nitumie” [Isaya 6:8].

Chapisha