Mkutano Mkuu
Naomba Yeye Atutumie Sisi
Mkutano Mkuu wa Oktoba 2021


10:36

Naomba Yeye Atutumie Sisi

Juhudi ndogo kwa pamoja zinakuwa na nguvu kubwa, zikipanua vitu vingi vidogo tunavyofanya kama wanafunzi wa Yesu Kristo.

Biskuti hii iliyotengenezwa kwa kinyunya cha filo na jungu za pistachio ni ya shukrani. Ilitengenezewa na familia ya Kadado ambayo, kwa miongo, walimiliki tanuri mikate tatu huko Damascus, Syria. Vita ilipotokea, vizuizi vilisitisha vyakula na bidhaa kufika sehemu yao ya mji. Akina Kadado walianza kufa njaa. Katika kilele cha hali hii ya kukatisha tamaa, Latter-day Saints Charities na baadhi ya wafanyakazi wa Rahma Worldwide jasiri walianza kutoa chakula kilichopikwa kila siku pamoja na maziwa kwa ajili watoto wadogo. Baada muda mgumu, familia hii ilianza maisha yao—pamoja na tanuri yao ya mikate—mara ingine tena katika nchi mpya.

Karibuni, boksi la biskuti lilifika ofisini za Kanisa likiwa na ujumbe ufuatao: “Kwa zaidi ya miezi miwili, tulipata chakula kutoka katika jiko la Rahma–Latter-day Saints [Charities]. Bila hivyo tungepatwa na njaa mpaka kifo. Tafadhali pokeeni sampli hii … kutoka katika duka langu dogo kama ishara ndogo ya shukrani. Ninamuomba Mwenyezi Mungu awabariki … katika kila kitu mnachofanya.”1

Biskuti ya shukrani na ukumbusho. Ni kwa ajili yenu. Kwa wale wote walioomba baada ya kuangalia hadithi hii katika taarifa za habari, kwa wale ambao walijitolea wakati haikuwa rahisi au wale walichangia kifedha kwenye mfuko wa msaada wa kibinadamu, wakiamini zitafanya wema fulani, asanteni.

Jukumu Takatifu la Kuwatunza Maskini

Kanisa la Yesu Kristo lina agizo takatifu la kuwatunza maskini.2 Ni mojawapo ya nguzo za kazi ya wokozi na kuinuliwa.3 Kile kilichokuwa kweli wakati wa siku za Alma hakika ni kweli kwetu: “Na hivyo, hata katika hali yao ya kufanikiwa, hawakumfukuza yeyote aliyekuwa uchi, au walio na njaa, au walio na kiu, au wale ambao walikuwa wagonjwa, au wale ambao hawakuwa wamelishwa; na hawakuweka mioyo yao katika utajiri; kwa hivyo walikuwa wakarimu kwa wote, wote wazee kwa vijana, wote watumwa na walio huru, wote wanaume kwa wanawake, washiriki wa kanisa na wale wasio washiriki wa kanisa, bila kubagua wale wote walio na shida.”4

Kanisa hujibu agizo hili kwa njia nyingi tofauti, ikijumuisha:

  • Uhudumiaji tunaofanya kupitia Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama, akidi za ukuhani, na madarasa.

  • Kufunga na kutumia matoleo ya mfungo.

  • Mashamba na viwanda vya kutia vyakula makoponi.

  • Vituo vya makaribisho kwa wahamiaji.

  • Mipango ya kufikia wale walio gerezani.

  • Juhudi za msaada wa kibinadamu za Kanisa.

  • Na programu ya JustServe app, ambayo inaoanisha wenye kujitolea na nafasi za kutumikia.

Hizi zote ni njia, zilizopangwa kupitia ukuhani, ambapo juhudi ndogo kwa pamoja zinakuwa na nguvu kubwa, zikipanua vitu vingi vidogo tunavyofanya kama wanafunzi wa Yesu Kristo.

Manabii Wana Usimamizi kwa ajili ya Dunia Yote

Manabii wana agizo kwa ajili ya dunia yote, si tu kwa waumini wa Kanisa. Ninaweza kuripoti kutokana na uzoefu wangu mwenyewe jinsi Urais wa Kwanza kibinafsi na kwa kujitolea wanachukulia agizo hilo. Jinsi mahitaji yanavyozidi, Urais wa Kwanza wametupa agizo la kuzidisha juhudi zetu za msaada wa kibinadamu katika njia kubwa sana. Wanapendezwa na mwelekeo mkubwa na utondoti ulio mdogo sana.

Hivi karibuni, tuliwaletea wao mojawapo wa magauni ulinzi ya kitibabu ambayo BeehiveClothing walishona kwa ajili ya hospital kwa matumizi wakati wa janga. Kama daktari tibabu, Rais Russell M. Nelson alipendezwa sana. Hakutaka tu kuona. Alitaka kujaribu kuvalia—kukagua vifungo na urefu na jinsi linafungwa kwa nyuma. Alituambia sisi baadaye, kwa mhemko katika sauti yake, “Mnakutana na watu katika kazi zenu, washukuru kwa ajili kufunga kwao, matoleo yao, na uhudumiaji wao katika jina la Bwana.

Ripoti ya Huduma za Kibinadamu

Chini ya maelekezo ya Rais Nelson, mimi ninaripoti kwenu kuhusu jinsi Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho wanavyofanya wakati wa vimbunga, matetemeko ya ardhi, wakimbizi—hata pia janga—shukrani kwa ukarimu wa Watakatifu wa Siku za Mwisho na marafiki wengi. Hali miradi zaidi ya 1500 ya UVIKO-19 ilikuwa hakika ndio fokasi ya msaada wa Kanisa katika miezi 18, Kanisa pia lilijibu majanga asili 933 na matatizo ya wakimbizi katika nchi 108. Lakini takwimu hazisemi hadithi yote. Acha nishiriki mifano minne kwa kifupi ili kuonyesha kionjo kidogo sana cha kile kinachofanyika.

Msaada wa UVIKO wa Africa Kusini

Dieke Mphuti wa miaka kumi na sita wa Welkom, Afrika kusini, aliwapoteza wazazi wake miaka mingi iliyopita, akiachwa kuwatunza ndugu zake watatu yeye mwenyewe. Daima imekuwa vigumu kwake kupata chakula cha kutosha, lakini upungufu wa bidhaa wakati wa UVIKO na karantini ilifanya iwe vigumu kabisa. Kila mara walikuwa na njaa, wakitegemea tu ukarimu wa majirani.

Dieke Mphuti

Siku moja angavu katika Agosti 2020, Dieke alishangazwa kwa kugongwa kwa mlango wao. Aliufungua na kuwaona wageni wawili—mmoja mwakilishi wa Kanisa kutoka ofisi ya eneo katika Johannesburg na mwingine kutoka kwa Idara ya Ustawi wa Jamii ya Afrika Kusini.

Taasisi hizi mbili ziliungana kuleta chakula kwenye familia zilizoathirika. Msaada ulimshangaza sana Dieke alipotazama rundo la unga wa mahindi na vyakula vingine vya kawaida, vilivyonunuliwa na mifuko ya huduma ya kibinadamu ya Kanisa. Hivi vingesaidia kukidhi familia yao kwa wiki kadhaa mpaka msaada wa serikali ungeanza kufika na kumsaidia.

Hadithi ya Dieke ni mojawapo ya maelfu ya uzoefu unatokea kote ulimwenguni wakati wa janga la UVIKO shukrani kwa michango yenu ya kujitolea.

Msaada kwa Waafghani huko Ramstein

Wote tumeona picha nyingi katika taarifa za habari, maelfu ya wahamiaji waliabiri ndege kutoka Afghanistan. Wengi waliwasili katika vituo vya ndege la jeshi la angani au maeneo ya muda katika Qatar, Marekani, Ujerumani, na Uhispania kabla ya kuendelea mwisho wa safari yao. Mahitaji yao yalikuwa ya dharura, na Kanisa lilitoa bidhaa na watu wa kujitolea. Katika Kituo cha Ndege cha Ramstein katika Ujerumani, Kanisa lilitoa msaada mkubwa wa daipa, chakula cha watoto wachanga, chakula, na viatu.

Michango ya kibinadamu kwa wakimbizi
Wanawake wakishona kwa ajili ya wakimbizi Waafghani

Baadhi ya akina dada wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama waligundua kwamba wanawake wengi wa Kiafghani walikuwa wanatumia mashati ya waume wao kujifunika vichwa vyao kwa sababu nguo za tamaduni za kufunika vichwa zilikuwa zimepotea katika fujo za uwanja wa ndege wa Kabul. Katika kitendo cha urafiki kinachovuka mipaka ya kidini au tamaduni, akina dada wa Kata ya Kwanza ya Ramstein walishona nguo ya tamaduni ya kiislamu kwa ajili ya wanawake Waafghani. Dada Bethani Halls alisema, “Tulisikia kwamba wanawake walikuwa wanahitaji nguo za sala, na sisi tunashona ili kwamba wao waweze kufurahia wakati wa sala,”5

Msaada wa Tetemeko la Haiti

Huu mfano mwingine unoanyesha si lazima uwe tajiri au mzee kuwa chombo cha wema. Marie “Djadjou” Jacques wa miaka kumi na nane kutoka Tawi la Cavaillon katika Haiti. Wakati tetemeko angamizi lilipotokea karibu na mji wake katika Agosti, nyumba ya familia yao ilikuwa mojawapo ya maelfu ya majengo yaliyobomoka. Ni vigumu kabisa kufikiria dhiki ya kupoteza nyumba yako. Lakini badala ya kukubali dhiki hiyo, Djadjou—ajabu sana—aligeukia nje.

Marie Jacques
Tetemeko la Haiti

Associated Press

Alimwona jirani mkongwe akisumbuka na akaanza kumtunza. Aliwasaidia wengine kufagia vifusi. Licha kuchoka, alijiunga na waumini wengine wa Kanisa kugawa chakula na vifaa vya afya kwa wengine. Hadithi ya Djadjou ni mojawapo tu ya mifano ya nguvu ya huduma iliyofanywa na vijana na vijana wakubwa jinsi walivyojitahidi kufuata mfano wa Yesu Kristo.

Msaada wa Mafuriko Ujerumani

Wiki chache kabla ya tetemeko, kundi lingine la vijana wakubwa walikuwa na huduma kama hiyo upande mwingine wa Atlantic. Mafuriko ambayo yalisomba kote katika Ulaya magharibi mwezi Julai yalikuwa makali sana katika miongo.

Mafuriko Ujerumani

Wakati hatimaye maji yalipopungua, mwenye duka mmoja katika wilaya iliyo karibu na mto katika Ahrweiler, Ujerumani, alitathimini uharibifu na alizidiwa kabisa. Huyu mwanamume mnyenyekevu, Mkatoliki mcha Mungu, aliomba kimya kimya kwamba Mungu angeweza kumtuma mtu amsaidie. Asubuhi iliyofuata, Rais Dan Hammon wa Misheni ya Germany Frankfurt aliwasili mtaani na kikosi cha wamisionari kilichovalia vesti ya njano za Mikono Saidizi. Maji yalikuwa yamefika kimo cha futi 10 (Mita 3) ukutani, yaliacha tope la kina kikubwa. Watu wa kujitolea waliondoa tope, wakaondoa zulia na kuta za ubao wa vibanzi, na kuweka kila kitu mtaani ili viondolewe. Mwenye duka aliye na furaha sana alifanya pamoja nao kwa masaa, alishangaa kwamba Bwana alituma kundi la watumishi Wake kujibu sala yake—katika saa 24!6

“Basi, Naomba Yeye Atutumie Sisi”

Akizungumzia juhudi za msaada wa kibinadamu wa Kanisa, Mzee Jeffrey R. Holland wakati mmoja alisema: “Maombi hujibiwa … wakati wote … na Mungu akiwatumia watu wengine. Basi, Naomba Yeye Atutumie Sisi. Ninaomba kwamba tutakuwa jibu la maombi ya watu.”7

Akina kaka na akina dada, kupitia huduma yenu, michango yenu, muda wenu, na upendo wenu, mmekuwa jibu la maombi mengi sana. Na bado kuna mengi sana ya kufanya. Kama waumini waliobatizwa wa Kanisa, tuko chini ya agano la kuwatunza wale walio na uhitaji. Juhudi zetu binafsi hazihitaji fedha au maeneo ya mbali:8 zinahitaji mwongozo wa Roho Mtakatifu na moyo ulio tayari kusema kwa Bwana: “Mimi hapa, nitume mimi.”9

Mwaka wa Bwana Uliokubaliwa

Luka 4 imeandikwa kwamba Yesu alikuja Nazareti, ambapo alikuwa amelelewa, na akisima katika sinagogi kusoma. Hii ilikuwa karibu na mwanzo wa huduma Yake duniani, na Yeye alinukuu kifungu hicho kutoka katika kitabu cha Isaya:

“Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa,

Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.”…

“… Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.”10

Ninashuhudia kwamba maandiko yanatimia katika wakati wetu vile vile. Ninashuhudia kwamba Yesu Kristo alikuja kuiponya mioyo iliyovunjika. Injili Yake ni ya kuponya vipofu. Kanisa Lake ni la kutangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na wanafunzi Wake kote ulimwenguni wanajitahidi, kuwaacha huru waliosetwa.

Acha nihitimishe kwa kurudia swali Yesu alilomuuliza Mtume Wake Simoni Petro: “Wanipenda?”11 Kiini cha injili kiko katika jinsi tunajibu swali hilo kwetu wenyewe na “lisha kondoo [Zake]”12 Kwa heshima kubwa na upendo kwa ajili ya Yesu Kristo Bwana wetu, nimwalika kila mmoja wetu kuwa sehemu ya huduma Yake kuu, na naomba Yeye atutumie sisi. Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.