Mkutano Mkuu
Mali Nyingi
Mkutano Mkuu wa Oktoba 2021


Mali Nyingi

Kila mmoja wetu anapaswa kuja kwa Kristo tukiwa na utayari usioyumba kwenye injili Yake.

Maandiko yanazungumza kuhusu mtawala kijana tajiri, ambaye alimkimbilia Yesu, akapiga magoti miguuni Pake, na, kwa uaminifu wa dhati, alimwuliza Bwana, “Nifanye nini ili niweze kurithi uzima wa milele?” Baada ya kuchambua orodha ndefu ya amri mtu huyu alizozitii kwa uaminifu, Yesu alimwambia mtu huyu kuuza mali zake, mapato awape masikini, achukue msalaba wake, na amfuate Yeye. Ujasiri wa agizo hili ulisababisha mtawala kijana—licha ya kandambili zake za gharama—kupata ubaridi miguuni, na aliondoka akihuzunika kwa sababu, maandiko yanasema, “Alikuwa na mali nyingi.”1

Kwa kawaida, hii ni hadithi muhimu ya onyo kuhusu matumizi ya utajiri na mahitaji ya masikini. Lakini mwishowe ni hadithi kuhusu moyo mkunjufu, moyo kamili wa kujitoa kikamilifu kwenye majukumu matakatifu. Kwa kuwa na, au kutokuwa na utajiri, kila mmoja wetu anapaswa kuja kwa Kristo tukiwa na utayari uleule usioyumba kwenye injili Yake ambao ulitegemewa kwa kijana huyu. Katika lahaja ya vijana wa kileo, tunatakiwa kujitangaza kuwa “wote tumo.”2

Katika tabia yake mashuhuri ya nadhari, C.S. Lewis anamfikiria Bwana akisema kwetu kitu fulani kama hiki: “Sitaki … muda wako … [au] pesa zako … [au] kazi yako, [kama zaidi] ninavyokutaka [tu] wewe. [Mti huu unaupogoa.] Sitaki kulikata tawi hapa na tawi pale, Ninataka … mti [wote] ukatwe. [Na jino hilo.] Sitaki [kulitoboa], au kulifanya liwe zuri, au [kulijaza]. [Nataka] kuling’oa. [Kwa kweli, Ninakutaka unipe] utu wako wote wa tabia ya asili. … [Na] Nitakupa utu mpya kama mbadala. Kwa kweli, Nitajitoa kwako: matakwa Yangu … yatakuwa [matakwa yako].’”3

Wale wanaozungumza nasi katika mkutano huu mkuu wote watakuwa wakisema, katika njia moja au nyingine, kile Kristo alichokisema kwa mtu huyu tajiri: “Njoo kwa Mwokozi wako. Njoo kikamilifu na kwa moyo wote. Jitwike msalaba wako bila kujali ni mzito kiasi gani na umfuate Yeye.”4 Watasema haya wakijua kwamba katika ufalme wa Mungu, hapawezi kuwa na viwango visivyo kamili, hakuna kuanza na kusimama, hakuna kurudi nyuma. Kwa wale walioomba ruhusa ya kumzika mzazi aliyekufa au kusema kwaheri kwa wanafamilia wengine, jibu la Yesu lilikuwa la kuhitaji na la moja kwa moja. “Waachie hilo wengine,” Yeye alisema. “Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu.”5 Wakati tunapoombwa kufanya mambo magumu, hata yale yaliyo kinyume na matamanio ya mioyo yetu, kumbukeni kwamba uaminifu tunaoahidi kwenye kusudi la Kristo unapaswa kuwa azimio la juu kabisa la maisha yetu. Ingawa Isaya anatuhakikishia tena kwamba linapatikana “bila pesa na bila thamani,”6—la ndivyo ilivyo—lazima tuwe tumejiandaa, tukitumia mstari wa T.S. Elliot, iwe linagharimu “kila kitu tulichonacho.”7

Ndiyo, sote tuna baadhi ya desturi au hitilafu au historia binafsi ambazo zinaweza kutuzuia kuzama kikamilifu kiroho katika kazi hii. Lakini Mungu ni Baba yetu na mzuri kwa kipekee kwenye kusamehe na kusahau dhambi tulizozitelekeza, pengine kwa sababu tunampa mazoea mengi katika kufanya hivyo. Kwa vyovyote vile, kuna msaada wa kiungu kwa kila mmoja wetu saa yoyote tunapohisi kufanya mabadiliko katika tabia zetu. Mungu alimpa Sauli “moyo mwingine.”8 Ezekieli aliwaita waisraeli wote wa kale kuyatupa maisha yao ya zamani na “kujifanyia … moyo mpya na roho mpya.”9 Alma aliomba “badiliko kuu”10 ambalo lingesababisha nafsi kuvimba, na Yesu Mwenyewe alifundisha kwamba “mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.”11 Hakika uwezekano wa badiliko na kuishi kwenye kiwango kilichoinuliwa zaidi umekuwa siku zote moja ya vipawa vya Mungu kwa wale wanaokitafuta.

Marafiki, katika wakati wetu wa sasa tunapata aina zote za migawanyiko na utengano, makundi na vikundi, makabila ya kileo na utambulisho wa kisiasa, pamoja na uadui mkubwa unaoendelea. Je hatupaswi kujiuliza kama “maisha ya juu na matakatifu”12 kwa kutumia kirai cha Rais Nelson, yanaweza kuwa kitu fulani ambacho tungeweza kukitafuta? Wakati tunafanya hivyo, tutafanya vyema kukumbuka wakati ule mzuri katika kitabu cha Mormoni ambapo watu wale waliuliza na kujibu swali hilo kwa uthabiti:

“Na ikawa kwamba hakukuwa na ubishi miongoni mwa watu wote, katika ile nchi yote … kwa sababu ya mapenzi ya Mungu ambayo yaliishi katika mioyo ya watu.

“Na hakukuwa na wivu, wala ubishi, … wala aina yoyote ya ukahaba; na kwa kweli hakujakuwa na watu ambao wangekuwa na furaha zaidi miongoni mwa watu wote ambao waliumbwa na mkono wa Mungu.

“Hakukuwa na wanyang’anyi, wala wauaji, wala hakukuwa na Walamani, wala aina yoyote ya vikundi; lakini walikuwa kitu kimoja, watoto wa Kristo, na warithi wa ufalme wa Mungu.

Na jinsi gani walibarikiwa!13

Ni nini kilikuwa msingi wa maendeleo haya katika kuishi maisha ya kuridhika, ya furaha? Kimekaa pale katika maandiko katika sentensi moja: “Mapenzi ya Mungu … yaliishi katika mioyo ya watu.”14 Wakati mapenzi ya Mungu yanapoweka toni kwa ajili ya maisha yetu, kwa ajili ya mahusiano yetu kwa kila mmoja wetu na hatimaye hisia zetu kwa wanadamu wote, kisha tofauti za zamani, utambulisho wenye ukomo, na migawanyiko ya kinafiki inaanza kutoweka, na amani inaongezeka. Hicho ndicho hasa kilichotokea katika mfano wetu wa kitabu cha Mormoni. Hapakuwepo tena Walamani au Wayakobo au Wajoseph au Wazoramu. Hapakuwa na “-wa fulani” kabisa. Watu walikuwa wamejichukulia utambulisho mmoja mpya upitao uwezo wa kibinadamu. Wote ilikuwa, kinasema, wajulikane kama “watoto wa Kristo.”15

Bila shaka, tunazungumza hapa juu ya amri kuu ya kwanza iliyotolewa kwa familia ya mwanadamu—kumpenda Mungu kwa moyo wote, bila shaka au vigezo, ambayo ni, kwa moyo wetu wote, nguvu, akili na uwezo.16 Upendo huu wa Mungu ni amri kuu ya kwanza ulimwenguni. Lakini ukweli mkuu wa kwanza ulimwenguni ni kwamba Mungu anatupenda sawa sawa kwa njia hiyo—kwa moyo Wake wote, bila shaka au vigezo, kwa moyo Wake wote, nguvu, akili na uwezo. Na wakati nguvu hizo kuu za moyo Wake na mioyo yetu zinapokutana bila kizuizi, kuna uhakika wa mlipuko wa nguvu ya kiroho, ya uadilifu. Kisha, kama Teilhard de Chardin alivyoandika, “kwa [mara] ya pili katika historia ya Ulimwengu, binadamu atakuwa amegundua moto.”17

Ni wakati huo, na kwa kweli ni wakati huo pekee ambapo tunaweza kwa weledi kutii amri kuu ya pili katika njia ambazo sio za kinafiki au zisizo na maana. Kama tunampenda Mungu vya kutosha kujaribu kuwa waaminifu kikamilifu Kwake, Atatupa uwezo, nafasi, nia na njia ya kuwapenda majirani zetu na sisi wenyewe. Pengine hapo ndipo tutaweza kusema tena, “Hakujakuwa watu wenye furaha zaidi miongoni mwa watu wote ambao wameumbwa na mkono wa Mungu.”18

Akina kaka na akina dada, ninaomba tuweze kuendelea pale ambapo kijana yule tajiri alishindwa, kwamba tutachukua msalaba wa Kristo, licha ya mahitaji unayoweza kuwa nayo, bila ya kujali mambo yaliyopo na bila kujali gharama. ninatoa ushahidi kwamba tunapoahidi kumfuata Yeye, njia, kwa namna moja au nyingine, itapita kwenye taji la miiba na msalaba wa kuogofya wa Kirumi. Haidhuru jinsi gani kijana wetu mtawala alikuwa tajiri, hakuwa tajiri vya kutosha kununua uhuru wake nje ya makutano ya kaburi na msalaba, na hata sisi hatuwezi. Kwani baraka za kupokea utajiri wote—baraka ya uzima wa milele—ni kubwa ikilinganishwa na kuchukuwa msalaba wetu na kumfuata Kuhani Mkuu wa Maungamo yetu, Nyota yetu ya asubuhi, Wakili, na Mfalme. Ninashuhudia na Amaleki wa kale ambaye hakuwa maarufu kwamba kila mmoja wetu tunapaswa, “[kutoa ] nafsi zetu zote kama sadaka Kwake.”19 Tukiwa na uaminifu kama huo wa dhati, imara tunaimba:

Sifa kwa mlima; ambapo juu yake nimesimama:

Mlima wa upendo wako ukomboao. …

Huu hapa moyo wangu, Ee uchukuwe na uutie muhuri,

Utie muhuri kwa ajili ya enzi zako juu.20

Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.

Chapisha