Mkutano Mkuu
Inua Mwangaza Wako
Mkutano Mkuu wa Oktoba 2021


Inua Mwangaza Wako

Mwaliko wangu leo ni rahisi: shiriki injili. Kuwa wewe na inua mwangaza wako.

Nikiwa kwenye ndege kuelekea Peru miaka michache iliyopita, pembeni yangu alikaa aliyejiita mtu asiye mwamini Mungu. Aliniuliza kwa nini ninamwamini Mungu. Katika mazungumzo mazuri yaliyofuata baada ya hapo, nilimwambia kwamba ninamwamini Mungu kwa sababu Joseph Smith Alimwona—na pia niliongezea kwamba elimu yangu kuhusu Mungu pia ilitokana na uzoefu wangu binafisi, na halisi wa kiroho. Nilimshirikisha imani yangu kuwa “mambo yote yanaashiria kuwa kuna Mungu”1 na kumuuliza ni kwa jinsi gani aliamini dunia—oasis hii ya maisha katika utupu wa nafasi—iliweza kuwepo. Alijibu kwamba, katika maneno yake, “bahati mbaya” huenda ilitokea kipindi kirefu cha muda. Nilipo mwelezea ni kwa kiasi gani ingekuwa vigumu kwa “bahati mbaya” kuzalisha mpangilio kama huu, alinyamaza kwa muda na kusema, “umeniweza.” Nilimuuliza kama angeweza kusoma Kitabu cha Mormoni. Alisema angeweza, hivyo nilimtumia nakala.

Miaka kadhaa baadaye nilipata rafiki mpya nilipokuwa uwanja wa ndege wa Lagos, Nigeria. Tuliweza kufahamiana alipoangalia paspoti yangu. Nilimuuliza kuhusu imani ya dini yake, na alielezea imani kubwa kwa Mungu. Nilishiriki furaha na msisimko wa injili ya urejesho ya Yesu Kristo na nikamuuliza kama angependa kujifunza zaidi kutoka kwa wamisionari. Alisema ndio, alifundishwa na alibatizwa. Mwaka mmoja au miwili, wakati natembea kwenye uwanja wa ndege huko Liberia, nilisikia sauti ikiita jina langu. Niligeuka, na yule kijana mdogo alinikaribia akiwa na tabasamu kubwa. Kwa furaha tulikumbatiana, na akanijulisha kuwa alikuwa ni muumini hai Kanisani akifanya kazi na wamisionari kumfundisha rafiki yake wa kike.

Sijui kama rafiki yangu asiyemwamini Mungu aliwahi kusoma kitabu cha Mormoni au kujiunga na Kanisa. Rafiki yangu wa pili alijiunga na Kanisa. Kwa wote, wajibu wangu2—fursa yangu—ilikuwa sawa: kubeba mwangaza wa injili—kupenda, kushiriki, na kualika katika hali ya asili, na ya kawaida.3

Akina kaka na dada, nina uzoefu wa baraka za kushiriki injili, na ni kubwa mno. Hizi ni baadhi ya hizo:

Kushiriki Injili Huleta Shangwe na Tumaini

Mimi na wewe, tunajua kwamba tuliishi kama watoto wa Baba yetu wa Mbinguni kabla ya kuja katika dunia hii4 na kwamba dunia iliumbwa kwa lengo la kumpa fursa kila mtu kupata mwili, kupata uzoefu, kujifunza, na kukua ili aweze kupata uzima wa milele—ambao ni maisha ya Mungu.5 Baba wa Mbinguni alijua kuwa tungeteseka na kutenda dhambi duniani, hivyo Alimtuma Mwanaye, ambaaye kwa “maisha yake yasiyo na kifani”6 na sadaka ya milele7 inafanya uwezekano kwetu kusamehewa, kuponywa, na kufanya yote.8

Kujua kweli hizi hubadili maisha! Mtu anapojifunza dhumuni tukufu la maisha, anaelewa kuwa Kristo husamehe na huwasaidia wale wanaomfuata Yeye, na kisha anachagua kumfuata Kristo katika maji ya ubatizo, maisha hubadilika—hata kama hali za kimaisha hazijabadilika.

Dada mwenye furaha niliyekutana naye Onitisha, Nigeria, aliniambia kuwa kuanzia muda alipojifunza injili na kubatizwa, (na natumia maneno yake ), “Kila kitu nikizuri kwangu. Nina furaha. Niko mbinguni.”9 Kushiriki injili huleta furaha na tumaini katika mioyo ya wote anayetoa na kupokea. Hakika, “shangwe yako itakuwa kiasi gani”10 unaposhiriki injili! Kushiriki injili ni furaha juu ya furaha, tumaini juu ya tumaini.11

Kushiriki Injili Huleta Nguvu za Mungu Katika Maisha Yetu

Tulipobatizwa, kila mmoja wetu aliingia katika agano12 endelevu na Mungu “Kumtumikia Yeye na kushika amri Zake,”13 ambalo hujumuisha “ kusimama kama shahidi [Wake] nyakati zote na katika mambo yote na katika sehemu zote.”14 Kadiri “tunavyokaa” ndani Yake kwa kutii agano hili, nguvu za kukuza, kusaidia na kusafisha za uungu hutiririka katika maisha yetu kutoka kwa Kristo, kama tawi lipokeavyo lishe kutoka kwenye mti.15

Kushiriki Injili Hutulinda Dhidi ya Majaribu

Bwana alitangaza:

“Inueni juu nuru yenu ili ing’are ulimwenguni. Tazama Mimi ni mwangaza ambao mtainua—ambao mmeniona mimi nikifanya. …

“… Nimeamuru kwamba … yawapasa kuja kwangu, ili muweze kuhisi na kuona; vivyo hivyo mtafanya kwa ulimwengu; na yeyote anayeasi hii amri anakubali mwenyewe kuongozwa majaribuni.”16

Kutokuchagua kubeba mwangaza wa injili hutupeleka katika vivuli, ambako tunahusika zaidi na majaribu. Lamuhimu, kinyume chake ni kweli: kuchagua kubeba mwangaza wa injili hutuleta kikamilifu kwenye ule mwanga na kinga inayoutoa dhidi ya majaribu. Ni baraka ya kushangazz kiasi gani katika ulimwengu wa leo!

Kushiriki Injili Huleta Uponyaji

Dada Tiffany Myloan alikubali mwaliko wa kuwasaidia wamisionari licha ya changamoto nzito binafisi, ikijumuisha maswali binafisi kuhusu imani yake. Hivi karibuni aliniambia kwamba kuwasaidia wamisionari kumejenga upya imani yake na fikra za kuwa bora. Katika maneno yake, “kazi ya Umisionari inaponya.”17

Shangwe. Tumaini. Nguvu saidizi toka kwa Mungu. Kulindwa dhidi ya majaribu. Uponyaji Yote haya—na zaidi (ikijumuisha msamaha wa dhambi)15—hutonatona juu yetu kutoka mbinguni kadiri tunavyoshiriki injili.

Sasa, Tukigeukia Fursa Yetu Kuu

Akina kaka na dada, kuna wengi kati ya … vyama, [makundi,] na madhehebu … ambao wametengwa na ukweli sababu hawajui wapi pa kuupata.”19 Hitaji la kuinua mwangaza wa injili ya Kristo iliyorejeshwa ni kubwa katika historia ya binadamu kuliko hapo awali. Na ukweli unapatikana zaidi kuliko hapo awali.

Jimmy Ton, aliyekulia kwenye Ubudha, alifurahishwa na familia iliyoshiriki maisha yao kwenye You Tube. Wakati alipojua kwamba walikuwa waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, yeye mwenyewe alijifunza injili mtandaoni, alisoma Kitabu cha Mormoni akitumia programu, na alibatizwa baada ya kukutana na wamisionari chuoni.20 Mzee Ton kwa sasa ni mmisionari.

Yeye na wamisionari wenzake ulimwenguni kote ni jeshi la Bwana—Nikimnukuu nabii wetu.21 Wamisionari hawa huenda kinyume na kawaida ya ulimwengu: wakati utafiti unaarifu kwamba kizazi kinachochipukia kinageuka mbali kutoka kwa Mungu,22 mashujaa wetu23 wazee na akina dada wanageuza watu kuelekea kwa Mungu. Na kuongezeka kwa idadi ya waumini wa Kanisa wakiungana na wamisionari katika kushiriki injili, wakisaidia marafiki zaidi na zaidi kuja kwa Kristo na Kanisa Lake.

Waumini wetu wa Siku za Mwisho huko Liberia walisaidia marafiki 507 kuingia kwenye maji ya ubatizo kwa miezi 10 wakati hapakuwepo na wamisionari wa kuhudumu kwenye nchi yao. Wakati mmoja wa marais wetu wazuri wa vigingi huko Liberia aliposikia kwamba wamisionari wanaweza kurudi, alisema: “Oh vizuri, sasa wanaweza kutusaidia na kazi yetu.”

Yuko sahihi: kusanya Israeli—kazi iliyo kuu hapa duniani ni wajibu24wetu kimaagano. Na huu ni muda wetu! Mwaliko wangu leo ni rahisi: shiriki injili. Kuwa wewe na inua mwangaza wako. Omba msaada wa mbingu na fuata msukumo wa kiroho. Shiriki maisha yako kikawaida na kiuhalisia; mwalike mtu mwingine aje na aone, aje na kusaidia, na aje na awe mmoja wapo.25 Na kisha shangilia wakati wewe na wale uwapendao wanapata baraka zilizoahidiwa.

Najua kwamba katika Kristo habari hizi njema zinahubiriwa kwa wanyonge; katika Kristo wale wenye mioyo iliyovunjika hufarijiwa; katika Kristo ni uhuru umetangazwa kwa wafungwa, na katika Kristo, pekee katika Kristo wale wanao omboleza wanapewa tumaini.26 Hivyo, kuwepo kwa hitaji kubwa kufanya mambo haya kujulikana!27

Nashuhudia kwamba Yesu Kristo ni mwandishi na mmaliziaji wa imani yetu.28 Atamaliza, Atakamilisha, zoezi letu la imani—hata kama si kamilifu—katika kuinua mwangaza wa injili. Atatenda miujiza katika maisha yetu na katika maisha ya wote Awakusanyao, kwani ni Mungu wa miujiza.29 Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.

Chapisha