Kutoa Utakatifu kwa Bwana
Dhabihu, kidogo inahusu “kuacha kitu” na ni zaidi kuhusu “kutoa kwa“ Bwana.
Mwaka jana, nikitumikia katika Urais wa Eneo la Asia Kaskazini, nilipokea simu kutoka kwa Rais Russell M. Nelson akinialika kutumikia kama Mshauri wa Pili katika Uaskofu Simamizi. Kwa heshima alimwalika mke wangu, Lori, kujiunga na mazungumzo. Baada ya mazungumzo kuisha, sisi tulikuwa katika hali ya kutoamini wakati mke wangu aliuliza, “Uaskofu Simamizi hufanya kazi gani? Baada ya muda wa tafakari, nilijibu, “Sijui hakika!”
Mwaka mmoja baadaye—baada ya hisia nzito za unyenyekevu na shukrani—Naweza kujibu swali la mke wangu kwa uelewa mkubwa. Miongoni mwa vitu vingine vingi, Uaskofu Simamizi husimamia kazi ya ustawi na huduma ya kibinadamu ya Kanisa. Kazi hii sasa ina upana ulimwenguni kote na hubariki watoto wengi wa Mungu kuliko hapo awali.
Kama Uaskofu Simamizi, tunasaidiwa na wafanyakazi wa ajabu wa Kanisa na wengine, ikijumuisha Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama, ambao unatumikia pamoja nasi katika Kamati Tendaji ya Kanisa ya Ustawi na Kujitegemea. Katika nafasi yetu kama washiriki wa kamati hiyo, Urais wa Kwanza umeniomba mimi—vile vile Dada Sharon Eubank, ambaye alinena nasi jioni ya jana—kushiriki nanyi taarifa mpya juu ya juhudi za huduma ya kibinadamu za karibuni. Wao pia hasa wameomba kwamba tutoe shukrani zao za dhati—kwa sababu, akina kaka na akina dada, ni ninyi ambao mmefanya hizo juhudi za huduma ya kibinadamu kuwezekana.
Kama tulivyoona kwa wasiwasi athari za mapema za kiuchumi za shida ya UVIKO-19 kote ulimwenguni, kwa urahisi tungetarajia kupunguka kwa michango ya kifedha ambayo Watakatifu wangeweza kutoa. Hata hivyo, waumini wetu wenyewe hawakusazwa na shida za janga. Fikiria hisia zetu wakati tunaona kinyume chake! Michango ya huduma ya kibinadamu katika mwaka 2020 ikawa ya juu sana kuliko wakati mwingine—na inaendelea vivyo hivyo mwaka huu. Kama matokeo ya ukarimu wenu, Kanisa limeweza kutimiza huduma yenye mapana tangu kuasisiwa kwa Hazina ya Huduma ya Kibinadamu, kukiwa na miradi ya msaada 1,500 ya UVIKO katika nchi zaidi ya 150. Michango hii, ambayo ninyi mmetoa kwa kujitolea sana kwa Bwana, imegeuzwa kuwa chakula cha kukidhi maisha, oxgini, vifaa vya utibabu, na chanjo kwa wale kivingine hawangepata.
Muhimu kama ilivyo mchango wa bidhaa uweza kuzidi sana kwa wakati na nguvu ambazo waumini wa Kanisa huchangia kwa shughuli za huduma ya kibinadamu. Hata vile janga lilivyotanda, majanga ya asili, vurugu za kiraia, na kuyumba-yumba kiuchumi kumekuwa kukiendelea bila kupunguka na kuendela kuwaondoa kutoka mnyumbani mwao. Umoja wa Mataifa sasa unaripoti kwamba kuna zaidi ya milioni 82 waliofurushwa ulimwenguni.1 Ongeza hawa kwa mamilioni wengine ambao wamechagua kukimbia kutoka kwa umaskini au ukandamizaji kwa minajili ya kutafuta maisha bora kwa wao wenyewe au watoto wao, na unaweza kupata picha ya ukubwa wa hali hii duniani.
Ninafurahia kuripoti kwamba shukrani kwa muda wa kujitolea na talanta za wengi sana, Kanisa huendesha vituo vya makaribisho kwa wakimbizi na wahamiaji katika maeneo mengi katika Marekani na Ulaya. Shukrani kwa michango yenu, tunatoa bidhaa, fedha, na wenye kujitolea kusaidia miradi kama hiyo inayoendeshwa na taasisi zingine kote duniani.
Acha nitoe shukrani za moyo wa dhati kwa Watakatifu wale ambao wamejitolea kuwalisha, kuwavisha, na kuwa marafiki wa hawa wakimbizi na kuwasaidia wao kujisimamia na kujitegemea.
Jana jioni, Dada Eubank alishiriki pamoja nanyi juhudi za ajabu za Watakatifu wachache kuhusu hili. Ninapotafakari juu juhudi hizi, mawazo yangu mara nyingi ugeukia kanuni ya dhabihu na muunganiko wa moja kwa moja kwa kanuni hii kwa amri mbili za kumpenda Mungu na kumpenda jirani yako.
Matumizi ya kisasa, neno dhabihu yamekuja kutoa dhana ya “kuacha” vitu kwa ajili ya Bwana na ufalme Wake. Hata hivyo, katika siku za kale, maana ya neno dhabihu lilihusishwa na vyanzo viwili vya Kilatini sacer, kumaanisha takatifu au utakatifu, na facere, kumaanisha “kufanya.”2 Kwa hiyo, dhabihu ya kale ilimaanisha hasa kufanya kitu au mtu kuwa mtakatifu.3 Kwa mtazamo kama huu, dhabihu ni mchakato wa kuwa mtakatifu na kuja kumjua Mungu, si tukio au kaida za kidini za “kuacha” vitu kwa ajili ya Bwana.
Bwana alisema,“Nataka [fadhili] wala si sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa.”4 Bwana hututaka sisi kuwa watakatifu,5 kujawa na fadhili,6 na kuja kumjua Yeye.7 Kama Mtume Paulo alivyofunza, “Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.”8 Hatimaye, Bwana hutaka mioyo yetu; Yeye anataka tuwe viumbe vipya katika Kristo.9 Kama Yeye alivyowaelekeza Wanefi, “Na mtatoa kwangu dhabihu ya moyo uliopondeka na roho iliyovunjika.”10
Dhabihu, kidogo inahusu “kuacha kitu” na ni zaidi kuhusu “kutoa kwa“ Bwana. Yamechongwa juu ya mlango wa kila mojawapo ya mahekalu yetu maneno, “Utakatifu kwa Bwana; Nyumba ya Bwana.” Tunaposhika maagano yetu kwa dhabihu, tunafanywa watakatifu kupitia neema ya Yesu Kristo, na katika madhabahu ya hekalu takatifu, kwa moyo uliopondeka na roho iliyovunjika, kuishi utakatifu wetu kwa Bwana. Mzee Neal A. Maxwell alifundisha: “Kusalimisha mapenzi [au moyo11] kweli ndiyo kitu pekee cha mtu binafsi tunachotakiwa kukiweka juu ya madhabahu ya Bwana. … Hata hivyo, wakati wewe na mimi hatimaye tunajitoa wenyewe, kwa kuachia mapenzi yetu binafsi kumezwa katika mapenzi ya Mungu, kisha kwa kweli tunatoa kitu Kwake!”12
Wakati dhabihu zetu kwa niaba ya wengine zinatazamwa kutoka kwa matazamo wa “kuacha,” tunaweza kuziona kama mzigo na kuvunjika moyo wakati dhabihu zetu zisipotambuliwa au kuzawadiwa. Hata hivyo, wakati zinatazamwa kutoka kwa mtazamo wa “kutoa kwake” Bwana, dhabihu zetu kwa niaba ya wengine huwa zawadi, na furaha ya kutoa kwa ukunjufu huwa zawadi yetu wenyewe. Kuwa huru na haja ya upendo, idhini, au shukrani kutoka kwa wengine, dhabihu zetu huwa safi na onyesho la kina la shukrani zetu na upendo wetu kwa Mwokozi na wanadamu wenzetu. Aina yoyote ya dhabibu binafsi yenye kiburi huondoa hisia za shukrani, ukarimu, kuridhika, na furaha.13
Kitu fulani hufanywa kitakatifu—iwe katika maisha yetu, mali yetu, muda wetu, au talanta zetu—si kiurahisi kwa kuacha bali kwa kukitoa14 kwa Bwana. Kazi ya huduma ya kibinadamu ya Kanisa ni zawadi kama hiyo. Ni zao la matoleo yaliyowekwa wakfu ya pamoja ya Watakatifu, onyesho la upendo wetu kwa Mungu na watoto Wake.15
Steve na Anita Canfield ni wawakilishi wa Watakatifu wa Siku za Mwisho kote ulimwenguni ambao wana uzoefu wao wenyewe wa baraka zenye kubadilisha kuacha kwa ajili ya Bwana. Kama wamisionari wa ustawi na kujitemea, akina Canfield waliombwa kutoa msaada kwenye kambi ya wakimbizi na vituo vya wahamiaji kote Ulaya. Katika maisha ya kazi yake, Dada Canfield alikuwa msanifu wa kiwango cha juu ulimwenguni, akiwa mkandarasi wa wateja matajiri kupamba nyumba zao. Ghafla akajipata ametupwa katika ulimwengu ambao ulikuwa tofauti alipotumikia miongoni mwa watu ambao walikuwa wamepoteza karibu kila kitu katika mali za ulimwenguni. Kwa maneno yao, alibalidishana “uwanda wa marumaru kwa sakafu ya udongo” na kwa kufanya hivyo alipata kiasi kikubwa cha kuridhika, wakati yeye na mume wake walianza kufanya urafiki—na punde kuwapenda na kuwakumbatia—wale ambao walihitaji utunzaji wao.
Akina Canfield walisema, “Hatukuhisi kama vile ‘tuliacha’ chochote ili kumtumikia Bwana. Hamu yetu alikuwa tu ‘kutoa’ muda wetu na nguvu zetu Kwake kuwabariki watoto Wake katika njia yoyote Yeye aliyoona anafaa kututumia. Tulipofanya pamoja na akina kaka na akina dada, mwonekano wa nje—tofuati zozote za uraia wetu au mali—ziliyeyuka kwetu, na tunaona tu mioyo ya mmoja kwa mwingine. Hakuna kiwango chochote cha ajiri au mali ambacho kinaweza kutoshana na vile uzoefu huu, wa kutumikia miongoni mwa watoto wanyonge wa Mungu kumetusitawisha.”
Hadithi ya akina Canfield na wengine wengi zimetusaidia kuelewa vyema maneno rahisi hali muhimu ya wimbo wa Msingi:
“Toa,” kijito kidogo kilisema,
Kilipokuwa kikitiririka toka kilimali;
“Mimi ni mdogo, lakini najua kokote niendako
Mashamba yaendelea kuwa kijani bado.”
Ndiyo, kila mmoja wetu ni mdogo, lakini pamoja tunapoharakisha kutoa kwa Mungu na wanadamu wenzetu, popote tuendapo maisha yanastawishwa na kubarikiwa
Kifungu cha tatu cha wimbo huu hakijulikani sana lakini huhitimisha kwa mwaliko wa upendo:
Toa, basi, kama Yesu atoavyo;
Kuna kitu sote tunachoweza kutoa.
Fanya kama vijito na maua kuchanua:
Kuishi kwa ajili ya Mungu na wengine.16
Akina kaka na akina dada wapendwa, tunapoishi kwa ajili ya Mungu na wengine kwa kutoa mali yetu, muda wetu, naam hata sisi wenyewe, tunauacha ulimwengu ukiwa kijani kidogo, tunawaacha watoto wa Mungu wakiwa na furaha kidogo, na, katika mchakato huu, tunakuwa watakatifu kidogo zaidi.
Na Bwana awabariki sana kwa dhabihu ambazo mnatoa Kwake kwa ukunjufu.
Ninashuhudia kwamba Mungu anaishi! “Mtu wa Utakatifu ndilo jina lake.”17 Yesu Kristo ni Mwanawe na mtoa wa zawadi zote nzuri.18 Na kwa kupitia neema Yake na kushika maagano yetu kwa dhabihu kufanywe kuwa takatifu na daima tutoe zaidi upendo na utakatifu kwa Bwana.19 Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.