Nyumba ya Mfululizo wa Utaratibu
“Mfululizo wa utaratibu” ni njia thabiti, rahisi, asili kwa ajili ya Bwana kutufundisha sisi, kama watoto Wake, kanuni muhimu.
Katika maisha yangu ya ajira na huduma yangu katika Kanisa, nimefanya hivi mara maelfu—kamwe sijafanya hivyo kukiwa na wanaume 15 wamekaa nyuma yangu. Ninahisi sala zao na zenu.
Akina kaka na kina dada, mimi ni mzawa wa Ufalme wa Tonga katika Pacific ya Kusini ila nilikulia Amerika ya Kaskazini. Mlipuko wa ugonjwa umewaweka mamia, labda maelfu ya vijana wamisionari wa Kitonga waliokuwa wakihudumu duniani kote kurudi katika nchi yao pendwa kwa sababu ya kufungwa kwa mipaka yake. Baadhi ya wazee Watonga wamekuwa katika misheni yao kwa miaka mitatu na akina dada kwa miaka miwili! Wanasubiri kwa subra na imani ambayo watu wetu hujulikana kwayo. Wakati huo, usishangazwe sana kama baadhi yao wanatumikia katika kata zenu na vigingi wanaonekana zaidi kama mimi—umri mkubwa na kijivu. Tunashukuru kwa ajili ya wamisionari popote pale kwa huduma yao ya kujitoa, hata ikiwa ni ndefu au fupi kuliko walivyotegemea kwa sababu ya janga kubwa.
Jumapili moja nilipokuwa shemasi, nilikuwa kwenye ukumbi na sinia ya maji nikipitisha sakramenti wakati mwanamke mmoja alipoingia kwenye jengo. Kwa uadilifu, nilimsogelea na kumpa sinia. Aliinama kichwa, akatabasamu, na alichukua kikombe cha maji. Alikuwa amechelewa sana kupokea mkate. Muda mfupi baada ya uzoefu huu, mwalimu wangu wa nyumbani, Ned Brimley, alinifundisha kwamba vipengele vingi na baraka za injili ya Yesu Kristo hutolewa kwetu katika mfululizo wa utaratibu.
Baadae juma hilo, Ned na mshirika wake walikuja nyumbani kwetu na somo la kukumbukwa. Ned alitukumbusha kwamba kulikuwepo na utaratibu ambao Mungu aliumba nchi. Bwana alichukua uangalifu mkubwa sana katika kumuelezea Musa utaratibu ambao Aliumba nchi. Kwanza, Alianza kwa kutenganisha mwanga kutoka katika giza, baadae maji kutoka nchi kavu. Aliongezea mti wa uzima na wanyama kabla ya kutambulisha sayari mpya aliyounda uumbaji Wake mkubwa: wanadamu kuanzia na Adamu na Hawa.
“Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. …
“Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana.” (Mwanzo 1:27, 31).
Bwana akapendezwa. Na Yeye alipumzika siku ya saba.
Mfululizo wa utaratibu ambao dunia iliumbwa hutupa kuona sio tu kile kilicho muhimu kwa Mungu bali kwa nini na kwa ajili ya nani Yeye aliumba dunia.
Ned Brimley alinyambulisha somo lake lililomhamasisha na tamko rahisi: “Vai, nyumba ya Mungu ni ya utaratibu. Anakutarajia wewe kuishi maisha yako kwa utaratibu. Katika mfululizo sahihi. Anakutaka wewe kutumikia misheni kabla ya kuoa.” Kwa jambo hili, viongozi wa Kanisa kwa sasa hufundisha kwamba “Bwana anatarajia kila mvulana mwenye uwezo kujiandaa kutumikia misheni. … Wasichana … wanaotamani kutumikia wanapaswa kujiandaa pia” (General Handbook: Serving in The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints, 24.0, ChurchofJesusChrist.org). Kaka Brimley aliendelea: “Mungu anataka wewe uoe kabla ya kupata watoto. Na Yeye anakutaka wewe kuendeleza talanta zako unapopata elimu.” Ikiwa utachagua kuishi maisha yako nje ya mfululizo, utakuta maisha yanakuwa magumu na yenye ghasia.
Kaka Brimley pia alitufundisha kuwa kupitia dhabihu yake ya upatanisho, Mwokozi anatusaidia kurudisha utaratibu kwenye maisha yetu yenye vurugu au nje ya mfumo kwa chaguzi zetu wenyewe dhaifu au za wengine.
Toka wakati huo na kuendelea, nimekuwa na mvuto kwenye “mfululizo wa utaratibu.” Nilijenga tabia ya kuangalia mfululizo wa miundo katika maisha na katika injili.
Mzee David A. Bednar alifundisha kanuni hii: “Tunaposoma, kujifunza, na kuishi injili ya Yesu Kristo, mfululizo mara nyingi unafunza. Fikiria, kwa mfano, somo tunalojifunza kuhusu vipaumbele vya kiroho kutoka kwenye matukio makubwa yaliyotokea kama ukamilifu wa injili ya Mwokozi ilivyorejeshwa katika siku hizi za mwisho.”
Mzee Bedinar aliorodhesha Ono la Kwanza na kuonekana kwanza Moroni kwa Joseph Smith kama fundisho kwa kijana nabii kwanza, asili na tabia ya Mungu, ikifuatiwa na jukumu la Kitabu cha Mormoni na Elia angefanya katika kukusanya Israeli katika pande zote za pazia katika nyakati hizi za mwisho.
Mzee Bednar anahitimisha: “Mfululizo huu wenye msukumo unafundisha kuhusu mambo ya kiroho ya kipaumbele cha juu sana ya Kiungu” (”Mioyo ya Watoto Itageukia,” Liahona, Nov. 2011, 24).
Jambo moja nilililofahamu ni kwamba “mfululizo wa utaratibu” ni nija thabiti, rahisi, asili kwa ajili ya Bwana kutufundisha sisi, kama watoto Wake, kanuni muhimu.
Tumekuja duniani kujifunza na kupata uzoefu ambao la tusingeweza kuwa nao. Kukua kwetu ni kwa kipekee kwa kila mmoja wetu na sehemu muhimu ya mpango wa Baba yetu wa Mbinguni. Kukua kwetu kimwili na kiroho huanza kwa hatua na kuendelea pole pole kadiri tunavyopata uzoefu kwa mfululizo.
Alma anatoa mahubiri yenye nguvu juu ya imani—kutoka kwenye mfano wa mbegu, ambayo, ikiwa itaangaliwa na kuilisha vizuri, chipukizi kutoka kwenye miche midogo na kuwa mti-kamili, uliokomaa ambao huzaa matunda matamu (ona Alma 32:28–43). Somo ni kwamba imani yako itaongezeka kadiri unavyoipa mbegu nafasi na kuilisha—au neno la Mungu—katika mioyo yenu. Imani yako itaongezeka kadiri neno la Mungu linavyoanza “kuvimba ndani ya vifua vyenu” (msitari wa 28). Kwamba “inavyovimba, na kumea, na kuanza kukua” (msitari wa 30) yote ni ya kuonekana na kufunza. Pia ni ya mfululizo.
Bwana anatufundisha kila mmoja wetu kulingana na uwezo wetu wa kujifunza na namna tunajifunza. Kukua kwetu kunategemea kwa undani utashi wetu, matamanio ya asili, kiwango cha imani, na uelewa.
Nefi alifundishwa kile Joseph Smithi angejifunza huko Kirtland, Ohio, zaidi ya miaka 2,300 baadae: “Kwani tazama, hivi asema Bwana Mungu: Nitawapatia watoto wa watu mstari juu ya mstari, amri juu ya amri, hapa kidogo na pale kidogo; na heri wale wanaosikiliza kanuni zangu, na kutii mashauri yangu, kwani watasoma hekima” (2 Nefi 28:30).
Kwamba tunajifunza “msitari juu ya msitari, amri juu ya amri, hapa kidogo na pale kidogo” pia ni mfululizo.
Fikiria kauli zifuatazo tulizosikia mara nyingi maishani mwetu: “Kwanza mambo ya kwanza” au “Walishe maziwa kwanza kabla ya nyama.” Vipi kuhusu “Tunapaswa kutembea kabla ya kukimbia”? Kila moja ya semi hizi huelezea kitu ambacho ni mfululizo.
Miujiza hutenda kulingana na mfululizo wa utaratibu. Miujiza hutendeka kadiri tunavyoonyesha imani. Imani hutangulia miujiza.
Wavulana pia hutawazwa kwenye ofisi za Ukuhani wa Haruni pia hutolewa kwa mfululizo, kulingana na umri wa yule anayetawazwa: shemasi, mwalimu, na baadae kuhani.
Ibada za wokovu na kuinuliwa ni za mfululizo kwa asili. Tunabatizwa kabla ya kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Ibada za Hekaluni ni mfululizo sawa. Naam, kama rafiki yangu Ned Brimley kwa hekima aliweza kunifundisha, sakramenti ni mfululizo—inaanza na mkate, na kufuatiwa na maji.
“Na walipokuwa wakila, Yesu alitwaa mkate na akaumega, na akaubariki, na akawapa wanafunzi wake, akisema, Twaeni, mle.
Kisha akakitwaa kikombe kilichojaa divai na akashukuru na akawapa kikombe, akisema, “Nyweni nyote katika hiki;
“Kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi” (Mathayo 26:26–28).
Katika Yerusalemu na katika Amerika, Mwokozi aliadhimisha sakramenti katika utaratibu uleule.
Tazama, nyumba yangu ni nyumba ya utaratibu, asema Bwana Mungu, na siyo nyumba ya vurugu” (Mafundisho na Maagano 132:8).
Toba ni mfululizo. Inaanza na imani katika Yesu Kristo, hata kama ni punje. Imani inahitaji unyenyekevu, ambayo ni kipengele muhimu cha kuwa na “moyo uliovunjika na roho iliyopondeka” (2 Nefi 2:7).
Hakika, kanuni nne za mwanzo za injili ni mfululizo. “Tunaamini kwamba kanuni na ibada za kwanza za Injili ni: kwanza, Imani katika Bwana Yesu Kristo; pili, Toba; tatu, Ubatizo kwa kuzamishwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi; nne, Kuwekewa mikono kwa ajili ya kipawa cha Roho Mtakatifu” (Makala ya Imani 1:4).
Mfalme Benyamini aliwafundisha watu wake ukweli huu muhimu: “Na mhakikishe kwamba vitu hivi vyote vinafanywa kwa hekima na mpango; kwani haimpasi mwanadamu kukimbia zaidi kuliko nguvu zake. Na tena, ni lazima awe na bidii, ili ashinde zawadi; kwa hivyo, vitu vyote lazima vitendeke kwa mpango” (Mosia 4:27).
Na tuishi maisha yetu kwa utaratibu na kutafuta kufuata mfululizo Bwana ameuonyesha kwa ajili yetu. Tutabarikiwa kadiri tunavyotafuta na kufuata muundo na mfululizo ambao kwao Bwana anafundisha kile kilicho muhimu Kwake. Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.