Mkutano Mkuu
Njoo kwa Kristo na Usije Peke Yako
Mkutano Mkuu wa Oktoba 2021


Njoo kwa Kristo na Usije Peke Yako

Njia bora zaidi ya ninyi kuboresha ulimwengu ni kwa kuuandaa ulimwengu kwa ajili ya Kristo kwa kuwaalika wote kumfuata Yeye.

Hivi karibuni nilipokea barua toka kwa msichana mwenye hamu ya kujifunza. Aliandika: “Nimekwama. … Sina uhakika wa mimi ni nani, lakini nahisi niko hapa kwa ajili ya kitu kikuu.”

Je, umewahi kuhisi aina hiyo ya hisia, ukijiuliza kama Baba wa Mbinguni anakujua wewe ni nani na kama Anakuhitaji? Vijana wangu wapendwa, na kwa wote, ninashuhudia kuwa jibu ni ndio! Bwana ana mpango kwa ajili yako. Yeye amewaandaa kwa ajili ya siku hii, hivi sasa, kuwa nguvu na ushawishi wa uzuri katika kazi Yake. Tunawahitaji! Kiufupi haiwezi kuwa kuu bila ninyi!

Katika hali tukufu, nabii wetu mpendwa, Rais Russell M. Nelson, alinikumbusha kweli mbili rahisi ambazo ni msingi wa kazi yenu kuu na tukufu.

Nikiwa nimekaa kwenye kochi pamoja na mume wangu, nabii wetu mpendwa alivuta kiti chake, karibu kabisa na magoti yetu, na kuniangalia kwa macho yake penyevu ya samawati. Sikuwa na uhakika kama moyo wangu ulikuwa ukienda mbio au ulikuwa umesimama kabisa wakati aliponiita kutumikia kama Rais Mkuu wa Wasichana. Aliniuliza swali ambalo bado linasikika moyoni mwangu, “Bonnie, kipi ni muhimu zaidi ambacho [vijana] wanahitaji kujua?”

Nilitafakari kwa muda na kusema, “Wanahitaji kujua wao ni akina nani.”

“NDIO!” alitamka kwa mshangao, “na wanahitaji kujua dhumuni lao.”

Utambulisho Wetu wa Kiungu

Wewe ni mtoto mpendwa, na wa thamani wa Baba wa Mbinguni. Anakupenda kikamilifu kwamba Alimtuma Mwanawe, Yesu Kristo, kufanya upatanisho kwa ajili yako na mimi.1 Upendo wa Mwokozi kwetu ni usioshindwa—hata pale tunaposhindwa! Hakuna kitakacho tutenganisha na upendo wa Mungu.2 Kukumbuka upendo huu kunaweza kukusaidia kusukuma nyuma mkanganyiko wa ulimwengu ambao unajaribu kudhoofisha ujasiri wako juu ya utambulisho wako wa kiungu na kukupofusha juu ya kile unachoweza kuwa.

Katika Mkutano wa KNV, nilikutana na wasichana wawili ambao wamekuwa wakisumbuka. Wote wawili walizungumzia juu ya kugeukia kwao kwenye baraka za patriaki na kugundua tena upendo wa Bwana na mwongozo binafsi. Tafuta kadi yako ya baraka za patriaki, ifute vumbi kama utahitajika kufanya hivyo, lakini isome kila mara. Kama huna, zitafute—mapema. Usichelewe kugundua kile Bwana anachotaka kukwambia sasa kuhusu wewe ni nani.

Dhumuni Letu la Milele

Ukweli wa pili kutoka kwa Rais Nelson uliosemwa kwetu siku hiyo ni kujua dhumuni letu. Hili ni jukumu kuu na takatifu.

Miaka mingi iliyopita, mwanangu aitwaye Tanner alikuwa na miaka takribani mitano alipocheza mchezo wake wa kwanza wa mpira wa miguu. Alifurahi sana!

Wakati tulipofika kwenye mchezo, tulitambua kwamba timu yake ilikuwa ikitumia goli la kawaida la mpira wa miguu—si goli dogo bali nyavu ambayo ilionekana kuwa kubwa sana kwa mtoto wa miaka mitano.

Mchezo ulioneka kuwa wa muhimu sana wakati nilipomuona Tanner akichukua nafasi yake kama kipa. Nilishangazwa sana. Je, kweli alielewa dhumuni lake kwenye goli?

Kipenga kilipulizwa, na tulimezwa na mchezo na tukasahau yote kuhusu Tanner. Ghafla mmoja wa wachezaji wa timu pinzani alipata mpira na kuukokota kwa haraka kuelekea kwa Tanner. Niliangalia upande aliokuwepo Tanner kuhakikisha kwamba alikuwa tayari kusimama ardhini na kulinda goli. Niliona kitu ambacho sikukitegemea.

Picha
mvulana akicheza kama mlinda goli

Wakati fulani katika mchezo, Tanner alikuwa ameacha kuwa makini na kuanza kupunga mkono wake wa kushoto kupitia matundu mbalimbali ya nyavu. Kisha alifanya kitu hicho hicho kwa mkono wake wa kulia. Baadaye, kwa mguu wake wa kushoto. Mwishowe, kwa mguu wake wa kulia. Tanner alikuwa amekamatwa kabisa kwenye nyavu. Alikuwa amesahau dhumuni lake na kile alichokuwa ameaminiwa kukifanya.

Picha
Mvulana amenaswa na wavu

Wakati malengo ya Tanner kwenye mpira wa miguu hayakudumu sana, somo lake kwangu siku ile kamwe halitafutika. Sote wakati fulani tunavurugwa umakini kutoka kujua kwa nini tuko hapa na kutumia nguvu zetu mahali pengine kabisa. Moja kati ya silaha zenye uwezo sana za Shetani ni kutukanganya na vitu ambavyo ni vizuri na vizuri zaidi ambavyo, katika wakati wa uhitaji, vinaweza kutupofusha na kututoa kwenye kazi nzuri—kazi hasa ambayo tumeitiwa hapa ulimwenguni.3

Dhumuni letu la milele ni kwenda kwa Kristo na kikamilifu kujiunga Nae katika kazi Yake kuu. Ni rahisi kama vile kufanya kile Rais Nelson alichokifundisha “Muda wowote tunapofanya kitu fulani ambacho kinamsaidia yoyote … kushika na kutunza maagano yao na Mungu, tunasaidia kukusanya Israeli.” Na wakati tunapofanya kazi Yake pamoja Naye, tutamjua na kumpenda Yeye zaidi.

Tunaendelea daima kutafuta kusonga karibu na Mwokozi kupitia imani, toba ya dhati na kutii amri. Wakati tukiunganishwa Naye kupitia maagano na ibada, maisha yetu yanajazwa na ujasiri,5 ulinzi,6 na shangwe ya kina na ya kudumu.7

Tunaposonga kwake, tunawaona wengine kupitia macho Yake.8 Njoo kwa Kristo. Njoo sasa, lakini usije peke yako!9

Injili ya Yesu Kristo si tu ni nzuri; bali ni muhimu kwa wote. “Hakuna njia nyingine wala gharama ambayo kwayo [sisi] tunaweza kuokolewa, isipokuwa kupitia kwa Kristo.”10 Tunamhitaji Yesu Kristo! Ulimwengu unamhitaji Yesu Kristo.11

Kumbuka, njia bora zaidi ya ninyi kuboresha ulimwengu ni kwa kuuandaa ulimwengu kwa ajili ya Kristo kwa kuwaalika wote kumfuata Yeye.

Kuna hadithi ya kutia nguvu katika Kitabu cha Mormoni kuhusu Mwokozi aliyefufuka akitumia muda pamoja na Wanefi. Je unaweza kufikiria hiyo ingekuwaje?

Wakati Kristo alipotangaza kwamba Yeye lazima arudi kwa Baba, “aliutazama umati tena.”12 Akiona machozi kwenye macho ya watu, Alijua mioyo yao ilitamani Abaki.

Picha
Mwokozi akiwaalika Wanefi ili waponywe

Aliuliza: “Mnao wowote ambao ni wagonjwa miongoni mwenu? Waleteni hapa. Mnao wowote ambao ni viwete, au vipofu, … viziwi, au ambao wanateseka kwa njia yoyote? Waleteni hapa na nitawaponya.”13

Akiwa na huruma nyingi, Yeye haweki ukomo na huwaita wote ambao “wanateseka kwa njia yoyote.” Ninapenda kwamba hakuna kilicho kikubwa sana au kidogo sana ambacho Yesu Kristo hawezi kuponya.

Yeye anajua masumbuko yetu na mahangaiko vilevile na anatuita, Waleteni wenye wasiwasi na mvunjiko wa moyo, waliochoka, wenye majivuno na wasioeleweka, “wapweke, au wale ambao wanateseka kwa njia yoyote.”

Picha
Uponyaji wa Mwokozi

Na umati wote “ulisonga mbele … ; na akawaponya kila mmoja wao. …

“… Na wote ambao walikuwa wameponywa, na wale ambao walikuwa wazima, waliinama chini miguuni mwake, na kumwabudu.”14

Kila mara ninaposoma hili, najiuliza: Je , ni nani nitamleta kwa Kristo? Je, nani utamleta ?

Je, tunaweza kuangalia tena, kama Yesu alivyofanya, ili kuhakikisha hakuna anayekosekana na kuwaalika kila mmoja kuja kumjua Yeye?

Acha nishiriki mfano wa jinsi inavyoweza kuwa rahisi. Rafiki yangu mdogo Peyton, wa miaka 15, alikuwa na lengo rahisi la kusoma mistari mitano ya maandiko wakati wa kifungua kinywa kila siku, lakini hakufanya hivyo mwenyewe. Akiangalia tena, Peyton aliwaalika wazazi wake na ndugu, hata kaka yake wa miaka mitano kufanya hivyo pia. Tendo hili ndogo ni kile ambacho Kristo alikifundisha wakati Alipowaalika, “waleteni hapa.”

Mwaliko huu kutoka kwa Bwana bado unatolewa hivi leo. Wasichana na wavulana, anzeni sasa, katika nyumba zenu. Je mnaweza kusali na kumuuliza Baba wa Mbinguni jinsi mnavyoweza kuwasaidia wazazi wenu wakati wakiendelea kuja kwa Kristo? Wanawahitaji kama vile mnavyowahitaji.

Kisha waangalieni tena ndugu zenu, marafiki na majirani. Ni nani utakayemleta kwa Kristo?

Mwokozi wetu alitangaza, “Tazama mimi ndimi nuru; nimewapatia mfano.”15 Tutahisi upendo na amani ya Mwokozi wakati tukiungana Naye katika kuokoa familia ya Mungu, kwani Ameahidi, “Yeye anifuataye, kamwe hatatembea gizani, lakini atakuwa na mwangaza wa maisha.”16

Ni wakati mtukufu ulioje kujihusisha katika kazi ya Kristo!

Ndio, mko hapa kwa ajili ya kitu kikuu. Ninaungana na Rais Nelson, ambaye alisema “Bwana anawahitaji ninyi muubadili ulimwengu. Mnapokubali na kufuata mapenzi Yake kwa ajili yenu, mtajikuta mkitimiza yasiyowezekana!”17

Kwa uthabiti ninashuhudia kwamba Bwana anawajua ninyi ni akina nani, na Anawapenda! Kwa pamoja, tutaendeleza dhumuni Lake mpaka siku ile kuu ambapo Kristo mwenyewe atarudi kwenye ulimwengu huu na kutuita kila mmoja wetu njoo “hapa.” Kwa furaha tutakusanyika pamoja, kwani sisi ni wale wanaoenda kwa Kristo, na hatuendi peke yetu. Katika Jina la Yesu Kristo, amina.

Chapisha