Mkutano Mkuu
Kuwakubali Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo na Maafisa Wakuu
Mkutano Mkuu wa Oktoba 2021


Kuwakubali Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo na Maafisa Wakuu

Akina kaka na dada, kama ilivyotangazwa, sasa nitawasilisha kwenu Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo na Maafisa Wakuu wa Kanisa kwa ajili ya kura yenu ya kuwakubali.

Tafadhali onesha kura yako katika njia iliyozoeleka popote ulipo. Kama kuna wale wanaopinga mapendekezo yoyote yaliyowasilishwa, tunaomba kwamba muwasiliane na rais wenu wa kigingi.

Inapendekezwa kwamba tumuidhinishe Russell Marion Nelson kama nabii, mwonaji na mfunuzi na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho; Dallin Harris Oaks kama Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza; na Henry Bennion Eyring kama Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza.

Wale wanaounga mkono wanaweza kuonesha.

Wale wanaopinga, kama wapo, wanaweza kuonesha.

Inapendekezwa kwamba tumuidhinishe Dallin H. Oaks kama Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili na M. Russell Ballard kama Kaimu Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.

Wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Yeyote anayepinga anaweza kuonesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: M. Russell Ballard, Jeffrey R. Holland, Dieter F. Uchtdorf, David A. Bednar, Quentin L. Cook, D. Todd Christofferson, Neil L. Andersen, Ronald A. Rasband, Gary E. Stevenson, Dale G. Renlund, Gerrit W. Gong na Ulisses Soares.

Wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Yeyote anayepinga anaweza kuonesha.

Inapendekezwa kwamba tuwaidhinishe washauri katika Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji na wafunuzi.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Kinyume, kama kuna yeyote, kwa ishara hiyo hiyo.

Tumewapumzisha Wazee J. Devn Cornish, Timothy J. Dyches, David F. Evans, Robert C. Gay, James B. Martino na Terence M. Vinson Kama Sabini Wenye Mamlaka na kuwapa hadhi hiyo wakiwa wamestaafu.

Wale ambao wangependa kutoa shukrani kwa ndugu hawa na familia zao kwa huduma yao ya kujitolea wanaweza kufanya hivyo kwa kuinua mkono juu.

Tunatambua kwamba Mzee Dean M. Davies, ambaye alifariki mnamo Agosti 31, 2021 angepumzishwa kama Sabini mwenye mamlaka kwenye mkutano huu. Tunatanguliza rambirambi zetu za dhati kwa Dada Darla Davies na familia, pamoja na shukrani kwa huduma ya Mzee Davies ya kujitolea.

Pia tunatambua kwa shukrani, Sabini wa Maeneo ambao wamemaliza huduma yao mwaka uliopita.

Wale wanaotaka kuungana pamoja katika kudhihirisha shukrani kwa ndugu hawa kwa huduma yao bora, tafadhali dhihirisheni.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali Viongozi wengine Wakuu Wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo—ikijumuisha Sabini wawili wapya wa Maeneo waliotangazwa wiki hii kwenye newsroom.ChurchofJesusChrist.org—na Maafisa wakuu kama ilivyo sasa.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Wanaopinga, kama kuna yeyote.

Tunawashukuru kwa imani yenu endelevu na sala kwa niaba ya viongozi wa Kanisa.

Mabadiliko kwa Sabini wa Maeneo

Sabini wa Maeneo wafuatao waliidhinishwa wakati wa kikao cha uongozi kilichofanyika kama sehemu ya mkutano mkuu:

Pedro E. Hernández na Charden Ndinga.

Sabini wa Maeneo wafuatao walipumzishwa wakati wa kikao cha uongozi kilichofanyika kama sehemu ya mkutano mkuu:

Guillermo I. Guardia na Gaëtan Kelounou.

Sabini wa Maeneo wafuatao walipumzishwa mnamo Agosti 1, 2021:

P. David Agazzani, Quilmer A. Agüero, Frederick O. Akinbo, Nelson Ardila, Richard C. Baquiran, Dong Chol Beh, Matthieu Bennasar, Lawrence P. Blunck, Luis J. Camey, Douglas B. Carter, Aroldo B. Cavalcante, Luis C. Chaverri, Ulises Chávez, Brent J. Christensen, Douglas L. Dance, M. T. Ben Davis, Marc C. Davis, J. Scott Dorius, M. Dirk Driscoll, Antonio F. Faúndez, José A. Fernández, Matías D. Fernández, Candido Fortuna, Bruce E. Ghent, Michael A. Gillenwater, Michael D. Groll, Daniel G. Hamilton, Tom-Atle Herland, Raymond S. Heyman, Jerat K. C. Igwe, Christophe Kawaya, John A. Koranteng, Ming-Shun Kuan, Todd S. Larkin, Juan J. Levrino, Carlo M. Lezano, Felix A. Martinez, J Vaun McArthur, Kevin K. Miskin, Helamán Montejo, Michael R. Murray, Ryan V. Pagaduan, A. Moroni Pérez, Carlos E. Perrotti, Mark P. Peteru, Thomas T. Priday, Brian L. Rawson, Rene Romay, Blake M. Roney, Luis G. Ruiz, Maximo A. Saavedra Jr., Pedro A. Sanhueza, Eric J. Schmutz, Paul H. Sinclair, Benjamin T. Sinjoux, David L. Stapleton, Daniel Texeira, Seiji Tokuzawa, Maxsimo C. Torres, Jesús Vélez, Carlos Villarreal, Paul H. Watkins, Robert K. William, C. Dale Willis, Kevin J Worthen na Luis G. Zapata.

Chapisha