2021
Hekalu na Msingi Wako wa Kiroho
Novemba 2021


“Hekalu na Msingi Wako wa Kiroho,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Nov. 2022.

Kikao cha Jumapili Asubuhi

Hekalu na Msingi Wako wa Kiroho

Dondoo

Yesu Kristo

Sitataka, na Yongsung Kim

Ukarabati wa Hekalu la Salt Lake

Mahali pa ujenzi wa Hekalu la Salt Lake

Kama mnavyojua, tunafanya marekebisho makubwa kwenye Hekalu la kihistoria la Salt Lake. …

Tunafanya kila juhudi inayowezekana ili kulipa hekalu hili la heshima, ambalo limezidi kuwa dhaifu, msingi ambao utastahimili nguvu za asili mpaka kwenye milenia. Katika hali sawa na hiyo, ni muda sasa kwamba kila mmoja achukue hatua za ziada—huenda hatua ambazo hatujawahi kuzichukua hapo kabla—ili kuimarisha misingi yetu binafsi ya kiroho. Nyakati za kipekee huhitaji hatua za kipekee.

Akina kaka na dada zangu wapendwa, hizi ni siku za mwisho. Kama mimi na wewe tunapaswa kustahimili hatari na mashinikizo yajayo, ni muhimu kwamba kila mmoja awe na msingi imara wa kiroho uliojengwa juu ya mwamba wa Mkombozi wetu, Yesu Kristo.

Kwa hivyo ninawauliza kila mmoja wenu, Msingi wako ni imara kiasi gani? Na ni uimarisho gani unahitajika kwenye ushuhuda na uelewa wako wa injili?

Hekalu ni kitovu cha kuimarisha imani yetu na uimara wa kiroho kwa sababu Mwokozi na mafundisho Yake ndiyo kiini hasa cha hekalu. …

Kama bado hupendi kuhudhuria hekaluni, nenda mara kwa mara—siyo mara chache. Acha Bwana, kupitia Roho Wake, akufundishe na kukupa msukumo ukiwa huko. …

Tafadhali mniamini ninaposema kwamba wakati msingi wako wa kiroho unapojengwa kwa uimara juu ya Yesu Kristo, huna haja ya kuogopa. Unapokuwa mkweli kwenye maagano yako uliyoyafanya hekaluni, utaimarishwa kwa nguvu yake. Kisha, wakati matetemeko ya kiroho yajapo, utaweza kusimama imara kwa sababu msingi wako wa kiroho ni imara na usioyumba.