2021
Urejesho wa Kila Siku
Novemba 2021


“Upendo wa Mungu,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Nov. 2022.

Kikao cha Jumapili Asubuhi

Urejesho wa Kila Siku

Dondoo

msichana akiwa kwenye ngazi, akifikia mwangaza juu yake

Je, si ya kushangaza jinsi vitu vidogo, vionekanavyo visivyo vya muhimu vinaweza kuleta tofauti kubwa katika maisha yetu? …

Mabadiliko mengi katika maisha yetu ya kiroho—yote chanya na hasi—hutokea taratibu, hatua kwa hatua. …

… Tuna alama muhimu zinazotegemewa na zinazoonekana ambazo tunaweza kutumia kutathmini mwenendo wetu.

Na alama hizi ni nini?

Hakika zinajumuisha sala ya kila siku na kutafakari maandiko na kutumia nyenzo zilizovuviwa kama Njoo, Unifuate. Kila siku, tunaweza kukikaribia kiti cha Mungu kwa unyenyekevu na uaminifu. Tunaweza kutafakari matendo yetu na kurejelea nyakati za siku yetu—tukilinganisha mapenzi na nia zetu na zile za Kwake. …

Ifikirie kama urejesho wako binafsi wa kila siku. Kwenye safari yetu kama wafuasi tukielekea njia ya utukufu, tunajua ni jinsi gani ilivyo rahisi kuanguka. Lakini kama vile tofauti ndogo inavyoweza kututoa kwenye Njia ya Mwokozi, vivyo hivyo vitendo vidogo na rahisi vya urekebishaji vinaweza kutuongoza kurejea. …

… Tunaweza kutembea kwenye njia yetu kupita kiza na majaribu ya maisha haya na kuipata njia yetu ya kurudi kwa Baba yetu mpendwa wa Mbinguni kama tutatafuta na kuzikubali alama elekezi za kiroho Yeye alizotoa, kuthamini ufunuo binafsi, na kujitahidi kwa ajili ya urejesho wa kila siku. Hivi ndivyo tunavyokuwa wafuasi wa kweli wa Mwokozi wetu mpendwa, Yesu Kristo.