“Mwalike Kristo Aandike Hadithi Yako,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Nov. 2022.
Kikao cha Jumapili Asubuhi
Mwalike Kristo Aandike Hadithi Yako
Dondoo
Nashuhudia kwamba Mwokozi ndiye “mwanzilishi na mkamilishaji wa imani yetu.” [Waebrania 12:2]. Je, utamwalika awe mwanzilishi na mkamilishaji wa hadithi yako?
Kanuni tukufu ya uhuru wa kujichagulia inaturuhusu tuandike hadithi zetu wenyewe—Daudi angeweza kurudi nyumbani, kwenye kuchunga kondoo. Lakini Yesu Kristo yuko tayari kututumia kama vyombo vitakatifu, penseli zilizonolewa mkononi Mwake, ili kuandika kitu cha thamani kubwa! …
… Kumruhusu Mungu ashinde, kumfanya Yeye awe mwanzilishi na mkamilishaji wa hadithi zetu, inahitaji sisi kushika amri zake na maagano ambayo tumefanya. Ni katika kushika kwetu amri na agano ambapo kutafungua njia ya mawasiliano ya sisi kupokea ufunuo kupitia Roho Mtakatifu. Na ni kupitia udhihirisho wa Roho kwamba tutahisi mkono wa Mwalimu ukiandika hadithi zetu pamoja nasi. …
Kwa nini tunataka Mwokozi awe mwanzilishi na mkamilishaji wa hadithi zetu? Kwa sababu anajua uwezo wetu kikamilifu, Atatufikisha mahali ambapo hatujawahi kupafikiria. Anaweza kutufanya kuwa Daudi au Esta. Atakuza uwezo wetu na kutusafisha ili tufanane Naye zaidi. Vitu tutakavyopokea tunapotenda kwa imani zaidi vitaongeza imani yetu katika Yesu Kristo. …
Tutahukumiwa kwa kitabu chetu cha uzima. Tunaweza kuchagua kujiandikia hadithi nzuri. Au tunaweza kumruhusu Mwandishi Mkuu na Mkamilishaji aandike hadithi yetu pamoja nasi, tukiruhusu jukumu Analohitaji sisi kufanya kuwa kipaumbele kuliko matamanio mengine.
Hebu Kristo awe mwanzilishi na mkamilishaji wa hadithi yako!