2022
“Tunaweza kuishi na kufanikiwa katika imani na shangwe”: Ziara ya Afrika ya Mzee Ronald A. Rasband
Aprili 2022


KURASA ZA ENEO

“Tunaweza kuishi na kufanikiwa katika imani na shangwe”: Ziara ya Afrika ya Mzee Ronald A. Rasband

Mnamo jioni ya Jumanne ya terehe 16 Novemba, kijana kutoka Afrika aliuliza swali la kutaka kujua kwa Mzee Rasband wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.

“Wakati wa janga la ulimwengu vijana wengi waseja walijikuta katika kufifia kiakili, kihisia na kiroho kutokana na kutojumuishwa,” mtu huyu alisema. “Ni ujumbe gani unao kwa wale wanaokabiliana na afya ya kiakili na kupitia hisia za kukata tamaa, woga au kukosa matumaini?”

Ilikuwa ni moja ya maswali kadhaa yasiyojulikana ya vijana wadogo na vijana wakubwa kutoka nchi 32 za maeneo ya Kati na Kusini mwa Afrika, ambaye alijiunga kuangalia majibu yake kwenye live Facebook broadcast.

Viongozi kadhaa wa Kanisa ulimwenguni na wa maeneo husika walihudhuria, na Kusimamiwa na Mzee Rasband. Hii ilihusisha Mzee Patrick Kearon (Rais Mwandamizi wa Sabini), na mkewe Jennifer; Askofu L. Todd Budge (wa Uaskofu Simamizi) na mkewe Lori; Mzee Christoffel Golden (Rais wa Eneo la Kusini mwa Afrika) na mkewe Diane; na Gladys Sitati, mke wa Mzee Joseph W. Sitati (Rais wa Eneo la Afrika ya Kati).

Kwa pamoja, walitoa ushauri na ushuhuda wa kutia moyo katika mada za chanjo ya Uviko-19, kunyanyaswa kijinsia, hadi kwenye majadiliano ya sifa ambazo mtu anapaswa kuzingatia kwa mwenza wake wa baadaye.

Takribani michango 800 ilitolewa kutoka kwa watazamaji waliokuwa wakiangalia kwa takribani saa moja.

“Asante kwa muda huu mzuri na roho tuliyemhisi wakati wa kipindi hiki,” alisema Yvresse Rousseau kutoka Kongo Brazzaville.

“Matangazo haya kweli yamesaidia,” alichangia Natalie Kapema kutoka Zambia.

Tukio hili lilikuwa sehemu ya ziara ya siku 11 Afrika ya Mzee Rasband, akina Kearons na Budges.

Kwa msaada wa teknolojia, viongozi waliotembelea walifanya Mikutano ya Uongozi wa Kikuhani na mikutano mingine katika Eneo la Afrika ya Kati na kuhudhuria katika mikutano ya kigingi huko Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Nairobi, Kenya. Viongozi pia walikutana kwa njia ya mtandao pamoja na wamisionari wanaotumikia Gabon na Cameroon, pamoja na wale ambao hivi karibuni wameondolewa kutoka Ethiopia kutokana na machafuko. Walikutana na viongozi wa kanisa na waumini katika Eneo la Kusini mwa Afrika na kufanya safari ya ghafla katika Kituo kilichokuwa kikifunguliwa upya cha Mafunzo ya Wamisionari huko Roodepoort, magharibi mwa Johannesburg, Afrika Kusini. Katika mandhari nyingi, Mzee Rasband alialika na kujibu maswali kutoka kwa watakatifu.

‘Ilikuwa ni kama vile Bwana anaongea mubashara kwenye changamoto zetu’

Mzee Joseph W. Sitati, Rais wa Eneo la Afrika ya Kati, alisema kwamba ujio wa Mzee Rasband—ambaye hivi karibuni amepangiwa kama Mtume Kiongozi kwa ajili ya Eneo la Kati na Kusini mwa Afrika—kunaleta hisia kwamba Bwana alikuwa anawafikia watakatifu wa bara la Afrika.

“Kuwa na Mtume wa Bwana aliyefokasi mahsusi kwenye Kanisa katika Eneo la Afrika ya Kati ilikuwa ni kama kuwa na Bwana Mwenyewe akiongea moja kwa moja kwenye changamoto ambazo sisi kama viongozi na waumini huzipitia,” alisema.

Mzee Christoffel Golden, Rais wa Eneo la Kusini mwa Afrika, aliangazia baadhi ya jumbe ambazo zilibeba umuhimu wa ziara ya Mzee Rasband.

“Kanuni ya kwanza ilihusisha upendo,” alisema. “Mzee Rasband alisisitiza umuhimu wa kukuza upendo wa Mungu na upendo kwa wenzetu.

Pia “alitushauri kama viongozi kuliimarisha Kanisa na kuishi injili hapa Afrika,” kisha Mzee Golden aliendelea. “Alionyesha kwamba Bwana na Nabii wake, Russell M. Nelson, Urais wa Kwanza na Mitume Kumi na Wawili wanatupenda, wanafurahia huduma yetu na hutuhitaji katika kazi hii takatifu.

Pamoja na hilo ulikuja wito wa dhati wa kumfuata nabii anayeishi. Hili, alisema Mzee Sitati “lilikuwa jambo dhahiri katika muda ambao si tu wengi hawajachanjwa dhidi ya Uviko-19, lakini pia tuna sehemu kadhaa ambako kuna ongezeko la wasiwasi kutokana na kukosekana kwa amani kama vile Ethiopia, Uganda na baadhi ya maeneo ya DRC.”

‘Imani na Shangwe, bila kujali hali tuzipitiazo’

Lakini pamoja na changamoto hizi, alisema Mzee Golden, “tumepewa uhakika wa Kitume kwamba tunaweza kuishi na kufanikiwa katika imani na shangwe, bila kujali tunaishi wapi, katika hali zote na nyakati zote—hata katika janga la sasa laUviko-19.”

Mzee Sitati alielezea “faraja na hakikisho” ambalo huja kutoka kwa Mtume.

“Katika kuchangamana kwangu na Mzee Rasband, nimehisi ushahidi wa hakikisho ndani ya moyo wangu kwamba ni Mtume wa Bwana,” alisema. “Ni vigumu kwangu kuelezea vyema hisia za mtu mwingine, lakini kuwa karibu naye kumenifanya nijihisi mtakatifu.”

Muda mfupi kabla ya kurejea Marekani, Mzee Rasband alisema kwamba “alikuwa ameshangazwa na kupendezwa na” watu aliochangamana nao hapa Afrika.

“Hii ni mara ya sita nimepata kuwa Afrika na mara zote nafurahishwa na kuinuliwa na kila mmoja,” alisema. “Iwe uongozi ambao tumekuwa nao, au waumini, au wamisionari—ninavutiwa na watu hawa wema ambao wanafanya kwa kadiri wawezavyo na kujenga kanisa la Bwana na ufalme.”

Chapisha