2022
Aprili 2019: Uwekaji Wakfu wa Hekalu la Kinshasa
Aprili 2022


Mwezi Huu katika Historia ya Kanisa

Aprili 2019: Uwekaji Wakfu wa Hekalu la Kinshasa

Mnamo tarehe 6 Aprili 1830, kundi la wanawake na wanaume takriban 40 walikutana nyumbani kwa Peter Whitmer Mkubwa huko Fayette, New York kuanzisha Kanisa la kweli la Bwana. Kanisa lilijulikana kama Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho na kundi dogo la watu lilimkubali Joseph Smith kama Rais wa Kanisa na nabii wao. Mwaka uliofuatia ilifunuliwa kwa Joseph Smith kwamba “funguo za ufalme wa Mungu zimekabidhiwa kwa mwanadamu duniani, na tangu hapo na kuendelea injili itaenea kote hadi miisho ya dunia, na kutoka huko injili itaenea hata miisho ya dunia, kama vile jiwe lililochongwa mlimani bila kazi ya mikono litabiringika, hadi litaijaza dunia yote” (Mafundisho na Maagano 65:2).

Miaka mia moja themanini na tisa baada ya Kanisa kuanziswa, Hekalu la Kinshasa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo liliwekwa wakfu mnamo tarehe 14 ya Aprili 2019, likiwa hekalu la 163 linalofanya kazi la Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Lilikuwa hekalu la nne kuwekwa wakfu katika Bara la Afrika na la kwanza katika Eneo la Kati la Afrika.

Kanisa lililoanza na kundi dogo la waumini waliokuwa wamebatizwa punde mnamo Aprili ya 1830 linaendelea “kuenea” na kuijaza dunia yote kwa takriban waumini 700,000 kwenye Bara la Afrika pekee.