2022
Kanisa Linawalisha Watu 2,500 Wenye Njaa Ethiopia
Disemba 2022


Habari za Kibinadamu

Kanisa Linawalisha Watu 2,500 Wenye Njaa Ethiopia

Vifurushi vya chakula vilisambazwa kwa familia zaidi ya 500 huko Megenagna.

Takriban familia 550 zilizokabiliwa na umasikini zinazoishi Megenagna, Addis Ababa, zimepokea chakula kutoka Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kwa miezi kadhaa iliyopita, pamoja na zaidi ya watu 2,500 wenye njaa wakingojea kushibishwa.

Viongozi wa serikali kuu kutoka Megenagna huko Woreda (wilaya) 5, ambayo ina idadi kubwa ya watu wasio na makazi na wanaohangaika kiuchumi, wanafanya kazi sambamba na Kanisa kutambua familia zinazopaswa kupokea chakula. Vifurushi vya chakula vitasambazwa na shirika lisilo la kiserikali linalojulikana kama Real Humanitarian.

Mnamo Julai 16, 2022, Kanisa lilishiriki kwenye mpango wa chakula kama uanzishaji wa mkakati. Mzee Joseph Nelson, mmisionari wa Misheni ya Ethiopia Addis Ababa, alisema ilikuwa ni fursa ya kutoa msaada kwa wale katika jamii ambao aidha wanatafuta kazi au kuwasaidia watu wengi ambao wamehamishwa kwa sababu ya vita vya huko Ethiopia Kaskazini.

Mmoja wa watu hao ni Tigist Negus Kiros. “Nilikuja Addis Ababa peke yangu kwa sababu familia yangu ilikuwa kwenye uhitaji kutokana na vita katika kijiji chetu,” alisema Bwana Kiros. “Kwa kupata chakula hiki, nitaweza kutunza fedha zaidi za kuwatumia familia yangu ili waweze kuja hapa na kujiunga nami ili tuwe salama dhidi ya vita.”

Mpokeaji mwingine alikuwa Selam Mattieos Ayele, aliyesema kwamba kifurushi cha chakula kiliwakilisha tumaini kwa familia yake. “Nyakati hapa Ethiopia zimekuwa ngumu sana na ni vigumu kupata kazi na kupata chakula,” alisema Bwana Ayele.

“Natumaini kwamba chakula hiki kitawatosha familia yangu na tunaweza kunusurika kupita msimu huu wa mvua.”

Kwenye tukio, kiongozi wa eneo husika wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, Bwana Brehanu Molla aliviambia vyombo vya habari, wana jamii na viongozi ambao Kanisa limewapa msaada katika juhudi ya kufuata mafundisho ya Yesu Kristo.

“Kwa vile sote tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, tunahitajika kutenda mema kwa wanadamu wenzetu na kutoa kile tulichonacho kwa wenye uhitaji,” Bwana Molla alifafanua.

“Tunapaswa kufanya sehemu yetu ili kuleta amani na ustawi kwenye nchi yetu. Kanisa litaendelea kuwasaidia wenye uhitaji.”

Mzee Joshua Caleb Folau, mmisionari wa Kanisa ambaye alikuwepo kwenye tukio, alishiriki hisia zake kuhusu uzoefu huo.

“Fursa hii ya kufanya kazi na jamii ya eneo husika ili kutimiza mahitaji ya wale wanaoteseka inatuwezesha sisi kuleta tofauti wakati tukihudumu kama ambavyo Mwokozi angefanya,” alisema. “Yeye anampenda kila mmoja wetu zaidi ya vile tunavyodhani.”

Chapisha