Njoo, Unifuate 2024
Machi 18–24: “Hii Ndiyo Njia.” 2 Nefi 31–33


“Machi 18–24: ‘Hii Ndiyo Njia.’ 2 Nefi 31–33,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2024)

“Machi 18–24. 2 Nefi 31–33,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2024)

Picha
Yesu akiwafundisha wafuasi Wake

Kristo Akiwafundisha Wafuasi Wake, na Justin Kunz

Machi 18–24: “Hii Ndiyo Njia”

2 Nefi 31–33

Miongoni mwa maneno ya mwisho ya Nefi yaliyoandikwa, tunaona tamko hili: “Bwana ameniamuru, na lazima nitii” (2 Nefi 33:15). Huu ni ufupisho mzuri wa maisha ya Nefi. Alijaribu kuelewa mapenzi ya Mungu na kwa ujasiri kuyatii—iwe hiyo ilimaanisha kuhatarisha maisha yake ili ayapate yale mabamba ya shaba kutoka kwa Labani, kujenga merikebu na kuvuka bahari, au kwa uaminifu kufundisha mafundisho ya Kristo kwa uwazi na kwa nguvu. Nefi angeweza kuzungumza kwa ushawishi mkubwa juu ya umuhimu wa “kusonga mbele mkiwa na imani imara katika Kristo,” juu ya kufuata “njia hii nyembamba na iliyosonga ambayo inaelekea uzima wa milele” (2 Nefi 31:20, 18), kwa sababu hiyo ndiyo njia yeye aliyoifuata. Alijua kupitia uzoefu kwamba njia hii, ingawaje ni ngumu wakati mwingine, pia ina shangwe, na kwamba, “hakuna njia nyingine wala jina lililotolewa chini ya Mbingu ambalo mwanadamu anaweza kuokolewa katika ufalme wa Mungu” (2 Nefi 31:21).

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

2 Nefi 31

Yesu Kristo na mafundisho Yake ndiyo njia pekee kwenye uzima wa milele.

Kama wewe ungehitajika kufanya muhtasari wa njia ya uzima wa milele kwa maneno machache tu, ungesema nini? Ona ni jinsi gani Nefi anavyoeleza hili katika 2 Nefi 31. Fikiria kuchora njia na andika pembezoni mwa njia hiyo baadhi ya kanuni au hatua unazozipata kwenye milango hii. Ungeweza kuongeza kwenye mchoro wako ufupisho wako mwenyewe wa kitu ambacho Nefi alikifundisha kuhusu kila kanuni.

Wakati ukisoma 2 Nefi 31:18–20, tathmini juhudi zako mwenyewe za “kusonga mbele” katika njia ya injili.

Ona pia “Songeni Mbele Watakatifu,” Nyimbo za Dini, na. 38.

Picha
familia ikisali pamoja

Kufuata mafundisho ya Yesu Kristo kunatuongoza hadi kwenye uzima wa milele.

2 Nefi 31:4–13

Yesu Kristo alionesha mfano mkamilifu wa utiifu wakati alipobatizwa.

Iwe ubatizo wako ulifanyika jana au miaka 80 iliyopita, ulikuwa ni wakati muhimu. Wewe uliingia katika agano la milele la kumfuata Yesu Kristo. Fikiria kuhusu ubatizo wako unaposoma kuhusu ubatizo wa Mwokozi katika 2 Nefi 31:4–13. Kujibu maswali kama haya inaweza kusaidia:

  • Kwa nini Kristo alibatizwa? Kwa nini nilichagua kubatizwa?

  • Je, ni ahadi zipi niliziweka wakati nilipobatizwa? Je, Bwana anaahidi nini kama baraka? (ona mistari 12–13; ona pia Mosia 18:10, 13).

  • Je, ninawezaje kuonesha kwamba bado nina nia ya dhati ya kumfuata Yesu Kristo?

2 Nefi 31:15–20.

“Yule atakayevumilia hadi mwisho, huyo ataokolewa.”

Wakati ukisoma 2 Nefi 31:15–20, jiulize mwenyewe, “Je, nawezaje kujua ikiwa navumilia hadi mwisho?” Je, unajifunza nini kutoka kwa Nefi ambacho kinakusaidia ujibu swali hili?

Mzee Dale G. Renlund alifundisha: “kuvumilia hadi mwisho siyo hatua iliyojitenga katika fundisho la Kristo—kama vile tunamaliza hatua nne za mwanzo na kisha tunachuchumaa chini, kusaga meno yetu na kusubiri kufa. Hapana, kuvumilia hadi mwisho ni hatua zinazojirudia, thabiti na za dhati” (“Lifelong Conversion” [Brigham Young University devotional, Sept. 14, 2021], 2, speeches.byu.edu). Je unawezaje kurudia hatua kwenye injili ya Kristo (imani, toba, ubatizo na kumpokea Roho Mtakatifu)?

Picha
ikoni ya seminari

2 Nefi 32; 33:2

Kupitia maneno ya Kristo na Roho Mtakatifu, Mungu atanionesha kipi cha kufanya.

Je, umewahi kuhisi kutokuwa na hakika kuhusu hatua zinazofuata katika maisha yako? Watu wa Nefi walikuwa na mashaka kama hayo (ona 2 Nefi 32:1). Angalia jibu la Nefi katika 2 Nefi 32:2–9. Je, ungeelezaje kwa maneno yako mwenyewe kile ambacho Nefi alikifundisha? Je, ni mambo yapi yamekufundisha kwamba maneno ya Nefi ni ya kweli?

Fikiria kutengeneza orodha ya maamuzi au hali (za sasa na baadae) ambazo kwazo unahitaji mwongozo wa Mungu. Je, wewe unaweza kujifunza nini kutoka 2 Nefi 32 ambacho kitakusaidia ufanikiwe katika kupokea mwongozo wa kiungu kutoka Kwake? Je, ni kipi kinaweza kusababisha watu “washupaze mioyo yao dhidi ya Roho Mtakatifu”? (2 Nefi 33:2).

Wakati ukitafakari ushauri wa Nefi, fikiria kuhusu jinsi gani unajifunza maneno ya Mwokozi. Je, ungeelezea hali hii kama kula kitafunwa au karamu? Je, tofauti ni ipi, kwa maoni yako? Fikiria jinsi unavyoweza kuuweka uzoefu wako kwa maneno ya Mwokozi uwe zaidi kama karamu. Pengine ungeweza kupata mawazo kutoka kwa rafiki au mwanafamilia.

Kusherehekea Maneno ya Kristo. Kuna njia nyingi za kusherehekea maneno ya Kristo, ikijumuisha kusali kwa ajili ya kupata mwongozo wa kiungu, kuuliza maswali kabla na wakati wa kujifunza, kufafanua maneno, kutafakari, kurejelea, kuandika ufupisho, kutafuta kweli za injili na kulinganisha maandiko na maisha yetu (ona 1 Nefi 19:23).

Je, unamwalikaje Roho Mtakatifu awe mwenzi wako daima katika maisha yako, kuliko kuwa kama mgeni wa muda? Soma mapendekezo matatu ya David A. Bednar ili kufanya wenzi wa Roho Mtakatifu kuwa “uhalisia endelevu” katika “Receive the Holy Ghost” (Liahona, Nov. 2010, 94–97). Je utautumiaje ushauri wake?

Ona pia Mada za Injili, “Ufunuo,” Gospel Library; “Daily Bread: Pattern” (video), Gospel Library.

2 Nefi 33

Kitabu cha Mormoni kinatushawishi sisi sote tumwamini Kristo.

Katika 2 Nefi 33, wakati Nefi akihitimisha maandishi yake, alieleza kwanza kabisa ni kwa nini alikuwa anaandika. Je, ni sababu zipi unazipata katika mlango huu? Tafakari kuhusu hadithi na mafundisho ambayo umeyasoma hadi sasa katika 1 Nefi na 2 Nefi. Ni yapi yamekushawishi zaidi wewe na imani yako katika Kristo?

Ona pia “Nephi Records His Final Testimony” (video), Gospel Library.

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la Liahona na magazeti ya Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

2 Nefi 31:4–13

Ninapobatizwa, ninamfuata Yesu.

  • Kuna picha ya Yesu akiwa anabatizwa mwishoni wa muhtasari huu. Pengine watoto wako wangeweza kuitumia ili kukusimulia kile wanachokijua kuhusu tukio hili (ona pia Mathayo 3:13–17). Je, kwa nini Yesu anatutaka tubatizwe kama ilivyokuwa Kwake? Watoto wako wangeweza kusikiliza sababu wakati mnaposoma pamoja sehemu za 2 Nefi 31:4–13. Ingeweza kuwa yenye msaada kama mtu fulani ambaye amebatizwa hivi karibuni angeweza kushiriki uzoefu wake.

2 Nefi 31

Yesu Kristo alinifundisha jinsi gani ya kurudi kwa Baba wa Mbinguni.

  • Ili kuwasaidia watoto wako wapate taswira ya mafundisho katika 2 Nefi 31, wangeweza kuchora njia yenye picha ya Kristo mwishoni. Ungeweza kuwasaidia wapate au wachore picha ambazo zinawakilisha hatua kwenye njia hiyo, kama vile imani katika Kristo, toba, ubatizo, kipawa cha Roho Mtakatifu na kuvumilia hadi mwisho. Wageweza kuonesha kwenye picha wakati mkisoma 2 Nefi 31:31–20 pamoja.

2 Nefi 32:3–5

Ninaweza kusherehekea maneno ya Kristo.

  • Kufundisha kuhusu “kusherehekea” maneno ya Kristo, ungeweza kuwaomba watoto wako waigize jinsi gani wangeweza kusherehekea kwenye chakula chao pendwa. Katika 2 Nefi 32:3, Nefi alisema kipi ambacho tunapaswa kusherehekea juu yake? Ni kwa namna gani kusherehekea maneno ya Mungu ni tofauti na kuyasoma tu? Pengine watoto wako wangeigiza tofauti hiyo. Shiriki nao baraka ulizopokea pale uliposherehekea maandiko.

2 Nefi 32:8–9

Baba wa Mbinguni ananitaka nisali kila wakati.

  • Baada ya kusoma 2 Nefi 32:8–9, zungumza na watoto wako kuhusu kwa nini Shetani hataki tusali. Kwa nini Mungu anatutaka “tusali kila wakati”? Watoto wako wangeweza kutengeneza orodha au kuchora picha za hali ambapo wao wangeweza kusali. Kisha mngeweza kuimba wimbo ambao unafundisha kuhusu sala, kama vile “Je, Uliomba?Nyimbo za Dini, na. 72). Ungeweza kubadilisha baadhi ya maneno yaliyoko katika wimbo na kutumia ya kutoka kwenye orodha zao. Ni kwa namna gani Bwana anatubariki wakati tunaposali kila wakati?

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la gazeti la Rafiki.

Picha
Yohana Mbatizaji akimbatiza Yesu

Ili Kutimiza Haki Yote, na Liz Lemon Swindle

Chapisha