Njoo, Unifuate 2024
Machi 25–31: “Atafufuka … na Uponyaji katika Mabawa Yake.” Pasaka


“Machi 25–31: ‘Atafufuka … na Uponyaji katika Mabawa Yake.’ Pasaka,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2024)

“Machi 25–31. Pasaka,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2024)

Picha
Kristo aliyefufuka pamoja na Mitume Wake

Kristo na Mitume, na Del Parson

Machi 25–31: “Atafufuka … na Uponyaji katika Mabawa Yake”

Pasaka

Mitume wa kale walikuwa majasiri katika shuhuda zao juu ya Yesu Kristo na Ufufuko Wake (ona Matendo ya Mitume 4:33). Mamilioni ya watu wanaamini katika Yesu Kristo na wanajitahidi kumfuata kwa sababu ya maneno yao yaliyoandikwa katika Biblia. Bado watu wengine huenda wakajiuliza: kama Yesu Kristo ni Mwokozi wa ulimwengu wote, basi kwa nini mashahidi Wake waliomuona kwa macho ni watu wachache tu ambao walipatikana katika eneo moja dogo?

Kitabu cha Mormoni kinasimama kama nyongeza ya ushahidi, wenye kuthibitisha kwamba Yesu Kristo ndiye Mwokozi wa ulimwengu, “anayejidhihirisha kwa mataifa yote” (ukurasa wa Jina wa Kitabu cha Mormoni) na hutoa wokovu kwa wote wanaokuja Kwake. Kwa nyongeza, ushahidi huu wa pili pia unaweka wazi maana ya wokovu. Hii ndiyo sababu Nefi, Yakobo, Mormoni, na manabii wote walifanya kazi “kwa bidii kuchonga maneno haya kwenye mabamba”—ili kutangaza kwa vizazi vya siku zijazo kwamba wao pia “walijua kuhusu Kristo, na … walikuwa na tumaini la utukufu Wake” (Yakobo 4:3–4). Msimu huu wa Pasaka, tafakari kuhusu shuhuda zilizoko katika Kitabu cha Mormoni kwamba nguvu za Mwokozi ni kwa ajili ya watu wote na kwa mtu binafsi—zikiukomboa ulimwengu wote na kukukomboa wewe.

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Picha
ikoni ya seminari

Kwa sababu ya Yesu Kristo, nitafufuka.

Ni desturi wakati wa Pasaka kutafakari Ufufuko wa Yesu Kristo, lakini kufufuka ina maanisha nini hasa? Ni umaizi upi unatolewa na Kitabu cha Mormoni kuhusu ufufuko? Pengine majira haya ya Pasaka ungeweza kuorodhesha kweli kuhusu ufufuko ambazo unazipata katika 2 Nefi 9:6–15, 22; Alma 11:42–45; 40:21–25; 3 Nefi 26:4–5.

Ungeweza pia kuandika jinsi gani kweli hizi kuhusu ufufuko zinaathiri matendo yako na namna unavyoishi. Kwa mfano, fikiria jinsi ambavyo ungeweza kukamilisha sentesi hizi: Kama nisingejua mambo haya … na Kwa sababu ninajua mambo haya …

Wimbo wa dini kama “Najua Kristo Yu Hai” (Nyimbo za Dini, na. 68) ungeweza kukusaidia ufikirie kuhusu kwa nini ufufuko wa Mwokozi ni muhimu kwako. Wakati unapoimba, kusikiliza au kusoma wimbo huo, ungeweza kujiuliza, “Je maisha yangu ni tofauti jinsi gani kwa sababu Kristo Alifufuka?”

Gospel Library ina mkusanyiko wa video za Pasaka ambazo zinaweza kuwa sehemu yenye maana ya kujifunza kwako. Pengine ungeangalia moja au zaidi ya video hizi na kutafakari zinaongeza nini kwenye uelewa wako au shukrani kwa Ufufuko wa Mwokozi.

Ona pia Luka 24:36–43; Matendo ya Mitume 24:15; 1 Wakorintho 15:12–23; Reyna I. Aburto, “Kaburi Halina Ushindi,” Liahona, Mei 2021, 85–86; Mada za Injili, “Ufufuko,” Gospel Library; “Death, Grieving, and Loss” in the “Life Help” collection in Gospel Library.

Yesu Kristo alijichukulia juu Yake dhambi, maumivu na unyonge wangu.

Biblia inafundisha wazi ya kwamba Yesu Kristo alilipia dhambi zetu. Kitabu cha Mormoni, kinapanua uelewa wetu kuhusu dhabihu na mateso ya Yesu Kristo katika njia muhimu. Unaweza kupata baadhi ya mafunzo haya katika Mosia 3:7; 15:5–9; Alma 7:11–13. Baada ya kusoma vifungu hivi, zingatia kuandika kile ambacho umegundua katika chati kama hii:

Mwokozi aliteseka nini?

Kwa nini aliteseka?

Hii ina maana gani kwangu?

Hapa ni njia nyingine ya kujifunza sehemu hizi: tafuta wimbo wa dini ambao unahisi unaendana na jumbe zinazofundishwa. Fahirisi ya “maandiko” mwishoni mwa kitabu cha nyimbo za dini inaweza kusaidia. Je ni vifungu gani vya maneno kutoka nyimbo hizi za dini na maandiko vinakusaidia uwe na shukrani ya kina zaidi kwa dhabihu ya Mwokozi?

Ona pia Isaya 53; Waebrania 4:14–16; Gérald Caussé, “Shahidi Hai wa Kristo Aliye Hai,” Liahona, Mei 2020, 38–40.

Yesu Kristo anaweza kunisafisha na kunisaidia niwe mkamilifu.

Inaweza kusemwa ya kwamba Kitabu cha Mormoni ni historia ya watu ambao walibadilika kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo. Unaweza pia kusoma uzoefu huu katika Mosia 5:1–2; 27:8–28; Alma 15:3–12; 24:7–19. Ungeweza pia kufikiria juu ya kusoma mifano mingine. Je, unagundua vitu gani ambavyo vinafanana katika matukio haya? Je, ni tofauti zipi unazoziona? Je, mambo haya yanakufundisha nini kuhusu jinsi Mwokozi anavyoweza kukubadilisha?

Ona pia Alma 5:6–14; 13:11–12; 19:1–16; 22:1–26; 36:16–21; Etheri 12:27; Moroni 10:32–33.

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la Liahona na magazeti ya Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana..

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Kwa sababu Yesu Kristo alifufuka, mimi pia nitafufuka.

  • Unaweza kutumia “Sura ya 53: Yesu Anasulubiwa” na “Sura ya 54: Yesu Amefufuka” (katika Hadithi za Agano Jipya, 136–38, 139–44) kuwaambia watoto wako kuhusu Ufufuko wa Yesu Kristo. Au waruhusu watoto wako wakusimulie hadithi hii, wakitumia picha zilizoko kwenye sura hizo.

  • Matembezi ya Mwokozi Aliyefufuka katika bara la Amerika ni ushahidi wenye nguvu juu ya Ufufuko Wake. Zingatia kuwaeleza watoto wako kuhusu hilo, ukitumia 3 Nefi 1117; wimbo “Easter Hosanna”; au mstari wa mwisho wa “Book of Mormon Stories” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 68–69, 118–19). Wahimize watoto wako wafikirie jinsi ambavyo wao wangehisi kugusa makovu ya majeraha ya Mwokozi (ona 3 Nefi 11:14–15) au kuwa mmoja kati ya wale watoto aliowabariki (ona 3 Nefi 17:21). Shirikishaneni hisia zenu kuhusu Yesu Kristo na Ufufuko Wake.

  • Ili kuwasaidia watoto wako wagundue Kitabu cha Mormoni kinafundisha nini kuhusu ufufuko, ungeweza kuwaalika wafikirie kwamba hujui chochote kuhusu hilo na waombe walifafanue kwako. Wasaidie watafute katika 2 Nefi 9:10–15; Alma 11:41–45; na Alma 40:21–23 kwa ajili ya majibu ya maswali kama yafuatayo: Je, kufufuka maana yake nini? Ni nani atafufuliwa? Pia waalike watoe ushuhuda juu ya Ufufuko wa Mwokozi kama sehemu ya majibu yao.

Yesu Kristo anajua jinsi ya kunifariji.

  • Mosia 3:7 na Alma 7:11 zinaelezea baadhi ya mambo ambayo Mwokozi aliyapitia kama sehemu ya Upatanisho Wake. Ungeweza kusoma moja ya mistari hii kwa watoto wako na waombe wasikilize maneno ambayo yanawaambia kile Yesu alichokipitia. Kisha ungeweza kusoma Alma 7:12 ili kupata ni kwa nini aliteseka. Shuhudia kwamba Yesu Kristo alihisi maumivu yetu yote na magonjwa ili kwamba aweze kutufariji.

  • Je, watoto wako wanao wimbo wa dini au wa watoto wanaoupendelea kuhusu Yesu Kristo na Upatanisho Wake? Mngeweza kuuimba pamoja—au mjifunze wimbo mpya. Zungumzeni kuhusu maneno au virai katika mashairi ambavyo vinahusu faraja na amani ambayo Mwokozi Hutoa kwetu.

Picha
Kristo akisali katika Bustani ya Gethsemane

Gethsemane, na Michael T. Malm

Yesu Kristo anaweza kunifanya niwe msafi na anaweza kunisadia nibadilike.

  • Kitabu cha Mormoni hutoa mifano mingi ya watu ambao walibadilishwa kwa sababu ya Upatanisho wa Mwokozi. Pengine watoto wako wangeweza kuchagua mmojawapo ili wajifunze juu yake, kama vile Enoshi (ona Enoshi 1:2–8), Alma Mdogo (ona Mosia 27:8–24), au watu wa Anti-Nefi-Lehi ( Alma 24:7–19). Je, ni kwa namna gani watu hawa au kundi hili walibadilika kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo? Ni jinsi gani tunaweza kufuata mifano yao?

  • Wewe pamoja na watoto wako mngeweza pia kulinganisha kitu kisafi na kitu kichafu na kuzungumza jinsi vitu vichafu vinavyofanywa kuwa visafi. Someni pamoja Alma 13:11–13. Je, Yesu alifanya nini ili kwamba tuweze kusafishwa kutokana na dhambi zetu? Je, hili hutufanya tuhisi vipi kuhusu dhambi? Je, hutufanya tuhisi vipi kuhusu Mwokozi?

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la gazeti la Rafiki.

Ishi kwa kustahili mwongozo wa Roho. Roho ni mwalimu halisi. Unapotafuta mwongozo Wake na kuishi kwa ustahiki, Yeye atakupa mawazo na misukumo kuhusu jinsi gani ya kutosheleza mahitaji ya wale unaowafundisha.

Picha
Yesu akiwasalimia Wanefi

Kielelezo cha Kristo akiwa na Wanefi, na Ben Sowards

Chapisha