Njoo, Unifuate
Septemba 30–Oktoba 6: “Mimi Ndiye Sheria na Nuru.” 3 Nefi 12–16


“Septemba 30–Oktoba 6: ‘Mimi Ndiye Sheria na Nuru.’ 3 Nefi 12–16,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2023)

“Septemba 30–Oktoba 6. 3 Nefi 12–16,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2023)

Yesu akiwabainisha Mitume Kumi na Wawili

Nefi wa Tatu: Hawa Kumi na Wawili Ambao Nimewachagua, na Gary L. Kapp

Septemba 30–Oktoba 6: “Mimi Ndiye Sheria na Nuru”

3 Nefi 12–16

Kama vile wafuasi wa Yesu ambao walikusanyika kusikiliza Mahubiri ya Mlimani kule Galilaya, watu ambao walikusanyika hekaluni pale Neema walikuwa wameishi sheria ya Musa. Walikuwa wameifuata kwa sababu ilielekeza nafsi zao kwa Kristo (ona Yakobo 4:5), na sasa Kristo alisimama mbele yao, akitangaza sheria ya juu zaidi. Lakini hata wale miongoni mwetu ambao hatujawahi kuishi sheria ya Musa tunaweza kutambua kwamba kiwango ambacho Yesu aliwawekea wafuasi Wake ni cha juu zaidi. “Ningependa kwamba mngekuwa wakamilifu,” Yeye alitangaza (3 Nefi 12:48). Kama hili linakufanya uhisi umepungukiwa, kumbuka kwamba Yesu alisema, “Heri wale walio masikini rohoni, ambao wanakuja kwangu, kwani ufalme wa mbinguni ni wao” (3 Nefi 12:3). Sheria hii ya juu ni mwaliko—njia nyingine ya kusema “Njooni kwangu na muokolewe” (3 Nefi 12:20). Kama vile sheria ya Musa, sheria hii inatuelekeza kwa Kristo—Yeye Pekee anayeweza kutuokoa na kutukamilisha. “Tazama,” Yeye alisema, “Mimi Ndiye Sheria na Nuru.” Nitazameni mimi na mvumilie hadi mwisho na mtaishi”(3 Nefi 15:9).

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

3 Nefi 12–14

ikoni ya seminari
Ninaweza kuwa mfuasi wa kweli wa Yesu Kristo.

Hii ni njia moja ya kujifunza na kutumia kile Mwokozi alichofundisha katika 3 Nefi 12–14: Chagua kundi la mistari, na ona kama unaweza kufanya muhtasari wa kile ambacho mistari hiyo inafundisha katika sentensi moja inayoanza na “Wafuasi wa kweli wa Yesu Kristo …” Kwa mfano, muhtasari wa 3 Nefi 13:1-8 ungeweza kuwa “Wafuasi wa kweli wa Yesu Kristo hawatafuti sifa za umma kwa kufanya mema.” Jaribu na hivi vifungu vya maneno:

Baada ya kusoma mistari hii, ni kipi unahisi umetiwa msukumo kufanya ili kumfuata Yesu Kristo?

Amri katika 2 Nefi 12:48 inaweza kuonekana ya kuchosha sana—hata kutowezekana. Ni kipi unajifunza kutoka katika ujumbe wa Mzee Jeffrey R. Holland “Basi Ninyi Mtakuwa Wakamilifu—Hatimaye” (Liahona, Nov. 2017, 40–42) ambacho kinakusaidia uelewe maneno ya Mwokozi katika mstari huu? Kulingana na Moroni 10:32–33, ni kipi kinafanya iwezekane kuwa mkamilifu kama Mwokozi?

Ona pia Dallin H. Oaks, “Changamoto ya Kuwa,” Ensign, Nov. 2000, 32–34; Mada za Injili, “Kuwa Kama Yesu Kristo,” Maktaba ya Injili; “Bwana Kwako Naja; Nyimbo za Dini, na. 125; “Jesus Christ Teaches How to Live the Higher Law” (video), Maktaba ya Injili.

Tumia masomo ya vitendo. Mwokozi alitufundisha kweli muhimu kwa kurejelea vitu vya kawaida. Ungeweza kufanya kitu sawa na hicho unapojifunza au kufundisha kuhusu 3 Nefi 12–16. Kuangalia au kushikilia chumvi kiasi, mshumaa, au koti kungeweza kuboresha mazungumzo kuhusu kweli za milele Mwokozi alizofundisha.

3 Nefi 12:1–215:23–2416:1–6

Heri wao ambao wanaamini bila kuona.

Ni wachache kati ya watoto wa Mungu, ambao wamemuona Mwokozi na kuisikia sauti Yake, kama ilivyokuwa kwa watu wa Neema. Wengi wetu ni zaidi kama watu walioelezwa katika 3 Nefi 12:2; 15:23; na 16:4–6. Je, ni ahadi zipi zimetolewa kwa watu kama hao katika mistari hii? Ni kwa jinsi gani ahadi hizi zimetimizwa katika maisha yako?

Ona pia Yohana 20:26–29; 2 Nefi 26:12–13; Alma 32:16–18.

3 Nefi 12:21–30; 13:1–8, 16–18; 14:21–23

Ninaweza kujitahidi kutakasa matamanio ya moyo wangu.

Dhamira moja unayoweza kuigundua katika sura hizi ni mwaliko wa Mwokozi kuishi sheria ya juu—kuwa wenye haki siyo tu katika matendo yetu ya nje lakini pia katika mioyo yetu. Tafuta dhamira hii wakati Mwokozi anapozungumzia mabishano (3 Nefi 12:21–26), mmomonyoko wa maadili (3 Nefi 12:27–30), sala (3 Nefi 13:5–8) na mfungo (3 Nefi 13:16–18). Ni mifano gani mingine unayoweza kuipata? Unaweza kufanya nini ili kutakasa tamaa za moyo wako?

3 Nefi 14:7–11

Baba wa Mbinguni atanipa vitu vizuri ninapoomba, kutafuta na kubisha.

Unaposoma mwaliko wa Mwokozi katika 3 Nefi 14:7–11 wa kuomba, kutafuta, na kubisha, tafakari ni “vitu gani vizuri” Yeye angetaka uviombe. Maandiko ya ziada yafuatayo yanaweza kukusaidia uelewe jinsi ya kuomba, kutafuta na kubisha. Yanaweza pia kusaidia kufafanua kwa nini baadhi ya sala hazijibiwi kwa namna unayotarajia: Isaya 55:8–9; Helamani 10:4–5; Moroni 7:26–27, 33, 37; na Mafundisho na Maagano 9:7–9; 88:64. Ni kwa jinsi gani vifungu hivi vya maneno vinaathiri jinsi unavyoomba, kutafuta, na kubisha?

Ona pia Milton Camargo, “Omba, Tafuta na Bisha,” Liahona, Nov. 2020, 106–8.

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la Liahona na magazeti ya Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

3 Nefi 12:14–16

Ninaweza kuwa mfano mzuri kwa kumfuata Yesu.

  • Wakati mwingine watoto wanaweza wasitambue ni kwa kiasi gani mifano yao inaweza kuwabariki wengine. Tumia 3 Nefi 12:14–16 kuwatia moyo waache nuru yao iangaze. Kwa mfano, unaposoma “wewe” au “yako,” katika mistari hii, waombe watoto wako wajioneshe wao wenyewe kwa kidole. Waambie watoto kuhusu nuru unayoiona ndani yao wakati wanapomfuata Yesu Kristo na jinsi inavyokutia pia msukumo kumfuata Yeye. Mngeweza pia kuimba pamoja wimbo unaowahamasisha watoto wang’are kama nuru, kama vile “I Am like a Star” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 163).

  • Ili kuwatia moyo watoto wako wasifiche nuru yao (ona 3 Nefi 12:15), waruhusu wafanye zamu kuificha au kufunika taa au nuru nyingine. Wangeweza kuifungua nuru kila wakati wanapotaja kitu wanachofanya ili wawe mfano mzuri kwa wengine.

3 Nefi 13:19–21

“Jiwekeeni hazina mbinguni.”

  • Kusoma mistari hii kungeweza kushawishi majadiliano kuhusu vitu tunavyovithamini. Pengine ungeweza kuwaongoza watoto wako katika utafutaji wa hazina ili kupata vitu ambavyo vinawakumbusha hazina zenye thamani ya milele.

3 Nefi 14:7–11

Baba wa Mbinguni hujibu sala zangu.

  • Unaposoma 3 Nefi 14:7, watoto wako wangeweza kufanya vitendo ambavyo huwakilisha kila moja ya mialiko ya Mwokozi katika mstari huu. Kwa mfano, wangeweza kuinua mikono yao (omba), kutengeneza darubini kwa mikono yao (tafuta), au kuigiza wakibisha mlangoni (bisha). Wasaidie watoto wako wafikirie juu ya mambo wanayoweza kusema na kuomba katika sala zao.

  • Watoto wako wangeweza kufurahia mchezo ambapo wanaomba kitu na kupokea kitu tofauti kabisa. Katika 3 Nefi 14:7–11, ni kipi Mwokozi alitaka tujue kuhusu Baba yetu wa Mbinguni?

3 Nefi 14:21–27; 15:1

Mwokozi ananitaka nisikie na nitende kile Yeye anachofundisha.

  • Fikiria kuhusu njia ambazo ungeweza kuisaidia familia yako ipate taswira ya fumbo lililo katika mistari hii. Pengine wangeweza kuchora picha, kufanya matendo au kujenga vitu kwenye msingi imara na msingi wa mchanga. Wangeweza pia kuweka majina yao badala ya “mtu mwenye hekima” wanaposoma 3 Nefi 14:24–27 au kuimba “The Wise Man and the Foolish Man” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 281). Au wangeweza kusimama kila mara wanaposikia neno “fanya” katika 3 Nefi 14:21–27 na 15:1.

  • Hapa kuna somo la vitendo ambalo ungeweza kulijaribu: waombe watoto wako wafikirie kwamba mmoja wa miguu yao huwakilisha kusikia maneno ya Mwokozi na mwingine huwakilisha kufanya kile ambacho Mwokozi amefundisha. Waalike watoto wako wajaribu kusimama wima kwa mguu wao wa “kusikia” tu. Nini kingetokea kama upepo mkali utavuma kote chumbani? Kisha wewe na watoto wako mngeweza kutafuta vitu mahususi Mwokozi alivyotufundisha tufanye: ona 3 Nefi 12:3–12, 21–26; 13:5–8.

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la gazeti la Rafiki.

Yesu akiwafundisha Wanefi

Ziara ya Mwokozi kwa Watu wa Amerika, na Glen S. Hopkinson