Njoo, Unifuate
Julai 20–26. Alma 36–38: “Elekeza jicho kwa Mungu na Uishi”


“Julai 20–26. Alma 36–38: ‘Elekeza jicho kwa Mungu na Uishi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Julai 20–26. Alma 36–38,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020

Picha
mtu akisali

Kielelezo na Joshua Dennis

Julai 20–26

Alma 36–38

“Elekeza jicho kwa Mungu na Uishi”

“Utakapohisi shangwe inayotokana na kupata ufahamu wa injili, utataka kutenda kile unachojifunza” (Hubiri Injili Yangu [2004], 19). Andika mawazo na misukumo yako kuhusu jinsi ya kuzitumia kweli unazojifunza.

Andika Misukumo Yako

Wakati Alma alipoona uovu uliomzunguka, alihisi kuzidiwa sana na “huzuni,” “mateso,” na “kusononeka sana katika nafsi” (Alma 8:14). “Uovu miongoni mwa watu hawa,” alisema hivi kuwahusu Wazoramu, “unaumiza roho yangu” (Alma 31:30). Alihisi sawa na vile alivyohisi baada ya kurejea kutoka kwenye misheni yake kwa Wazoramu—alisema kuwa “mioyo ya watu ilianza kuwa migumu, na kwamba walianza kuudhika kwa sababu ya uhalisi wa neno,” na hili lilisababisha moyo wake “kuhuzunika sana” (Alma 35:15). Alma alifanya nini kuhusu yale aliyoona na kuhisi? Hakukatishwa tamaa tu au kuwa mbeuzi kuhusu hali ya ulimwengu. Badala yake, “alisababisha kwamba wana wake wakusanywe pamoja” na aliwafundisha “vitu vinavyohusiana na haki” (Alma 35:16). Aliwafundisha kwamba: “Hakuna njia nyingine yoyote au njia ambayo binadamu anaweza kuokolewa, ila tu kwa na kupitia kwa Kristo. Tazama, yeye ni neno la ukweli na haki” (Alma 38:9).

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Alma 36

Naweza kuzaliwa kwa Mungu pale ninapokuwa mnyenyekevu na ninapotubu.

Ni wachache ambao watakuwa na uzoefu wa ajabu kama vile kuongoka kwa Alma. Lakini kuna kanuni katika uzoefu wake ambazo sote tunaweza kujifunza kutokana nazo na kuzitumia, kwa sababu kila mmoja ni lazima “azaliwe kwa Mungu” (Alma 36:23). Unaposoma Alma 36, tafuta kanuni ambazo unaweza kuzitumia. Kwa mfano, ni kwa jinsi gani mtu aliyezaliwa kwa Mungu anahisi kuhusu dhambi? kuhusu Yesu Kristo? Waweza pia kutafuta mabadiliko unayoweza kutarajia kuona katika imani na vitendo vya mtu aliyezaliwa kwa Mungu.

Ona pia Mosia 5:7; 27:25–26; Alma 5:14; 22:15; Helamani 3:35; “Kuongoka,” Mada za Injili, topics.ChurchofJesusChrist.org.

Alma 36

Yesu Kristo alilipia dhambi za ulimwengu.

Unaweza kugundua marudio kiasi katika simulizi ya Alma ya kuongoka kwake katika sura hii. Hiyo ni kwa sababu Alma 36 ni mfano mkuu wa aina ya ushairi wa Kiebrania unaoitwa chiasmus, ambapo maneno au dhana vinawasilishwa kwa utaratibu fulani, na kuelekeza kwenye dhana kuu, na kisha kurudiwa kwa utaratibu wa kugeuzwa. Katika Alma 36, dhana katika mstari wa 3 inarudiwa katika mstari wa 27, dhana katika mstari wa 5 inarudiwa katika mstari wa 26, na kadhalika. Dhana kuu ni ujumbe muhimu zaidi wa chiasmus. Jaribu kama unaweza kupata dhana kuu katika mstari wa 17–18. Gundua jinsi “nilipofikiria wazo hili” kulimuathiri Alma na kubadili maisha yake. Jinsi gani ukweli huu umekuathiri wewe? Ni mawazo gani mengine yaliyorudiwa unayoyapata katika kifungu hiki?

Ni kwa jinsi gani maelezo haya ya toba na msamaha yanakutia moyo kufuata mfano wa Alma na kumgeukia Mwokozi?

Ili kupata taarifa zaidi kuhusu chiasmus, ona Kitabu cha Kiada cha Kitabu cha Mormoni cha Mwanafuzi (Kitabu cha kiada cha Mfumo wa Elimu ya Kanisa [2009], 232–33).

Alma 37

Maandiko yamehifadhiwa “kwa madhumuni ya busara.”

Je,umewahi kufikiria ni muujiza na baraka iliyoje kuwa na maandiko leo hii? Mungu “ametuamini [sisi] kwa vitu hivi, ambavyo ni vitakatatifu” (Alma 37:14). Unaposoma Alma 37, tafuta baraka zinazotokana na kuwa na maandiko. Ni kwa namna gani umepata uzoefu wa baraka hizi? Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia maandiko kusaidia “kuonyesha nguvu [za Mungu] kwa vizazi vijavyo?? (Alma 37:18).

Katika Alma 37:38–47, Alma analinganisha “neno la Kristo” na Liahona. Unapotafakari ulinganisho huu, fikiria kuhusu njia ambazo umepata uzoefu wa muujiza na nguvu ya mafundisho ya Kristo “siku hadi siku” (Alma 37:40).

Ona Pia D.Todd Christofferson, “Baraka ya Maandiko,” Ensign au Liahona, Mei 2010, 32–35.

Picha
mwanamke akisoma maandiko

Maandiko yanatufunza jinsi ya kumfuata Mungu.

Alma 37:6–7

“Kupitia kwa vitu vilivyo vidogo na rahisi vitu vikubwa hutendeka.”

Wakati mwingine tunaweza kuhisi kwamba shida zetu ni kubwa kupindukia na tatanishi kwamba suluhu lazima ziwe kubwa na tatanishi pia. Na bado muda baada ya muda, Bwana anachagua kutumia “vitu vilivyo vidogo na rahisi” (Alma 37:6) kutimiza kazi Yake na kubariki maisha ya watoto Wake. Unaposoma Alma 37: 6–7, tafakari na andika njia ambazo umeweza kuona kanuni hii ikifanya kazi maishani mwako. Je, ni nini baadhi ya vitu vilivyo vidogo na rahisi ambavyo Bwana huvitumia kubariki na kukamilisha kazi Yake?

Ona pia Alma 37:41–46; Dallin H. Oaks, “Vitu Vilivyo Vidogo na Rahisi,” Ensign au Liahona, Mei 2018, 89–92.

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mawazo.

Alma 36:5–26

Ingawaje uzoefu wa Alma ulikuwa wa ajabu, kuongoka kwake kunadhihirisha kanuni kadhaa ambazo zinatufaa sisi sote. Alika kila mwana familia achague mstari kutoka Alma 36:5–26 ambao unafundisha kuhusu “kuzaliwa kwa Mungu.” Tunajifunza nini kutoka kwenye mistari hii? Pengine wanafamilia wanaweza kushiriki jinsi ambavyo wameweza kutumia kanuni ambazo Alma ameelezea.

Alma 36:18–21, 24

Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia mistari hii kumsaidia mtu aweze kuona kwamba toba ni tukio la shangwe, sio la kuogopesha? Ni kwa jinsi gani toba yaweza kututia msukumo kushiriki injili na wengine?

Alma 37:6–7, 38–46

Ni nini baadhi ya “vitu vilivyo vidogo na rahisi” (Alma 37:6) ambavyo vinasababisha mambo makuu katika maisha yetu? Ni kwa jinsi gani neno la Kristo ni kama Liahona? Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kusaidiana kujifunza maandiko kwa bidii.

Alma 37:35

Kwa nini ni busara kujifunza kutii amri tukiwa “katika ujana [wetu]?

Alma 38:12

Je, familia yako inajua kigwe ni nini? Pengine unaweza kuwaonyesha picha ya kigwe na kuzungumza kuhusu jinsi kinavyotumika kumdhibiti mnyama. Je, inamaanisha nini “kuzuia tamaa [zetu]”? Ni kwa jinsi gani kuzuia tamaa zetu kunatusaidia “kujazwa na upendo”?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Andika misukumo. Wakati unapoandika misukumo ya kiroho, unamuonyesha Bwana kwamba unathamini mwongozo Wake, na atakubariki zaidi kwa ufunuo wa mara kwa mara. Unapojifunza, andika mawazo yako. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 1230.)

Picha
Malaika anamtokea Alma na wana wa Mosia

Malaika anamtokea Alma na wana wa Mosia, na Clark Kelley Price

Chapisha