“Oktoba 28–Novemba 3. 1 na 2 Timotheo; Tito; Filemoni: ‘Uwe Kielelezo kwao Waaminio’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)
“Novemba 28–Desemba 1. 1 na Timotheo; Tito; Filemoni,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019
Oktoba 28–Novemba 3
1 na 2 Timotheo; Tito; Filemoni
“Uwe Kielelezo kwao Waaminio”
Wakati mwingine inasaidia kuanza kujifunza kwako maandiko ukiwa na swali moja au zaidi akilini. Mualike Roho akuongoze kwenye majibu unapojifunza, na andika mwongozo wa kiungu wo wote unaopokea.
Andika Misukumo Yako
Katika nyaraka Paulo alizoandika kwa Timotheo, Tito, na Filemoni, tunapata kuona kidogo ndani ya moyo wa mtumishi wa Bwana. Tofauti na nyaraka zingine za Paulo kwa mkusanyiko wote, hizi ziliandikwa kwa watu binafsi—marafiki wa karibu wa Paulo na washirika katika kazi ya Mungu—na kuzisoma ni kama kusikiliza mazungumzo. Tunaona Paulo akiwatia moyo Timotheo na Tito, viongozi wawili wa mikusanyiko, katika huduma yao ya Kanisa. Tunamuona akimsihi rafiki yake Filemoni kumsamehe Mtakatifu mwenzake na kumchukulia kama kaka katika injili. Maneno ya Paulo hayakutulenga moja kwa moja, na hakutegemea kwamba watu wengi siku moja wangeyasoma. Bado tunapata katika nyaraka hizi ushauri na kutiwa moyo, bila kujali huduma yetu binafsi kwa Kristo.
Mawazo ya Kujifunza Maandiko Binafsi
1 na 2 Timotheo; Tito
Timotheo na Tito walikuwa kina nani?
Timotheo na Tito walitumikia pamoja na Paulo katika baadhi ya safari zake za kimisionari. Wakati wa huduma yao, walipata heshima na uaminifu kutoka kwa Paulo. Timotheo baadaye aliitwa kama kiongozi wa Kanisa huko Efeso, na Tito aliitwa kama kiongozi huko Krete. Katika nyaraka hizi, Paulo aliwapa viongozi maelekezo na kuwatia moyo kuhusiana na majukumu yao, ambayo yalijumuisha kuhubiri injili na kuwaita watu kutumikia kama maaskofu.
Ona pia Kamusi ya Biblia, “Nyaraka za Paulo,” “Timotheo,” “Tito.”
Kama mimi ni “kielelezo kwao waaminio,” ninaweza kuwaongoza wengine kwa Mwokozi na injili Yake.
Timotheo alikuwa bado kijana, lakini Paulo alijua kwamba angekuwa kiongozi mzuri wa Kanisa bila kujali ujana wake. Je, ni ushauri gani Paulo alimpa Timotheo katika 1 Timotheo 4:10–16? Je, ni kwa jinsi gani ushauri huu unaweza kukusaidia wewe kuwaongoza wengine kwenda kwa Mwokozi na injili Yake?
Ona pia Alma 5:1117
“Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.”
2 Timotheo inaaminika kuwa ni waraka wa mwisho ulioandikwa na Paulo, na inaonekana kwamba alijua muda wake duniani ulikuwa mfupi (ona 2 Timotheo 4:6–8). Unaposoma waraka huu, fikiria jinsi ambavyo Timotheo alijisikia kwa kujua kwamba punde asingekuwa na mshauri na kiongozi huyu aliyemwamini. Je, Paulo alisema nini ili kumtia moyo? Je, maneno ya Paulo hukufundisha nini wewe kuhusu kukabiliana na changamoto zako mwenyewe na woga?
Kuishi injili kunaleta usalama dhidi ya hatari za kiroho za siku za mwisho.
Tunaishi katika “siku za mwisho” ambazo Paulo aliziongelea, na “nyakati za hatari” zimekuja (2 Timotheo 3:1). Unaposoma 2 Timotheo 3, andika hatari za siku za mwisho ambazo zimetajwa (ona pia 1 Timotheo 4:1–3):
Unaweza kufikiria mifano ya hatari hizi katika ulimwengu unaokuzunguka—au katika maisha yako mwenyewe? Je, ni kwa jinsi gani hatari hizi, kama watu walioelezewa katika mstari wa 6, “huinyemelea [nyumba yako], na kukufanya [wewe] mateka”? Je, ni ushauri gani unapata katika 2 Timothy 3, na pengine popote katika nyaraka hizi, ambao utakuweka wewe na familia yako salama dhidi ya hatari hizi za kiroho? (Ona, kwa mfano, 1 Timotheo 1:3–11; 2 Timotheo 2:15–16; Tito 2:1–8).
Filemoni alikuwa nani?
Filemoni alikuwa Mkristo ambaye alikuwa ameongoka. Alimiliki mtumwa aliyeitwa Onesimo, ambaye alitoroka utumwani, akakutana na Paulo, na kuongoka katika injili pia. Katika barua kwa Filemoni, Paulo alimsihi rafiki yake kumsamehe Onesimo na kumpokea “si kama mtumwa, bali zaidi ya mtumwa, ndugu mpendwa” (mstari wa 16).
Wafuasi wa Kristo husameheana.
Umewahi kuwa katika hali ambayo mtu alitafuta msamaha wako? Fikiria kuhusu hali hiyo unaposoma waraka kwa Filemoni. Je, Paulo alimfundisha nini Filemoni kuhusu kwa nini amsamehe Onesimo? Je, kuna ujumbe wo wote kwa ajili yako katika waraka huu?
Ona pia 1 Nefi 7:16–21; Mosia 26:30–31; Mada za Injili, “Msamaha,” topics.lds.org.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani.
Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Hapa kuna baadhi ya mapendekezo:
Wakati vipengele vya ushauri wa Paulo kwa wanawake kuvaa mavazi ya kujisitiri havihusiki katika kipindi chetu, wote tunaweza kujifunza kutokana na ushauri wake wa “kujipamba [wenyewe] … kwa matendo mema.” Familia yako inaweza kufurahia kuandaa maonyesho ya mavazi, wanafamilia wakiwa wamevalia mavazi au mapambo yaliyobandikwa nembo za aina tofauti za matendo mema. Je, ni yapi baadhi ya matendo mema ambayo familia yako inaweza kufanya wiki hii?
Kuwasaidia wanafamilia yako kutamani kuwa “kielelezo kwao waaminio,” fikiria kuwaalika kuchora picha za jinsi ambavyo watu wamekuwa vielelezo bora kwao. Ni kwa jinsi gani watu hawa wametushawishi kumfuata Yesu Kristo? Ujumbe wa Rais Thomas S. Monson, “Kuwa Mfano na Nuru” (Ensign au Liahona, Nov. 2015, 86–88) unaweza kutoa baadhi ya mawazo.
Je, kwa nini unafikiri “kupenda fedha” kunafikiriwa kuwa “shina la mabaya ya kila namna”? Hatari za kuzingatia maisha yetu kwenye pesa ni zipi? Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuridhika na baraka tulizo nazo?
Kulingana na mistari hii, ni baraka zipi huja kwa wale wote wanaojua na kujifunza maandiko? Pengine wanafamilia wanaweza kuelezea maandiko waliyoona kuwa hasa “yanafaa.”
Je, Paulo alikuwa tayari kufanya nini kwa ajili ya Onesimo? Je, ni kwa jinsi gani hii inafanana na kile ambacho Mwokozi alikifanya kwa hiyari kwa ajili yetu? (Ona pia 1 Timotheo 2:5–6; M&M 45:3–5). Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata mfano wa Paulo na Mwokozi?
Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.