Njoo, Unifuate
Novemba 11–17. Waebrania 7–13: ‘Kuhani Mkuu wa Mambo Mema Yatakayokuwapo’


“Novemba 11–17. Waebrania 7–13: ‘Kuhani Mkuu wa Mambo Mema Yatakayokuwapo’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)

“Novemba 11–17. Waebrania 7–13,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

Picha
Melkizedeki akimbariki Abramu

Melkizedeki akimbariki Abramu, na Walter Rane

Novemba 11–17.

Waebrania 7–13

“Kuhani Mkuu wa Mambo Mema Yatakayokuwapo”

Unaposoma Waebrania 7–13, unaweza kupokea misukumo kupitia Roho Mtakatifu. Fikiria njia unazoweza kuyaandika; kwa mfano, unaweza kuiandika ndani ya muhtasari huu, kwenye nafasi ya pembeni ya maandiko yako, au Gospel Library app.

Andika Misukumo Yako

Hata Watakatifu waaminifu kuna wakati wanapata “shutma na mateso” ambayo yanaweza kutikisa kujiamini kwao (ona Waebrania 10:32–38). Paulo alijua kwamba waongofu wa Kiyahudi kwenye Ukristo walikuwa wakipitia mateso makali kwa sababu ya imani yao mpya. Kuwatia moyo kubaki wakweli kwenye shuhuda zao, aliwakumbusha juu ya utamaduni wa muda mrefu wa wafuasi waaminifu kutoka katika historia yao wenyewe: Abili, Henoko, Nuhu, Ibrahimu, Sara, Yusufu, Musa—”wingu kubwa la mashahidi” kwamba ahadi za Mungu ni za kweli na zinastahili kusubiriwa (Waebrania 12:1). Urithi huu wa imani unashirikiwa na wote wale wanaomtazamia “ Yesu [kama] mwanzilishi na mtimizaji wa imani yetu” (Waebrania 12:2). Kwa sababu Yake, wakati wowote adui anapotufanya “tusite-site,” sisi badala yake tunaweza “kukaribia kwa moyo wa kweli katika hakikisho timilifu la imani”(Waebrania 10:22, 38). Kwetu sisi, kama vile kwa Watakatifu wa kale, Yesu Kristo ni “kuhani wetu mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo” (Waebrania 9:11).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Binafsi

Waebrania 7:1–22

Ukuhani wa Melkizedeki ni ukuhani wa juu zaidi.

Kwa karne nyingi, Wayahudi walikuwa wakitumia Ukuhani wa Lawi, ambao huijulikana pia kama Ukuhani wa Haruni. Lakini kwa utimilifu wa injili ya Yesu Kristo ulikuja Ukuhani mkuu wa Melkizedeki, ambao ulitoa baraka kubwa zaidi. Je, unajifunza nini kuhusu Ukuhani wa Melkizedeki kutoka Waebrania 7? Hapa kuna baadhi ya mifano ya kweli unazoweza kuzipata:

Tafsiri ya Joseph Smith, Waebrania 7:3, 21:Na wale wote wanaotawazwa katika Ukuhani wa Melkizedeki “hufanywa kama vile kwa Mwana wa Mungu, nao nia “[makuhani] milele.”

Waebrania 7:1: Ukuhani wa Lawi hauleti “ukamilifu” na hivyo Ukuhani wa Melkizedeki ulichukua nafasi yake (ona M&M 84:18–22).

Waebrania 7:20–21:Ukuhani wa Melkizedeki hupokelewa kwa kiapo (ona M&M 84:19–44).

Ni baraka gani umepokea kutoka kwa Ukuhani wa Melkizedeki na ibada zake zinazoendana nao?

Ona pia Alma 13:1–13; Mafundisho na Maagano 121:36–46; Mada za Injili, “Ukuhani wa Melkizedeki,” topics.lds.org; Mwongozo wa Maandiko, “Melkizedeki,” scriptures.lds.org; Henry B. Eyring, “Imani na Kiapo na Agano la Ukuhani,” Ensign au Liahona, Mei 2008, 61–64; Dallin H. Oaks, “Funguo na Mamlaka ya Ukuhani,” Ensign au Liahona, Mei 2014, 49–52.

Waebrania 9:1–10:22

Ibada za kale na za sasa huelekeza kwa Yesu Kristo.

Wasomaji wa asili wa Kiebrania wa waraka huu wangeweza kuwa na ufahamu wa maskani ya kale na ibada ambazo Paulo alizoelezea. Lakini baadhi hawakutambua kikamilifu kwamba lengo la ibada hizi lilikuwa ni kuelekeza kwenye dhabihu ya Yesu Kristo ya upatanisho.

Katika nyakati za biblia, katika sikukuu ya kila mwaka iliyoitwa Siku ya Upatanisho, kuhani mkuu aliingia mahali patakatifu (au Patakatifu pa Patakatifu) ndani ya hekalu la Yerusalemu na kutoa dhabihu ya mbuzi au kondoo kulipia dhambi za Israeli. Paulo alielezea kwamba Yesu Kristo ni kuhani mkuu ambaye hutoa dhabihu ya mara moja—maisha Yake mwenyewe—ili kulipia dhambi za ulimwengu (ona Waebrania 9:24–10:14).

Fikiria kuhusu ibada ambazo wewe unashiriki leo. Je, ni kwa jinsi gani ibada hizi hukuelekeza kwa Yesu Kristo?

Kujifunza zaidi kuhusu sherehe za Wayahudi wa kale na ishara zake, angalia filamu “Maskani” na “Dhabihu na Sakramenti” (LDS.org).

Waebrania 11

Imani huhitaji kutegemea katika ahadi za Mungu.

Kama mtu angekutaka kuelezea maana ya imani, ungesema nini? Dada Anne C. Pingree, aliyekuwa katika Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama, alivuta lugha kutoka Waebrania 11 ili kutoa maana hii: “Imani, ni uwezo wa kiroho wa kushawishika juu ya baraka ambazo huonekana ‘kutokea mbali’ lakini ambazo haziwezi kupatikana katika maisha haya, ni kipimo cha uhakika cha wale wanaoamini kweli” (“Kuona Ahadi kutokea Mbali,” Ensign au Liahona, Nov. 2003, 14).

Fikiria kutengeneza maana yako mwenyewe ya imani unapotafakari mawazo yaliyomo katika Waebrania 11. Je, mifano ya watu waliotajwa katika sura hii hukufundisha nini kuhusu imani? (Ona pia Etheri 12:6–22.)

Ona pia Alma 32:21, 26–43; Jeffrey R. Holland, “Kuhani Mkuu wa Mambo Mema Yatakayokuwapo,” Ensign, Nov. 1999, 36–38; Mada za Injili, “Imani katika Yesu Kristo,” topics.lds.org.

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia.

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani.

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Hapa kuna baadhi ya mapendekezo:

Waebrania 10:32–36

Unaweza kuwaalika wanafamilia kuelezea uzoefu wa kiroho wakati walipohisi “kuangazwa” na kweli. Je, ni jinsi gani uzoefu huu hutusadia “kutotupilia mbali kujiamini [kwetu]” katika nyakati za majaribu na shaka?

Waebrania 11

Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia wanafamilia kujifunza kutoka kwenye mifano ya uaminifu iliyotajwa katika Waebrania 11? Inaweza kuwa ya kufurahisha kuigiza hadithi za mifano hii. Au pengine familia yako inaweza kujadili mifano ya watu wengine waaminifu mnaowajua—ikijumuisha mababu, viongozi wa Kanisa, na watu wa jumuiya yako.

Waebrania 12:2

Kulingana na mstari huu, kwa nini Yesu alikuwa tayari kuvumilia maumivu na mateso ya msalaba? Hii inatufundisha nini kuhusu jinsi tunavyoweza kuvumilia majaribu yetu? Rais Russell M. Nelson alitoa utambuzi wa msaada kwenye mstari huu katika ujumbe wake “Furaha na Kuendelea Kuishi Kiroho” (Ensign au Liahona, Nov. 2016, 81–84).

Waebrania 12:5–11

Je, ni kwa nini Bwana huturudi na kutusahihisha? Je, wanafamilia wanagundua nini kuhusu jinsi Bwana anavyoona kuadabisha mnaposoma mistari hii pamoja? Je, ni kwa jinsi gani mistari hii huathiri jinsi unavyotoa au kupokea adabisho?

Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia muziki ili umwalike Roho Mtakatifu na kujifunza mafundisho. Urais wa Kwanza umesema, “Muziki unazo nguvu zisizo na kipimo katika kutusogeza [sisi] kuelekea kuwa watu wa kiroho zaidi” (“Dibaji ya Urais wa Kwanza,” Nyimbo za Kanisa, x). Pengine wimbo kuhusu imani, kama vile “Kweli katika Imani” (wimbo, no. 254), unaweza kuongezea kwenye mjadala wa familia kutoka Waebrania 11.

Picha
Mfano wa Yerusalemu ya kale

Ishara ya hekalu la kale na ibada zake zilifundisha kuhusu kazi ya Yesu Kristo.

Chapisha