Njoo, Unifuate
Novemba 18–24. Yakobo: ‘Iweni Watendaji wa Neno, wala Si Wasikiaji Tu’


“Novemba 18–24. Yakobo: ‘Iweni Watendaji wa Neno, wala Si Wasikiaji Tu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)

“Novemba 18–24. Yakobo,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

Picha
Ibrahimu akiomba nje ya hema lake

Ibrahimu katika Msitu wa Mamre, na Grant Romney Clawson

Novemba 18–24.

Yakobo

Yakobo: “Iweni Watendaji wa Neno, wala Si Wasikiaji Tu”

Unaposoma Waraka wa Yakobo, tilia maanani virai vinavyojitokeza kwako, na uviandike. Je, ni kwa jinsi gani unashawishika kuishi kweli hizi?

Andika Misukumo Yako

Wakati mwingine mstari mmoja tu wa maandiko unaweza kubadilisha ulimwengu. Yakobo 1:5 huonekana kama sehemu ndogo rahisi ya ushauri—ukihitaji hekima, omba dua kwa Mungu. Lakini wakati Joseph Smith wa miaka-14 aliposoma mstari huo, “ulionekana kuingia kwa nguvu kubwa katika kila hisia ya moyo [wake]” (Joseph Smith—Historia ya 1:12). Hivyo kwa mwongozo wa kiungu, Joseph alifanyia kazi ushauri wa Yakobo na kutafuta hekima kutoka kwa Mungu kupitia sala. Na Mungu kwa hakika alitoa kwa ukarimu, akimpa Joseph moja ya matembezi ya kimbingu ya kusifika katika historia ya mwanadamu—Ono la Kwanza. Ono hili lilibadilisha mwenendo wa maisha ya Joseph na kuongoza Urejesho wa Kanisa la Yesu Kristo duniani. Sisi wote tumebarikiwa leo kwa sababu Joseph Smith alisoma na kufanyia kazi Yakobo 1:5.

Je, utapata nini unapojifunza Waraka wa Yakobo? Pengine mstari mmoja au miwili itakubadilisha au kumbadilisha mtu unayempenda. Unaweza kupata muongozo unapotafuta kutimiza misheni yako katika maisha. Unaweza kupata kutiwa moyo kuongea kwa ukarimu au kuwa mvumilivu zaidi. Chochote kinachokushawishi, acha maneno haya “yaingie … katika kila hisia ya moyo [wako].” Kumbuka “kupokea kwa upole … neno,” kama Yakobo alivyoandika, “liwezalo kuziokoa roho zenu” (Yakobo 1:21).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Binafsi

Yakobo

Yakobo alikuwa nani?

Kwa ujumla inaaminika kwamba mwandishi wa Waraka wa Yakobo alikuwa mwanawe Mariamu, mama wa Yesu Kristo, kwa hivyo huyu ni kaka wa kambo wa Mwokozi. Yakobo ametajwa katika Mathayo 13:55; Marko 6:3; Matendo 12:17; 15:13; 21:18; na Wagalatia 1:19; 2:9. Inaonekana kutoka katika maandiko haya kwamba Yakobo alikuwa kiongozi wa Kanisa katika Yerusalemu na alikuwa ameitwa kama Mtume (ona Wagalatia 1:19).

Yakobo 1:2–4; 5:7–11

Kustahimili katika uvumilivu hutuongoza kwenye ukamilifu.

“Kusubiri inaweza kuwa vigumu,” Rais Dieter F. Uchtdorf alifundisha. “Tunataka tunachotaka, na tunakitaka sasa. Kwa hivyo, wazo hasa la uvumilivu laweza kuonekana lisilopendeza” (“Endeleeni katika Uvumilivu,” Ensign au Liahona, Mei 2010, 56). Baada ya kusoma Yakobo 1:2–4; 5:7–11, je unaweza kusema ujumbe mkuu wa Yakobo kuhusu uvumilivu ulikuwa nini? Ni utambuzi upi wa ziada ulionao baada ya kusoma ujumbe uliosalia wa Rais Uchtdorf? Je, ni kwa jinsi gani unaweza kumuonyesha Bwana kwamba uko radhi kuwa mvumilivu?

Yakobo 1:3–8, 21–25; 2:14–26; 4:17

Imani huhitaji matendo.

Je, unajuaje kama una imani katika Yesu Kristo? Je, ni kwa jinsi gani matendo yako huonyesha imani yako kwa Mungu? Fikiria kuhusu maswali haya unapojifunza mafundisho ya Yakobo kuhusu imani. Inaweza kuwa ya kuvutia pia kusoma kuhusu Ibrahimu na Rahabu, mifano miwili iliyotajwa na Yakobo (ona Mwanzo 22:1–12; Yoshua 2). Je, ni kwa jinsi gani wao walionyesha kwamba walikuwa na imani katika Mungu?

Kusoma Yakobo 1:3–8, 21–25; 2:14–26; 4:17 kunaweza kukusaidia kufikiria njia za kuweza kuwa mtendaji mzuri wa neno. Andika misukumo yo yote unayopokea, na uweke mipango ya kuyafanyia kazi.

Ona pia Alma 34:27–29; 3 Nefi 27:21.

Yakobo 1:263:1–18

Maneno ninayoongea yana nguvu ya kuwaumiza au kuwabariki wengine.

Miongoni mwa matumizi mengi ya tamathali za semi Yakobo alizotumia kote katika waraka wake, baadhi ya lugha yake dhahiri kabisa inapatikana katika ushauri wake kuhusu lugha. Fikiria kutengeneza orodha ya njia zote Yakobo alizoelezea ulimi na mdomo. Je, ni nini kila linganisho au picha hupendekeza kuhusu maneno tunayoongea? Fikiria juu ya kitu unachoweza kufanya ili kumbariki mtu kwa maneno yako (ona M&M 108:7).

Yakobo 2:1–9.

Kama mfuasi wa Yesu Kristo, ninapaswa kuwapenda watu wote, bila kujali hali zao.

Yakobo aliwaonya Watakatifu hususani dhidi ya kuwapendelea matajiri na kuwadharau maskini, lakini onyo lake linaweza kutumika kwa upendeleo wo wote au chuki tunayoweza kuwa nayo kwa wengine. Inaweza kuwa vigumu kupangilia upya njia ambazo kwazo kwa njia hasi tunawahukumu wengine, lakini Bwana ameahidi kwamba Yeye atatusaidia kuona wapi tunahitaji kufanya vizuri zaidi (ona Etheri 12:27). Kwa sala unapojifunza Yakobo 2:1–9, jichunguze mwenyewe moyoni mwako na sikiliza ushawishi wa Roho Mtakatifu. Unahisi mabadiliko yoyote unayohitaji kufanya juu ya jinsi unavyowachukulia wengine au kuwafikiria wengine?

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia.

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani.

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Hapa kuna baadhi ya mapendekezo:

Yakobo1:5

Fikiria kusoma Yakobo 1:5 na kumualika mwanafamilia kufupisha maelezo ya ono la kwanza (ona Joseph Smith—Historia ya 1:8–13 au filamu “Mwombe Mungu: Ono la Kwanza la Joseph Smith” kwenye LDS.org). Waalike wanafamilia kutoa shuhuda zao juu ya Nabii Joseph Smith na uzoefu ambapo Baba wa Mbinguni alijibu sala zao.

Yakobo 1:26–27

Fikiria kuangalia filamu “Ukristo wa Kweli” (LDS.org) katika uwiano na mistari hii. Kisha soma maana ya Yakobo ya dini safi na jadili njia ambazo familia yako inaweza kufanya utekelezaji wa dini yako safi zaidi.

Yakobo 3

Yakobo 3 hujumuisha taswira nyingi ambazo zinaweza kushawishi somo la vitendo la kukumbukwa ili kuisaidia familia yako kukumbuka kuongea kwa ukarimu. Kwa mfano, unaweza kujadili jinsi cheche ndogo au njiti ya kiberiti inavyoweza kuanzisha moto mkubwa, na wanafamilia wanaweza kufikiria nyakati ambapo neno lisilo la ukarimu lilisababisha tatizo (ona mistari 5–6). Au unaweza kuandaa kitu kichachu au kichungu katika kitu ambacho kwa kawaida hutumika kwa chakula kitamu—kama vile juisi ya limao ndani ya chupa ya asali. Hii inaweza kuwapeleka kwenye mjadala kuhusu kuhakikisha kwamba maneno yetu ni mazuri na yenye kuinua (ona mistari 9–14).

Yakobo 4:5–8

Kwa nini “tusogee karibu na Mungu” tunapokabiliwa na majaribu?

Yakobo 5:14–16

Pengine kusimulia uzoefu binafsi kuhusu kupokea baraka ya ukuhani kunaweza kuwatia moyo wanafamilia “kuomba baraka ya ukuhani wakati wanapokuwa katika hitaji la nguvu ya kiroho” (Dallin H. Oaks, “Umuhimu wa Baraka za Ukuhani,” New Era, Julai 2012, 4).

Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Fanyia kazi kile unachojifunza. Unapojifunza, sikiliza ushawishi kutoka kwa Roho kuhusu jinsi unavyoweza kutumia kile unachojifunza kwenye maisha yako. Jiwekee ahadi kufuata ushawishi huo na kuishi injili kikamilifu zaidi. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 35.)

Picha
Joseph Smith mdogo akisoma maandiko nje ya nyumba yao

Na Aombe Dua kwa Mungu, na John McNaughton

Chapisha