Agano Jipya 2023
Desemba 25–31. Ufunuo 15–22: “Yeye Ashindaye Atayarithi Haya”


“Desemba 25–31. Ufunuo 15–22: ‘Yeye Ashindaye Atayarithi Haya’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya (2023)

“Desemba 25–31. Ufunuo 15–22,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2023

Yesu Kristo akiwasalimia watu katika Ujio Wake wa Pili

Jiji la Milele, na Keith Larson

Desemba 25–31

Ufunuo 15–22

“Yeye Ashindaye Atayarithi Haya”

Wakati mwingine kikwazo kikubwa cha kujifunza ni dhana yetu kwamba hatuhitaji kujifunza—kwamba tayari tunajua. Unaposoma maandiko, kuwa wazi kwa ajili ya umaizi mpya ambao Bwana anataka kukupatia.

Andika Misukumo Yako

Kama unavyoweza kukumbuka, kitabu cha Ufunuo kinaanza na Mwokozi akijitangaza Mwenyewe kuwa ni “mwanzo na mwisho” (Ufunuo 1:8). Vyema ya kutosha, huishia na maneno hayo hayo: “Mimi ni … mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho” (Ufunuo 22:13). Lakini hilo linamaanisha nini? Mwanzo na mwisho wa nini? Kitabu cha Ufunuo kwa nguvu hushuhudia kwamba Yesu Kristo ndiye mwanzo na mwisho wa kila kitu—wa ukuu, wa mkanganyiko mkubwa uliopo wa uwepo wa mwanadamu na wokovu. Yeye ni “Mwanakondoo aliyechinjwa tangu msingi wa dunia (Ufunuo 13:8). Na Yeye ni Mfalme wa wafalme ambaye huleta mwisho wa uovu, huzuni, na hata kifo chenyewe na kuanzisha “mbingu mpya na nchi mpya” (Ufunuo 21:1).

Hali kabla ya hii mbingu mpya na nchi mpya kufika, kuna mengi kwa ajili yetu kuyashinda: mapigo, vita, uovu uliokithiri—yote ambayo Ufunuo unaelezea wazi wazi. Lakini Yesu Kristo yu pamoja nasi katika sehemu hii pia. Yeye ndiye “nyota yenye kung’aa asubuhi” ambayo hung’aa katika anga la kiza kama ahadi kwamba machweo yatakuja punde (Ufunuo 22:16). Na yanakuja punde. Yeye yuaja. Hata kama vile Yeye anavyotualika, “Njooni kwangu” (Mathayo 11:28), Yeye pia yuaja kwetu. “Naja upesi,” Yeye anatangaza. Na kwa tumaini na imani ambayo inatusafisha katika moyo wa dhiki ya siku za mwisho, sisi tunajibu, “Na uje, Bwana Yesu” (Ufunuo 22:20).

ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Ufunuo 16–18; 21– 22

Bwana hunialika kuikimbia Babeli na kuurithi “mji mtakatifu.”

Baada ya kushuhudia maangamizo na vurugu za siku za mwisho, Yohana aliona siku yetu ambayo inaweza kusemekana katika tamko la Bwana “Tazama, nayafanya yote kuwa mapya” (Ufunuo 21:5). Njia moja ya kuelewa hilo humaanisha nini ni kutofautisha maelezo ya Yohana ya Babeli, ishara ya ulimwengu na uovu (ona Ufunuo 16:18), na maelezo ya Yerusalemu mpya, ishara ya utukufu wa selestia katika uwepo wa Mungu (ona Ufunuo 21:22). Chati hapo chini ingeweza kukusaidia:

Babeli

Yerusalemu Mpya

Babeli

Ufunuo 16:3–6

Yerusalemu Mpya

Ufunuo 21:6; 22:1–2, 17

Babeli

Ufunuo 16:10; 18:23

Yerusalemu Mpya

Ufunuo 21:23–24; 22:5

Babeli

Ufunuo 17:1–5

Yerusalemu Mpya

Ufunuo 21:2

Babeli

Ufunuo 18:11, 15

Yerusalemu Mpya

Ufunuo 21:4

Babeli

Ufunuo 18:12–14

Yerusalemu Mpya

Ufunuo 21:18–21; 22:1-2

Ni tofauti gani nyingine unazoziona?

Ungeweza pia kutafakari kile inachomaanisha kuwa “tokeni kwake” Babeli (Ufunuo 18: 4). Unapata nini katika Ufunuo 21:22 ambacho kinavutia wewe kufanya hivyo?

Yesu na watu katika nuru mkono Wake wa kulia na watu gizani mkono wake wa kushoto.

Hukumu ya Mwisho, na John Scott

Ufunuo 20:20–15; 21:1–4

Watoto wote wa Mungu watahukumiwa kutoka katika kitabu cha uzima.

Chukulia kwamba mwandishi amejitolea kuandika kitabu kuhusu maisha yako wewe. Ni maelezo gani au matukio gani ungetaka yajumuishwe? Kama ungejua kwamba matendo yako ya baadaye yangeandikwa pia, jinsi gani ungeyakabili maisha yako kwa namna tofauti? Fikiria kuhusu hili unaposoma Ufunuo 20:21–15. Nini unatumaini kitaandikwa kuhusu wewe katika kitabu cha uzima? Ni kwa jinsi gani ungeelezea nafasi ya Mwokozi katika kitabu chako cha uzima? Katika maoni yako, kwa nini ni muhimu kwamba kinaitwa “kitabu cha uzima cha Mwanakondoo”? (Ufunuo 21:27).

Kama wazo la kusimama mbele za Mungu kuhukumiwa halileti faraja kwako, fikira kusoma Ufunuo 21:1–4. Akirejelea mistari hii, Mzee Dieter F. Uchtdorf alisema:

“Siku ile ya Hukumu itakuwa siku ya rehema na upendo—siku ambayo mioyo iliyovunjika inaponywa, wakati machozi ya huzuni yanabadilishwa na kuwa machozi ya shukrani, wakati vyote vitafanywa sawa. Ndiyo, kutakuwa na huzuni kubwa kwa sababu ya dhambi. Ndiyo, kutakuwa na majuto na hata uchungu moyoni kwa sababu ya makosa yetu, ujinga wetu, na ukaidi wetu ambao ulitusababishia kukosa nafasi ya maisha makuu ya baadae.

“Lakini nina imani kwamba hatutatosheka tu na hukumu ya Mungu; pia tutastaajabishwa na kuzidiwa na hisani Yake isiyo na mwisho, huruma ukarimu na upendo kwetu sisi, watoto Wake” (“Ee Jinsi Gani Ulivyo Mkuu Mpango wa Mungu Wetu!,” Liahona, Nov. 2016, 21).

Ni kwa jinsi gani kweli hizi zinagusa jinsi unavyoitazama Hukumu ya Mwisho? Je, ni nini kweli hizi zinakushawishi wewe kubadilisha katika maisha yako?

Ona pia Kamusi ya Biblia, “Kitabu cha uzima.”

Ufunuo 22:18–19

Je, mistari hii inamaanisha kwamba hakuwezi kuwepo maandiko yoyote ya ziada tofauti na Biblia?

Baadhi ya watu wamedondoa Ufunuo 22:18–19 kama sababu ya kukataa Kitabu cha Mormoni na maandiko mengine ya siku za mwisho. Unaweza pia kupata majibu ya pingamizi hili katika ujumbe wa Mzee Jeffrey R. Holland “Maneno Yangu … Kamwe Hayatakoma” (Liahona, Mei 2008, 91–94).

ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Ufunuo 15:2–4.Familia yako inapojadili mistari hii, ambayo inarejelea “wimbo wa Musa” na “wimbo wa Mwanakondoo,” mngeweza kusoma wimbo wa Musa katika Kutoka 15:1–19, pamoja na wimbo mwingine uliotajwa katika maandiko, kama vile Mafundisho na Maagano 84:98–102. Kwa nini yawezekana wale wanaopata “ushindi dhidi ya yule mnyama” (Ufunuo 15:2) wanajisikia kuimba nyimbo kama hizi? Pengine familia yako ingeweza kuimba pamoja wimbo wa dini au wimbo wa watoto wa sifa.

Ufunuo 19:7–9.Pengine ungeweza kuangalia picha za harusi kutoka katika historia ya familia yako au kuzungumza kuhusu wakati familia yako ilipohudhuria sherehe za harusi. Kwa nini ndoa ni mfananisho mzuri kwa ajili ya agano la Bwana na Kanisa Lake? (Ona pia Mathayo 22:1–14.)

Ufunuo 20:2–3.Je, ni kwa jinsi gani 1 Nefi 22:26 hutusaidia kuelewa kile inachoweza kumaanisha kwa Shetani “kufungwa”?

Ufunuo 22:1–4.Je, inamaanisha nini jina la Mwokozi kuwa “katika nyuso zetu”? (Ufunuo 22:4; ona pia Kutoka 28:36–38; Mosia 5:7–9; Alma 5:14; Moroni 4:3; Mafunisho na Maagano 109:22; David A. Bednar, “Kwa Heshima Kuwa na Jina na Msimamo,” Liahona, Mei 2009, 97–100).

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa “When He Comes Again,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 82–83.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Fuatilia mialiko ya kutenda. “Wakati unapofuatilia mwaliko wa kutenda, wewe unawaonyesha [wanafamilia yako] kwamba unawajali na jinsi gani injili inabariki maisha yao. Unawapa pia fursa kushiriki uzoefu wao” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi35).

Yesu Kristo akishuka na farasi kutoka mbinguni katika Ujio Wake wa Pili

Kristo katika vazi jekundu ameketi juu ya farasi mweupe.