Agano Jipya 2023
Uongofu Ndiyo Lengo Letu


”Uongofu Ndiyo Lengo Letu,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023 (2022)

“Uongofu Ndiyo Lengo Letu,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2023

Picha
mwanamke akisoma maandiko

Uongofu Ndiyo Lengo Letu

Dhumuni la kujifunza na kufundisha injili ni kuongeza uongofu wetu kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo na kutusaidia sisi kuwa zaidi kama Wao. Kwa sababu hii, tunapojifunza injili, hatutafuti tu taarifa mpya; tunataka kuwa “kiumbe kipya” (2 Wakorintho 5:17). Hii inamaanisha kuwategemea Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo ili watusaidie kubadili mioyo yetu, mitizamo yetu, matendo yetu, na asili yetu hasa.

Lakini aina ya kujifunza injili inayoimarisha imani yetu na kutuongoza kwenye badiliko la kimiujiza la uongofu haitokei yote kwa wakati mmoja. Inakwenda zaidi ya darasani mpaka ndani ya mioyo yetu na majumbani mwetu. Inahitaji jitihada endelevu, za kila siku ili kuelewa na kuishi injili. Kujifunza injili ambako kunatuongoza kwenye uongofu wa kweli kunahitaji ushawishi wa Roho Mtakatifu.

Roho Mtakatifu hutuongoza kwenye ukweli na hushuhudia juu ya ukweli huo (ona Yohana 16:13). Yeye huangaza akili zetu, anahuisha uelewa wetu, na hugusa mioyo yetu kwa ufunuo kutoka kwa Mungu, aliye chanzo cha ukweli wote. Roho Mtakatifu huitakasa mioyo yetu. Yeye huchochea ndani yetu hamu ya kuishi katika kweli, na hutunong’onezea njia za kufanya hili. Kwa kweli, “Roho Mtakatifu … atatufundisha [sisi] mambo yote” (Yohana 14:26).

Kwa sababu hizi, katika juhudi zetu za kuishi, kujifunza, na kufundisha injili, tunapaswa kwanza na zaidi ya yote tutafute wenzi wa Roho. Lengo hili linapaswa kutawala chaguzi zetu na kuongoza mawazo na matendo yetu. Tunapaswa kutafuta chochote kinachokaribisha ushawishi wa Roho na kukataa chochote kinachofukuzia mbali ushawishi huo—kwani tunajua kwamba kama tunaweza kuwa wenye kustahili uwepo wa Roho Mtakatifu, tunaweza pia kustahili kuishi katika uwepo wa Baba wa Mbinguni na Mwanawe, Yesu Kristo.

Chapisha