Agano Jipya 2023
Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia


“Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia,Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023 (2022)

“Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia,Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2023

Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia

Nyenzo Hii Ni Kwa Ajili ya Nani?

Nyenzo hii ni kwa ajili ya kila mtu binafsi na familia katika Kanisa. Imekusudiwa ili kukusaidia wewe kujifunza injili—iwe peke yako au na familia yako. Kama hujajifunza injili mara kwa mara hapo awali, nyenzo hii inaweza kukusaidia kuanza. Kama tayari una mazoea mazuri ya kujifunza injili, nyenzo hii inaweza kukusaidia kupata uzoefu mwingi wa maana.

Picha
mume na mke wakijifunza maandiko

Je, Ni Kwa Namna Gani Ninapaswa Kuitumia Nyenzo Hii?

Tumia nyenzo hii katika njia yoyote ambayo ina manufaa kwako. Unaweza kuona ina manufaa kama mwongozo au msaada wa kujifunza maandiko kwako binafsi na kifamilia. Unaweza pia kuitumia kwa ajili ya jioni ya familia nyumbani. Mihutasari huonyesha kanuni muhimu zinazopatikana ndani ya Agano Jipya, hupendekeza mawazo ya kujifunza na shughuli kwa ajili ya watu binafsi na familia, na hutoa sehemu za kuandika mawazo yako.

Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia haikusudiwi kuwa mbadala au kushindana na mambo mazuri unayofanya ili kujifunza injili. Fuata mwongozo wa Roho ili kuamua jinsi ya kuanza kujifunza kwako mwenyewe neno la Mungu.

Ni Kwa Jinsi Gani Nyenzo Hii Inahusiana na Kile Kinachotokea Kanisani?

Mihutasari katika nyenzo hii imepangwa kulingana na ratiba ya kusoma kila wiki. Nyenzo ya Njoo, Unifuate kwa ajili ya Msingi, kwa ajili ya Shule ya Jumapili, na kwa ajili ya madarasa ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana hufuata ratiba hiyo hiyo. Ili kusaidia juhudi zako za kujifunza na kuishi injili nyumbani, walimu wako kanisani watakupa fursa za kushiriki uzoefu wako, mawazo, na maswali kuhusu vifungu vya maandiko ambavyo umekuwa ukijifunza ukiwa nyumbani.

Kwa sababu Shule ya Jumapili inafundishwa mara mbili tu kwa mwezi, walimu wa Shule ya Jumapili wanaweza kuchagua kuunganisha au kuacha mihutasari ili kwenda sambamba na ratiba ya kila wiki. Hii yaweza pia kuwa ya muhimu (kwa zote Shule ya Jumapili na Msingi) katika wiki ambapo mikutano ya kawaida ya Kanisa haifanyiki kwa sababu ya mkutano wa kigingi au kwa sababu nyinginezo. Katika muda wa wiki hizi unaalikwa kuendelea kujifunza Agano Jipya nyumbani.

Je, Ninahitaji Kufuata Ratiba?

Ratiba itakusaidia wewe uwe umesoma Agano Jipya kufikia mwisho wa mwaka. Kwa kuongezea, kufuata ratiba hiyo hiyo kama wengine kunaweza kuongoza kwenye uzoefu wa maana nyumbani, kanisani, na kwingineko. Lakini usijisikie kufungwa na ratiba au kulazimishwa kusoma kila mstari; ratiba ni mwongozo wa kukusaidia kirahisi kujipima mwenyewe. Kitu muhimu ni kwamba wewe unajifunza injili kama mtu binafsi na kama familia.

Chapisha