Agano Jipya 2023
Nyenzo za Ziada


“Nyenzo za Ziada,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023 (2022)

“Nyenzo za ziada,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2023

familia ikijifunza maandiko

Nyenzo za Ziada

Nyenzo hizi zinaweza kupatikana katika Programu ya Maktaba ya Injili kwenye ChurchofJesusChrist.org.

Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto

Muziki mtakatifu humwalika Roho, hutusaidia kuhisi upendo wa Mungu, na hufundisha injili katika njia ya kukumbukwa. Katika kuongezea kwenye kutumia matoleo yaliyochapishwa ya Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto, unaweza kupata rekodi za sauti na video za nyimbo nyingi za kanisa na nyimbo za watoto kwenye music.ChurchofJesusChrist.org na katika programu za Muziki Mtakatifu na Vyombo vya Habari vya Injili.

Vitabu vya Kiada vya Seminari na Chuo

Vitabu vya Kiada vya Seminari na Chuo hutoa chimbuko la kihistoria na maoni ya kimafundisho kwa kanuni na matukio yanayopatikana katika maandiko.

Magazeti ya Kanisa

Magazeti ya Rafiki, Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, na Liahona hutoa hadithi na shughuli ambazo zinaweza kuwa nyongeza kwenye kanuni unazofundisha kutoka katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia.

Mada za Injili

Kwenye Mada za Injili (topics.ChurchofJesusChrist.org), unaweza kupata taarifa muhimu kuhusu mada mbali mbali za injili, pamoja na viunganishi kwenye nyenzo saidizi kama vile hotuba za mkutano mkuu, makala, maandiko, na video zinazoshabihiana. Unaweza pia kupata Insha za Mada za Injili, ambazo hutoa taarifa za kina kuhusu masuala ya kimafundisho na ya kihistoria, vile vile majibu ya maswali tofauti tofauti kuhusu Kanisa na mafundisho yake.

Hadithi za Agano Jipya

Hadithi za Agano Jipya zinaweza kuwasaidia watoto kujifunza mafundisho na hadithi zilizopatikana katika Agano Jipya. Unaweza pia kupata video za hadithi hizi katika Programu ya Maktaba ya Injili na kwenye GospelMedia.ChurchofJesusChrist.org.

Kitabu cha Hadithi za Maandiko cha Kupaka Rangi—Agano Jipya

Nyenzo hii ina kurasa za burudani za shughuli ya kupaka rangi zilizosanifiwa ili kuongeza hamu ya kujifunza kwa watoto kutoka kwenye Agano Jipya.

Video na Sanaa

Kazi ya sanaa, video, na vyombo vingine vya habari vinaweza kuisaidia familia yako kuelewa mafundisho na kuvuta taswira ya hadithi zenye uhusiano na maandiko. Tembelea Vyombo vya Habari vya Injili katika GospelMedia.ChurchofJesusChrist.org ili kuvinjari mkusanyiko wa nyenzo za habari za Kanisa. Vyombo vya Habari vya Injili pia vinapatikana kama programu ya simu ya mkononi. Picha nyingi ambazo unaweza kutumia zinapatikana katika Kitabu cha Sanaa ya Injili.

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi kunaweza kukusaida kujifunza kuhusu, na kutumia kanuni za kufundisha kama Kristo.