“Mawazo ya Kuweka Akilini: Manabii na Unabii,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)
“Mawazo ya Kuweka Akilini: Manabii na Unabii,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022
Mawazo ya Kuweka Akilini
Manabii na Unabii
Katika mgawanyiko wa jadi wa Kikristo wa Agano la Kale, sehemu ya mwisho (Isaya hadi Malaki) inaitwa “Manabii.”1 Sehemu hii, karibu theluthi moja ya Agano la Kale, ina maneno ya watumishi wa Mungu walioidhinishwa, ambao walizungumza na Bwana na kisha wakazungumza kwa ajili Yake, wakishiriki ujumbe Wake na watu kati ya karibu 900 na 500 KK.2
Manabii na unabii unachukua nafasi kubwa katika Agano la Kale lote. Mapatriaki Ibrahamu, Isaka, na Yakobo waliona maono na wakazungumza na wajumbe wa mbinguni. Musa aliongea na Mungu uso kwa uso na aliwasilisha mapenzi yake kwa wana wa Israeli. Vitabu vya Wafalme wa Kwanza na wa Pili vinaelezea kazi za kukumbukwa na jumbe za manabii Eliya na Elisha. Agano la Kale pia linazungumzia juu ya manabii kama Miriamu (ona Kutoka 15:20) na Debora (ona Waamuzi 4), pamoja na wanawake wengine waliobarikiwa na roho wa unabii (ona Mwanzo 25:21–23) na Hana (ona 1 Samweli 1:20–2:10). Na ingawa Zaburi hazijaandikwa na manabii rasmi, nazo pia zimejazwa na roho wa unabii, haswa zinapotarajia kuja kwa Masiya.
Hakuna kati ya hili linakuja kama kitu cha kushangaza kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho. Kwa kweli, injili ya urejesho ya Yesu Kristo inatufundisha kwamba manabii sio tu sehemu ya kuvutia ya historia lakini ni sehemu muhimu ya mpango wa Mungu. Wakati wengine wanaweza kuwaona manabii kama wa kipekee kwa nyakati za Agano la Kale, sisi tunawaona kama wa kawaida na nyakati za Agano la Kale.
Hata hivyo, kusoma sura kutoka kwa Isaya au Ezekieli unaweza kuhisi tofauti na kusoma ujumbe wa mkutano mkuu kutoka kwa Rais wa sasa wa Kanisa. Wakati mwingine inaweza kuwa vigumu kuona kwamba manabii wa kale walikuwa na kitu cha kusema nasi. Kwa maana, ulimwengu tunaoishi leo ni tofauti sana na ule ambao walihubiri na kutabiri. Na ukweli kwamba tunaye nabii aliye hai kunaweza kuleta swali: kwa nini inafaa kuweka juhudi—na inahitaji juhudi—kusoma maneno ya manabii wa kale?
Wana kitu cha kusema nasi
Kwa sehemu kubwa, watu leo sio hadhira ya msingi ya manabii wa Agano la Kale. Manabii hao walikuwa na matatizo ya haraka waliyoyaongelea katika nyakati zao na wakati wao—kama vile manabii wetu wa siku za mwisho wanavyoongelea matatizo yetu ya haraka ya leo.
Wakati huo huo, manabii wanaweza pia kutazama zaidi ya shida za wakati huu. Kwanza, wanafundisha kweli za milele, zinazohusiana na umri wowote. Na, wakibarikiwa na ufunuo, wanaona taswira kubwa, mtazamo mpana wa kazi ya Mungu. Kwa mfano, Isaya hakuweza tu kuwaonya watu wa siku zake juu ya dhambi zao—pia angeweza kuandika juu ya ukombozi kwa Waisraeli wanaoishi miaka 200 baadaye na wakati huo huo kufundisha juu ya ukombozi ambao watu wote wa Mungu wanautafuta. Kwa nyongeza, angeweza kuandika unabii ambao, hata leo, bado unasubiri utimilifu wake—kama ahadi za “nchi mpya” (Isaya 65:17) ambao “dunia itajawa na kumjua Bwana” (Isaya 11:9), ambako makabila yaliyopotea ya Israeli wamekusanyika na ambako “mataifa” “hawatajifunza vita tena kamwe.” (Isaya 2:4). Sehemu ya furaha na msukumo unaotokana na kusoma maneno ya manabii wa Agano la Kale kama Isaya ni kutambua kwamba sisi tunachukua jukumu katika siku tukufu waliyoiota.3
Kwa hivyo unaposoma unabii wa zamani, ni muhimu kujifunza juu ya muktadha ambao uliandikwa. Lakini unapaswa pia kujiona kuwa ndani yao, au “uwalinganishe na wewe mwenyewe],” kama Nefi alivyosema (ona 1 Nefi 19:23–24). Wakati mwingine hiyo inamaanisha kuitambua Babeli kama ishara ya ulimwengu na kiburi, sio tu kama jiji la kale. Inaweza kumaanisha kuielewa Israeli kama watu wa Mungu katika enzi yoyote na kuelewa Sayuni kama siku ya mwisho husababisha watu wa Mungu kuikumbatia, badala ya kama neno lingine tu kwa Yerusalemu.
Tunaweza kulinganisha maandiko kwa sababu tunaelewa kuwa unabii unaweza kutimizwa kwa njia nyingi.4 Mfano mzuri wa hii ni unabii katika Isaya 40:3: “Sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya Bwana.” Kwa Wayahudi waliotekwa nyara huko Babeli, taarifa hii inaweza kuwa ilimaanisha Bwana kutoa njia ya kutoka utumwani na kurudi Yerusalemu. Kwa Mathayo, Marko, na Luka, unabii huu ulitimizwa katika Yohana Mbatizaji, ambaye aliandaa njia ya Mwokozi ya huduma ya mwili wa kufa.5 Na Joseph Smith alipokea ufunuo kwamba unabii huu bado unatimizwa katika siku za mwisho kwa kujiandaa kwa huduma ya Kristo ya milenia.6 Kwa njia ambazo bado tunakuja kuelewa, manabii wa kale walivyo zungumza nasi. Na walifundisha kweli nyingi za thamani, kweli za milele ambazo zinafaa kwetu kama zilivyokuwa kwa Israeli ya kale.
Walishuhudia juu ya Yesu Kristo.
Labda muhimu zaidi kuliko kujiona katika unabii wa Agano la Kale ni kumwona Yesu Kristo ndani yao. Kama ukimtafuta, utampata Yeye, hata ikiwa Yeye hajatajwa kwa jina. Inaweza kusaidia kukumbuka kuwa Mungu wa Agano la Kale, Bwana Yehova, ni Yesu Kristo. Wakati wowote manabii wanaelezea kile ambacho anakifanya Bwana au kile Atakachofanya, wanazungumza juu ya Mwokozi.
Pia utapata marejeo kwa Mtiwa Mafuta (ona Isaya 61:1), Mkombozi (ona Hosea 13:14), na Mfalme ajaye kutoka uzao wa Daudi (ona Isaya 9:6–7; Zekaria 9:9). Huu wote ni unabii kuhusu Yesu Kristo. Kwa jumla zaidi, utasoma juu ya wokozi, msamaha, ukombozi, na urejesho. Ukiwa na Mwokozi akilini mwako na moyoni mwako, unabii huu kwa kawaida utakuelekeza kwa Mwana wa Mungu. Zaidi ya yote, njia bora ya kuelewa unabii ni kuwa na “roho ya unabii,” ambayo Yohana anatuambia ni “ushuhuda wa Yesu” (Ufunuo 19:10).